Uchaguzi wa Marekani umemalizika, tumeona umuhimu wa kujenga taasisi imara sio watu imara

Uchaguzi wa Marekani umemalizika, tumeona umuhimu wa kujenga taasisi imara sio watu imara

Uchaguzi wa Marekani umemalizika rasmi leo usiku kwa Rais mteule Joe Biden kuthibitishwa na mabunge yote mawili kuwa rais wa nchi hiyo baada ya rais Trump kwa kipindi cha miezi miwili kuhangaika kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Novemba mwaka jana.

Tulichojifunza zaidi ni jinsi uchaguzi huu ulivyofanyika na mapungufu yake yalivyofanyiwa kazi na vyombo husika chini ya mihimili mitatu ya nchi hiyo na jinsi utawala wa sheria ulivyoheshimiwa na demokrasia kuachwa ichukue mkondo wake.

Baada ya matokeo kutangazwa Trump alipeleka malalamiko yake Mahakamani akipinga matokeo ya baadhi ya majimbo, mahakama ikasema malalamiko yake hayakuwa na msingi wowote kwa vile hayana ushahidi.

A district court in Nevada shot down the Trump’s claims, finding “that there is no credible or reliable evidence that the 2020 General Election was affected by fraud.”

Jumamosi 2/1/2021 simu ya Trump ilidukuliwa akimpigia Afisa Tume ya uchaguzi wa Georgia Brad Raffensperger akitaka atafute kura 11,780 za ushindi akakataliwa.

“I just want to find 11,780 votes, which is one more than we have. Because we won the state," said Trump on call.

“President Trump, we’ve had several lawsuits, and we’ve had to respond in court to the lawsuits and the contentions," Raffensperger told Trump on the call. "We don’t agree that you have won."

Siku chache kabla ya Bunge la Congress kukutana kuthibitisha ushindi wa Biden, Makamu wa rais Mike Pence alikataa shinikizo la boss wake Trump la kumtaka kuingilia kati matokeo ya kura Electral College Votes na kuzuia kuthibitishwa kwa Rais mteule Jo Biden, Pence alimwambia hana uwezo huo.

"Our Founders were deeply skeptical of concentrations of power and created a Republic based on separation of powers and checks and balances under the Constitution.”

"The Presidency belongs to the American people, and to them alone," Pence told Trump.

Huu ni uthibitisho kuwa viongozi wengi walisimamia haki, utawala wa sheria, imagine makamu wa rais wa Tanzania au nchi yeyote ya Afrika angekataa maelekezo ya rais aliye madarakani.

Baada ya Trump kuona ugumu wa kuitumia mihimili ya Mahakama, Ofisi ya rais White House na Bunge, suluhisho la mwisho lilikuwa ni kuwatumia wafuasi wake na baadhi ya wabunge wa chama chake kuvamia bunge na kujaribu kuzuia mjadala wa kumthibitisha Biden kwa nguvu jaribio ambalo nalo halikufanikiwa.

Mitchell McConnell wa chama cha REPUBLICAN chama anachotoka TRUMP ndani ya Congress alisema;

"I will vote to respect the American people’s decision & defend our system of government. My full remarks".

Kwa Tanzania ni mbunge gani wa chama tawala anaweza kumwambia hivyo rais aliye madarakani.

Pamoja na wafuasi wa Trump kuvamia na kuingia hadi kwenye ukumbi wa bunge na ofisi ya Spika hatukuona polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya, najiuliza ingekuwa Dodoma watu wamevamia bunge kiasi hicho wakati huu tungekuwa na vifo vingapi na gereza la Isanga lisingetosha.

Pamoja na hayo yote leo Trump amekubali kukabidhi madaraka ifikapo 20/1/2021. Bila taasisi imara leo Trump asingekubali kutoka madarakani.

Tujifunze kuheshimu taasisi zetu, katiba na sheria tulizojitungia na tuache uhuru wa wananchi kufikisha hisia zao kwa vyombo vinavyohusika. Tutumie uchaguzi wa Marekani kuwa kama somo kwetu hasa kwa watawala wa nchi zetu za ki Afrika wanaojiona wao kama miungu watu, kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama ni rais.
Kweli mkuu ,kumtumikia pia wananchi kwa ushindi halali,kura halali,Kuna Raha yake asikwambie mtu, unakua unadeka KWA wananchi wako, vinginevyo itajikuta umepasua taifa, utafanya kila kitu kibaya au kizuri alihali kujipendekeza KWA wananchi,badala ya wananchi kukuona lulu na kujipendekeza kwako,
 
Naona umejaribu kutafuta "angle" nzuri ya kupenyeza ajenda yako katika hili.

Inawezekana ni kweli hizo taasisi unazozisema zikawa na nguvu na kutekeleza majukumu yao kulingana na matakwa ya wananchi.

Lakini Marekani wana taasisi nyingi sana zenye majukumu mbalimbali hivyo tukio hili pia limetufunza kwamba katika masuala ya kiusalama ilitakiwa Donald trump apitie vinu vikali kabla ya jina lake kupendekezwa mgombea wa uraisi mwaka 2015.

Hilo ni kosa namba moja, kumwachia mtu kama Donald Trump ambae mpaka sasa anaonekana ana mapungufu kiakili, kushika ofisi kubwa duniani ya uraisi na kukalia vitufe vya makombora ya nyuklia.

Pili, kuhusu ghasia za Capitol ni kwamba hakukuwepo polisi wa kutosha kwenye first barrier of security hivyo kulipotokea breach ikawa ngumu kwa polisi wachache walokuwepo kukabiliana na uwingi wa wafanya vurugu.

Hivyo hakukuwepo mpangilio maalum au planning kwamba Capitol pana mjadala wa kumpitisha Biden hivyo security lazima ingekuwa "beefed up".

Na mwisho ni kushindwa kwa integensia kutambua kuwepo na mpango wa vurugu hizo ambazo zimesababisha vifo vya watu watano akiwepo askari polisi.

Yaani vyombo vya kijasusi vya Marekani NSA, FBI na vingine kushindwa kubaini mipango ya vurugu, hapo pia tuna la kujifunza kwa upande wetu kama kainchi ka Afrika.

Ila vyombo vya usalama vya Tanzania pamoja na kauwezo vilivyo navyo vilijiandaa mapema kabla, wakati na baada ya uchaguzi na moja ya maeneo ya kuyaangalia kwa ukaribu ilikuwa ni mitandao ya kijamii na kuhakikisha Tweeter haitumiwi vibaya kusambaza taharuki.
Lakini hao hao tiss walishindwa kuzuia wizi wa kura.
 
WEWE NI MMOJA WA WANAOLINDWA NA MODERATORS NDIYO SABABU POST ZAKO ZA NCHI ZA NJE ZINALINDWA! ZA WENZAKO HAZICHUKUI DAKIKA ZINATUPWA KULE.
Si kweli inategemea na topic ulivyoijenga.
 
Wamekufa majambazi wa rais Trump level moja na akina bashite hawajafa waungwana wa nchi bali wale waliokuwa wanataka kutapeli uchaguzi halali wa rais.
Duuuh, aisee yaani siamini Kama na wewe unaleta utopolo huu...
Kumbe ni vema KILA ambaye ataonekana ni jambazi mbele ya serikali basi auawe tu
 
Duuuh, aisee yaani siamini Kama na wewe unaleta utopolo huu...
Kumbe ni vema KILA ambaye ataonekana ni jambazi mbele ya serikali basi auawe tu
Serikali inayoongozwa na Trump ndiyo iliyopeleka majambazi kwa amri trump sasa system ya kule ni ngumu siyo kama huku bashite anavamia kituo cha Tv na bunduki anaacha na waziri wa wizara husika anatumbuliwa baadaaye maigizo ya kuombana msamaha kwenye ujambazi yanafanyika wazi wazi ,utopolo wangu uko mheshimiwa?
 
Si kweli inategemea na topic ulivyoijenga.
Tafuta Topics zangu zaidi ya ishirini zilizoondolewa uniambie IPI INA kasoro. Wakati wa kampeni nilipigwa BAN kwa kutokubaliana na hoja ya mgombea wa CCM, nilipohoji nikapewa sababu za mwaka juzi kwenye REPLY wala haihusiani na siasa! Niliweka Post kuhusu vituko vya Trump, Post ikaunganishwa na Post tofauti kabisa! Niliweka Post kuiomba LATRA itumie mfumo tunaotumia kulipia bili au kununua umeme badala ya sisi kudaunilodi apu ambayo inahitaji intaneti, wakaihariri mwisho ikawa kama sikubaliani na mfumo mpya wa kununua tikiti kwa kutumia simu! Na wakaunganisha na kitu kingine wakati wachangiaji walikuwemo!
 
Eti Makamo wa Rais apinge agizo la Rais, Yule mama alisema wataunda serikali kwa vyovyote ata kabla ya uchaguzi wenyewe kufanyika .,
 
Back
Top Bottom