Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
umaskini kwa kwenda mbele,endeleeni tuu kuwachagua ila msije hapa mnalia Buzwagi wala BOT na Richmond...miaka karibu 50 ya uhuru hakuna umeme wala maji,sanasana ni rushwa tuu na wizi,mungu awasaidie kuwaonyesha njia maana hiyo ni disease.

Koba,

Nadhani unaifahamu 409 na the story behind it!
 
Nashindwa kuwaelewa watu ambao bado wanaipigia kura CCM.

Baada ya maskendo yote haya,je hawa watu hawaoni?

Je ni kitu gani CCM imewafanyia?

Nimechanganyikiwa !

..rubabi,

..pale walikuwa wanachagua chama au walikuwa wanachagua mwakilishi wao bungeni?

..au tanzania hatuna akili kiasi hichi?
 
Unajua wapinzani hawana sera hichi kibano wakizoee mpaka siku ile watakapobadirika na sera zao.
watu hatuoni kwanini wapewe CHADEMA/CUF/NCCR ambao hawafahamiki namna ya uendeshaji wao.

Hata wewe mkuu? Nilitegemea uwe critical kidogo kwa jinsi ninavyokujua. Yaani wewe kweli unaamini wapinzani wameshindwa kwa sababu ya sera? Hujiuliza ni kwa nini wananchi wameandamana maelefu kwa maelfu na kumshangilia sana Lowasa wakati sisi hapa wote tumekuwa tukimuona Lowasa ndio kiongozi wa ufisadi nchini mwetu? Hebu tulia kidogo, achana na ushabiki cheap na ujiulize zaidi, najua kabisa kwa jinsi ninavyokujua unaweza kufanya bora zaidi ya hapo!
 
umaskini kwa kwenda mbele,endeleeni tuu kuwachagua ila msije hapa mnalia Buzwagi wala BOT na Richmond...miaka karibu 50 ya uhuru hakuna umeme wala maji,sanasana ni rushwa tuu na wizi,mungu awasaidie kuwaonyesha njia maana hiyo ni disease.

..koba,

..point ya muhimu si kukichagua chama,bali kuchagua mtu anayefaa.

..sasa,labda tujadili huyu wa chadema alichomzidi wa ccm ni nini!

..kwani,waliowachagua kina mwakyembe and company walikosea? simply kwasababu wao ni ccm?
 
Nashindwa kuwaelewa watu ambao bado wanaipigia kura CCM.

Baada ya maskendo yote haya,je hawa watu hawaoni?

Je ni kitu gani CCM imewafanyia?

Nimechanganyikiwa !

You are a very good Joker, nafikiri ungewaambia wananchi wa Kiteto maneno haya kabla ya kura kupigwa, maana unadhani wananchi wa Kiteto ni mambumbumbu.

Kimsingi, kati ya mgombea wa CCM na CHADEMA, mgombea wa CCM alikuwa anakubalika zaidi ya mgombea wa CHADEMA. Huenda kama CHADEMA ama upinzani ungemsimamisha mtu anayekubalika zaidi labda matokeo yangekuwa tofauti na yalivyokuwa.

HONGERA CCM, WAPINZANI ENDELEENI KUJIPANGA YA KITETO NI HISTORIA SASA.
 
Hata wewe mkuu? Nilitegemea uwe critical kidogo kwa jinsi ninavyokujua. Yaani wewe kweli unaamini wapinzani wameshindwa kwa sababu ya sera? Hujiuliza ni kwa nini wananchi wameandamana maelefu kwa maelfu na kumshangilia sana Lowasa wakati sisi hapa wote tumekuwa tukimuona Lowasa ndio kiongozi wa ufisadi nchini mwetu? Hebu tulia kidogo, achana na ushabiki cheap na ujiulize zaidi, najua kabisa kwa jinsi ninavyokujua unaweza kufanya bora zaidi ya hapo!

..kitila,

..wapinzani[au vyama vingine nchini]vina kazi kubwa ya kujipanga kiuongozi[kwa kuwa na viongozi bora zaidi] na kimkakati wa kukuza vyama vyao na kujijenga kwenye mashina. bado kazi ngumu.

..issue ya lowassa ni suala la muda tu! tik tak tik tak!
 
Nashindwa kuwaelewa watu ambao bado wanaipigia kura CCM.

Baada ya maskendo yote haya,je hawa watu hawaoni?

Je ni kitu gani CCM imewafanyia?

Nimechanganyikiwa !

Rubabi,

Haya mambo ni taratibu na soon watu wakianza kuhamishwa toka kwenye nyumba zao kupisha Barrick na wenzake watumie ardhi hiyo kwa manufaa ya mgodi wa Buzwagi (kumbuka mkataba wa Buzwagi unaipa Barrick mamlaka ya kuchukua na kutumia ardhi, maliasili, vyanzo vya maji, na chochote Tanzania ambacho kitasaidia shughuli zake za uchimbaji madini).

Otherwise, una haki ya kuchanganyikiwa mkuu na pole sana. Ukiwa unakimbia ukijikwaa ukaanguka au ukisukumwa na mwenzio na ukaanguka, basi the best you do ni kuamka na kujifuta mavumbi na kuendelea na safari.
 
Chadema wanapaswa kuondokana na upuuzi wa kudhani kuwaonyesha wananchi 'helikopta' ndio mvuto mkubwa wananchi wawape kura. If anything, this in itself should be reason enough to vote against them.

Nakubaliana na mawazo ya Mkjj. Kila uchaguzi unategemea umejipanga vipi, na ni mikakati ipi umeiweka kufanikisha azma yako ya uchaguzi. Je, unawajua vizuri wapiga kura wako? Unayajua vizuri mahitaji yao?

Huwezi kwenda tu kuomba kura kwa kelele za jukwaani. Mgombea wa Chadema alishagalagazwa mara kadhaa katika jimbo hilo hilo. Je, kabla ya kumteua tena kugombea mara nyingine, walijiuliza ni sababu zipi zilizokuwa zinamfanya ashindwe; na kama walizijua, ni yapi waliyokuwa wameyafanya safari hii ili aweze kukubalika zaidi!

Chadema, kama chama inawabidi pia wakae chini ili wajitazame upya. Their top leadership may not be inspiring enough to the wananchi.

Kalamu, simplicity is the enemy of truth. Unarahisisha mambo mno hapa. Helicopter haiwezi kuwa moja ya sababu za CHADEMA kushindwa. Una uhuru wa kushangilia ushindi wa CCM lakini huna haki ya kupotosha mambo kwani hujafanya utafiti wowote wa kisayansi wa kukuwezesha kufikia hitimisho kubwa kama hili. Wote tulikiri hapa kwamba CHADEMA walitekeleza wajibu wao, wamewaeleza wananchi kwa nini wawachagua wao na sio CCM, wamefanya bidii kubwa hata matokeo yanaonyesha hivyo lakini walizidiwa kura na CCM. Sasa kwa vyovyote tatizo haliwezi kuwa upande wa CHADEMA pekee. The problem here is bigger than you seem to suggest. Clue mojawapo ya kuangalia ni hii; inawezekanaje wananchi, watanzania hawahawa wamshangilia Lowasa kwa kiwango tulichoshuhudia, mtu ambaye tumemzomea kila kona kwamba ni fisadi? Sasa hapa lazima ujue kwamba upeo wetu wa kuona mambo ni tofauti sana na wananchi. Narudia tena tatizo hapa ni kubwa zaidi kuliko unavyotaka tuamini hapa.
 
Mie naona udhaifu wa wapinzani ni huu mtindo wao eti kuibua uozo wa mwazako na kuufanya SERA,kuibua uozo ni vyema lakini kuufanya ndio mgongo wa kupandia ni makosa makubwa ,hii naifananisha kama mtu yule anayemtaka mwanamke kwa gia za kumuambia maovu ya mwanaume aliyenaye.Mwanaumme aliyenaye anaweza akawa muovu sana lakini wewe kupitia mgongo huo ili ufanikishe adhima yako na kama mwanamke huyo ni makini hakika hutompata

Na hii ndio ilikuwa inawafanya akina Mzee MwanaKijiji Kuamini kwamba watashinda Kiteto... bila hiyo wasingefikiri hivyo... sasa wasijue wamasai walikuwa wanachagua mwakilishi wao wa Jimbo la Kiteto sio mtambo wa kutoa na kuvurumisha mabomu... na wamasai sio watu wanafiki... ni miongoni mwa makabila yenye kusema na kutenda kweli... well exception wacheche....
 
..kitila,

..wapinzani[au vyama vingine nchini]vina kazi kubwa ya kujipanga kiuongozi[kwa kuwa na viongozi bora zaidi] na kimkakati wa kukuza vyama vyao na kujijenga kwenye mashina. bado kazi ngumu.

..issue ya lowassa ni suala la muda tu! tik tak tik tak!

I agree. Picha ambayo naanza kuipata ni kwamba kuna mambo ambayo sisi tunafikri ni matatizo wananchi wa kawaida hawaoni kama ni shida. Kwa mfano, hili swala la ufisadi sidhani kama watanzania wa maeneo ya Kiteto na kwingineko wanafikiri ni matatizo yanayowahusu. Yaani hawawezi kuoanisha kabisa kati ya shida walizo nazo na wizi wa pesa za serikali unaofanywa na CCM. Vinginevyo isingewezekana waichague CCM au kumshangilia Lowasa kwa kiwango tulichoona. Hapa ndipo nitakubaliana na Einstein kwamba "Siasa ni Ngumu Kuliko Fizikia"!
 
Hata wewe mkuu? Nilitegemea uwe critical kidogo kwa jinsi ninavyokujua. Yaani wewe kweli unaamini wapinzani wameshindwa kwa sababu ya sera? Hujiuliza ni kwa nini wananchi wameandamana maelefu kwa maelfu na kumshangilia sana Lowasa wakati sisi hapa wote tumekuwa tukimuona Lowasa ndio kiongozi wa ufisadi nchini mwetu? Hebu tulia kidogo, achana na ushabiki cheap na ujiulize zaidi, najua kabisa kwa jinsi ninavyokujua unaweza kufanya bora zaidi ya hapo!

Mkuu kopi na u pesiti maada yote maana ukipesti kijimstari haitaeleweka vizuri.

Mkuu mie sio mshabiki wa chama chochote ila nipo mshabiki wa mustakbali wa taifa letu.

Kushindwa kwa upinzani mie naamini kabisa ni SERA ndizo zinawashinda kuzitumia ,hawa wapinzani wamekua kama CCM kuamuka tu siku za uchaguzi na kuanza kupaa na madege angani huku wakisahau kua CCM wamejijenga toka zama zile hivyo kupaa kwa kipindi cha miezi kadhaa kubadirisha kilichojengeka vichwani kwa miaka kadhaa ni ngumu.

Na ili ubadirishe kilichokwisha jengeka kichwani ni lazima umu shawishi mtu husika kwa matendo mfano tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi ule mkuu wangejikita zaidi ktk maendeleo ya jamii mfano kwa hizo harambee na kutafuta wadhamini kuwapelekea huduma wananchi ya maji/umeme

kufanya harambee kuwajengea watu wanaoenda maili kadhaa kutafuta disipensari .

kufanya ma harambee na kutafuta wadhamini kujenga vyuo vikuu vya kutosha na vitu vingine vya namna hiyo.

Hapo wananchi watakua wameona nini maana ya upinzani na nini kinafanya na hapo ndipo kitakua kimejikita vichwani mwa wananchi.

Unajua kuna fomula moja ukitaka kushindana na mtetea taji unatakiwa uweke mikakati ya kumshinda kwelikweli hata asipate feva yoyote ambayo anaweza pata.

Huku kuja kuuza sera dakika za majeruhi tena kwa maneno matupu si njia muafaka Je tutaamini vipi hizo sera kama sio za kiulaghai?? Je wapinzani wapewe tu kwa vile wanaongea maneno matamu?? Je wewe unaweza kuamini mtu kwa maneno yake tu??

Wapinzani wabadirishe jinsi ya kupeperusha bendera vinginevyo ndiyo kama hayo ya kiteto na ya Mrema mwaka 1995.
 
Hapa ndipo nitakubaliana na Einstein kwamba "Siasa ni Ngumu Kuliko Fizikia"!

Kitila Mkumbo,

Nakubaliana nawe, lakini tujiulize pale makao makuu ya CHADEMA -Kinondon, Dar es Salaam... Neno "Kiteto" limeanza kutamkwa mara nyingi lini kama sio juzi wakati Mh. Mbunge wa kule alivyofariki...

Mimi nadhani niwapongeze wananchi wa Kiteto kwa sababu moja, kura sio za kuchukuliwa kirahisi tu, you have to be close to them!!! haiwezekani miezi miwili ya kuona helikopta iwe ndio kigezo cha kupewa kura, au kashfa ya Buzwagi, BOT, etc... udhani wapinzani wasafi pia... NARC ilivyoingia madarakani Kenya kwani ilifanya nini?

Tunahitaji chama tawala imara kinacho-be closely monitored.

Kwa vyovyote vile wewe uliosoma science, kweli siasa ni rocket science... that what I can say!!!
 
I agree. Picha ambayo naanza kuipata ni kwamba kuna mambo ambayo sisi tunafikri ni matatizo wananchi wa kawaida hawaoni kama ni shida. Kwa mfano, hili swala la ufisadi sidhani kama watanzania wa maeneo ya Kiteto na kwingineko wanafikiri ni matatizo yanayowahusu. Yaani hawawezi kuoanisha kabisa kati ya shida walizo nazo na wizi wa pesa za serikali unaofanywa na CCM. Vinginevyo isingewezekana waichague CCM au kumshangilia Lowasa kwa kiwango tulichoona. Hapa ndipo nitakubaliana na Einstein kwamba "Siasa ni Ngumu Kuliko Fizikia"!

Taratibu tu Kitila,

watu hujifunza kwa makosa na kadri muda unavyoenda wapenda maendeleo watajua nini cha kufanya ili wawatoe mafisadi toka madarakani kwa kura.

Nimependa comment ya memba mmoja aliyesema kuwa ushindani kwenye uchaguzi unahitaji strategy ya kushinda ambayo so far sisiemu wanajua vyema namna ya kuitumia.

Huu ni mwanzo na taratibu tu kitaeleweka.
 
Nilisema zamani hivi vyama vya upinzani viwachane na mambo ya kupiga kura ,waelekeze majeshi kwenye Katiba ya Nchi na tume ya Uchaguzi ,halafu mambo hayo yakishakuwekwa sawa basi hata mkuu wa Chama kama anatumika kuiunganishia CCM itakuwa vigumu kwani hata wapiga kura wanaonekana kusononeka ni kwa namna gani wameshindwa ,ukweli mchozo upo ndani ya tume ya Uchaguzi hakuna jengine haiwezekani CCM wakamate mpini na wapinzani wamekamata makali halafu mushangae kwa nini CCM hakukatika mikono itakuwa miujiza.
 
Haya jamani...kwa wale waliohsinda na kushindwa basi ingekuwa vyema tusahau ya kiteto na turudi kwenye hoja zetu kubwa...na si zingine zinasohusu mafisadi....

Sioni kama hapa kama kuna haja ya kushangilia au kusikitika...cha muhimu tujiulize...je haya yote yanayotokea leo...mtanzania wa hali ananufaika vipi....

Jimbo la kiteto ni moja tu kati ya majimbo ya uchaguzi hapa Tanzania...nguvu iliyotumika tumeiona...karibu nchi nzima iliamia uko...sema mkuu wa kaya alikuwa na mambo mengi bila shaka naye angeenda kwenye kampeni uko...sasa kama ikitokea zikaja chaguzi 20 kwa mpigo si itakuwa patashika...

Kwa aliyeshinda...ajiulize ameshindaje...na je akiangalia hali ya wana kiteto inaridhisha kuweza kujigamba hata kama wamenichagua nitaweza kuwasaidia kutatua matatizo yao ya muhimu. Na yule aliyeshindwa ajiulize nini kimepelekea ikawa hivyo na ana mipango ipi ya kujikwamua....

Yote tisa....kumi ni kurudi kwenye ajenda zetu muhimu zinazogusa watu karibia ya 38,000,000 na si nyingine....UFISADI, UFISADI, UFISADI...maana ili la kiteto linaweza kuwafanye wengine wazimike kabisa na wale waliokuwa wanazidiwa katika kujenga hoja waweze kutamba hapa....

Turudi kweny mjadala wa UFISADI...maaana tukikalia ya Kiteto mengi yaweza kutupita....
 
Kitila Mkumbo,

Nakubaliana nawe, lakini tujiulize pale makao makuu ya CHADEMA -Kinondon, Dar es Salaam... Neno "Kiteto" limeanza kutamkwa mara nyingi lini kama sio juzi wakati Mh. Mbunge wa kule alivyofariki...

Mimi nadhani niwapongeze wananchi wa Kiteto kwa sababu moja, kura sio za kuchukuliwa kirahisi tu, you have to be close to them!!! haiwezekani miezi miwili ya kuona helikopta iwe ndio kigezo cha kupewa kura, au kashfa ya Buzwagi, BOT, etc... udhani wapinzani wasafi pia... NARC ilivyoingia madarakani Kenya kwani ilifanya nini?

Tunahitaji chama tawala imara kinacho-be closely monitored.Kwa vyovyote vile wewe uliosoma science, kweli siasa ni rocket science... that what I can say!!!

Kasheshe unategea monitoring itatoka wapi kama upande mmoja umeamua kuwa ushindi ni wa lazima kwa gharama yoyote.
 
Wa town wako kama 99% ya wana JF ambao wanajua mambo .Hawajali Chama ila wanataka kuona Nchi yao inasonga mbele kwa maendeleo.Leo ukiweka kura JF naamini CCM hawataona ndani na ushahidi umeuona hata Mwema na kundi lake wakaamuwa kuwamata vijana wetu kwa sababu ambazo sizijui wala wewe .Wajanja wote wanaokataa CCM .Ukimuona mjanja anaipenda CCM jua yuko highly connected na UFISADI .

Kalamu, simplicity is the enemy of truth. Unarahisisha mambo mno hapa. Helicopter haiwezi kuwa moja ya sababu za CHADEMA kushindwa. Una uhuru wa kushangilia ushindi wa CCM lakini huna haki ya kupotosha mambo kwani hujafanya utafiti wowote wa kisayansi wa kukuwezesha kufikia hitimisho kubwa kama hili. Wote tulikiri hapa kwamba CHADEMA walitekeleza wajibu wao, wamewaeleza wananchi kwa nini wawachagua wao na sio CCM, wamefanya bidii kubwa hata matokeo yanaonyesha hivyo lakini walizidiwa kura na CCM. Sasa kwa vyovyote tatizo haliwezi kuwa upande wa CHADEMA pekee. The problem here is bigger than you seem to suggest. Clue mojawapo ya kuangalia ni hii; inawezekanaje wananchi, watanzania hawahawa wamshangilia Lowasa kwa kiwango tulichoshuhudia, mtu ambaye tumemzomea kila kona kwamba ni fisadi? Sasa hapa lazima ujue kwamba upeo wetu wa kuona mambo ni tofauti sana na wananchi. Narudia tena tatizo hapa ni kubwa zaidi kuliko unavyotaka tuamini hapa.

WAKUU KITILA NA LUNYUNGU,
WITH DUE RESPECT, PAMOJA NA MAPENZI MLIYONAYO KWA CHADEMA TUKUBALIANE KUWA MZEE KIMESERA HAKUWA MGOMBEA BORA KUTOKA KATIKA KAMBI YA UPINZANI, ALIKUWA NI 'BORA MGOMBEA'. KILICHOFANYIKA KUMTEUA MZEE KIMESERA SIYO OVERSIGHT, BALI INAONYESHA SIASA ZA UBWANYENYE ZILIVYOSHEHENI NDANI YA CHADEMA. WATU KADHAA WAMEKUWA WANALIONA HILI NA WANAJARIBU KULISEMA FROM TIME TO TIME LAKINI INAONEKA KUVUNJA BARRIERS ZILIZOPO ZA UBWANYENYE NDANI YA CHADEMA NI SAWASAWA NA KUJIFUNGULIA MLANGO WA KUTOKA NJE. YANAHITAJIKA MAPINDUZI YA KWELI NDANI YA CHADEMA LAKINI JE, NANI YUKO TAYARI KUMFUNGA PAKA KENGELE? MWENYEKITI MBOWE HAWEZI KULETA MAPINDUZI YA KWELI NDANI YA CHADEMA KWA SABABU YEYE ANATOKA NA MFUMO WA MABWANYENYE.
KIPINDI HIKI TULICHONACHO NI WAKATI MUAFAKA KWA CHADEMA KUJIIMARISHA KIUONGOZI NA KUTOA SURA YA KUWA NI CHAMA CHA WANANCHI ZAIDI YA WANACHAMA HII ITASAIDIA KUONDOA UBWANYENYE NDANI YA CHAMA.
 
You

Kimsingi, kati ya mgombea wa CCM na CHADEMA, mgombea wa CCM alikuwa anakubalika zaidi ya mgombea wa CHADEMA. Huenda kama CHADEMA ama upinzani ungemsimamisha mtu anayekubalika zaidi labda matokeo yangekuwa tofauti na yalivyokuwa.

Ndio nasema hoja zetu nyingi zimejengwa katika misingi ya hisia kiasi kwamba inakuwa vigumu sana kutoa counter-argument. Angalau kwa habari ambazo tulikuwa tunasoma kwenye magazeti tunajua hili sio kweli. Sio kweli kwa sababu huyu mgombea wa CCM alikuwa hawezi kabisa kuongea na ilifika mahala akipanda jukwaani wananchi wanamzomea. Siku za mwisho za kampeni ilibidi viongozi wa CCM waache kumsimamisha jukwaani ili kuepuka aibu ya kuzomewa. Kwa hiyo kimsingi wananchi wale wamechagua chama zaidi kuliko mgombea. Hii pia inajibu hoja ya Kasheshe.

Tunatambua sana kwamba hii biashara ya kujenga chama mbadala haitakuwa rahisi maana tunapambana na chama ambacho kimejijengea sura ya unchi kwa muda mrefu kwa juhudi zetu sote. Sasa tunachotarajia kutoka kwa colleagues kama JF members sio kejeli bali kutiwa moyo ili tuendelee na mapambano. Ndiyo CHADEMA wameshindwa Kiteto; lakini tutakuwa naive kukataa ukweli kwamba walipambana na juhudi hizo zinajionyesha katika idadi ya kura walizopata. Ni kweli pia kwamba lazima CHADEMA na upinzani kwa ujumla wajipange vizuri zaidi kwa ajili ya chaguzi zijazo na pengine kubadilisha mbinu na tunashukuru kwa wale wanaotoa mchango wa namna ya kuisadia CHADEMA ijipange. Tunapokea vijembe vya watu kama akina Mtu wa Pwani maana hawa tunajua ni watani zetu. But I don't expect other JF analysts to be simplistic and in their analysis in their attribution of CHADEMA's failure in Kiteto.
 
Nimepokea kwa masikitiko matokeo ya uchaguzi wa kiteto,lakini hii isitufanye tuingiwe simanzi saaana ila inabidi tuangalie ni jinsi gani tunaweza kuiokoa nchi yetu kutoka mikononi mwa mafisadi,tunajua kuwa CCM wanaweza sana michezo michafu kwa kuwa tayari wameshachafuka hivyo suala la kuwatoa ktk madaraka itachukua muda mrefu sana kwa kuwa wanajua michezo yote michafu ili waweze kushinda.
dawa ya kuwaangusha ni nini?kazi iliyopo sasa ni kuungana na kuitangaza sana hii FORUM yetu ili tuweze kupata watu ktk kila idara nyeti ya serikali ili tuweze kuyapata maovu mengi ya hawa viongozi na kuyaweka hadharani ili tuwaangushe kwa style hiyo.na hili linaweza kusaidia kwa sababu naamini kabisa kuwa nia yetu sote ni kuifanya tanzania kuwa paradiso na mtanzania ajivunie nchi yake,hivyo hata kama CCM watachukua viti vyote bungeni lakini watakuwa na adabu kwa wananchi waliowachagua na wataogopa kufanya UFISADI na huo utakuwa ushindi tosha kwa wapenda mabadiliko!
kwani sote tunaamini kuwa DAUDI ALIMSHINDA GOLIATHI,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom