Vipi kama pesa ya wizi ndiyo inatumika kulisha na kuendesha familia?
Kushindwa kwa upinzani mie naamini kabisa ni SERA ndizo zinawashinda kuzitumia ,hawa wapinzani wamekua kama CCM kuamuka tu siku za uchaguzi na kuanza kupaa na madege angani huku wakisahau kua CCM wamejijenga toka zama zile hivyo kupaa kwa kipindi cha miezi kadhaa kubadirisha kilichojengeka vichwani kwa miaka kadhaa ni ngumu.
Na ili ubadirishe kilichokwisha jengeka kichwani ni lazima umu shawishi mtu husika kwa matendo mfano tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi ule mkuu wangejikita zaidi ktk maendeleo ya jamii mfano kwa hizo harambee na kutafuta wadhamini kuwapelekea huduma wananchi ya maji/umeme
kufanya harambee kuwajengea watu wanaoenda maili kadhaa kutafuta disipensari .
kufanya ma harambee na kutafuta wadhamini kujenga vyuo vikuu vya kutosha na vitu vingine vya namna hiyo.
Hapo wananchi watakua wameona nini maana ya upinzani na nini kinafanya na hapo ndipo kitakua kimejikita vichwani mwa wananchi.
Unajua kuna fomula moja ukitaka kushindana na mtetea taji unatakiwa uweke mikakati ya kumshinda kwelikweli hata asipate feva yoyote ambayo anaweza pata.
Huku kuja kuuza sera dakika za majeruhi tena kwa maneno matupu si njia muafaka Je tutaamini vipi hizo sera kama sio za kiulaghai?? Je wapinzani wapewe tu kwa vile wanaongea maneno matamu?? Je wewe unaweza kuamini mtu kwa maneno yake tu??
Wapinzani wabadirishe jinsi ya kupeperusha bendera vinginevyo ndiyo kama hayo ya kiteto na ya Mrema mwaka 1995.
Huwezi kutumia wizi wa watu wachache ukasema ni chama ,chama sio physical entity ambacho kinaweza iba kitu.
Mfano ktk familia ya watu 8 mmoja kati yao anaweza akawa mjinga lakini huwezi sema familia ile ni jinga.
Failure ya tanzania sio ya CCM as CCM ila ya familia nzima yani watanzania.
Wapinzani wangapi wametulaghai wakati ule kwamba wao ni wema wamekimbia ccm maana ni chama kibaya leo hii NDIO viongozi na wafuasi wazuri wa CCM Je tutafahamu vipi huyu ni mlaghai,huyu ni propaganda ,huyu ni mtafuta madaraka??? kwa maneno matupu?? lahasha.
Haya mambo ya kuibua skendo si hoja kabisa ya kumfanya mtu apewe madaraka,kwani skendo hizi zimeanza kuibuliwa na wapinzani mbona mbunge wa CCM kama sikosei ni Mzee ndakaya ama kingunge ameibua skendo ngapi amefukuzisha mawaziri wangapi??
Kawaida ya mnafiki hua anakumonita tu ndg Kitila sehemu utapokesea ili ukumalize lakini mara kwa bahati mbaya juhudi za namna hii hua hazifanikiwi