Vugu-Vugu
JF-Expert Member
- Feb 24, 2017
- 1,430
- 1,637
Amani iwe nanyi,
Katika kile kinachoonekana kuwa ni "Joto la Uchaguzi " Kanda ya kati hali si shwali kwa upande wa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Kanda Mhe Lazaro Nyalandu anayetupa karata yake kumkabili Kijana machachari Sana Alphonce Mbassa Mwenyekiti anayemaliza muda wake,
Lazaro Nyalandu aliyewahi kuwa Waziri/Naibu waziri katika kipindi cha Serikali ya awamu ya nne, Nyalandu anayetajwa kuwa miongoni mwa majasusi na mwanadiplomasia mahiri ukanda wa Africa Mashariki ,Nyalandu alitimkia Chadema akitokea CCM baada ya kuzuiliwa na CCM kwenda Nairobi kumwona ndugu yake Mh Tundu Lissu Baada ya shambulio lake la Sept 07,
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wanatamani Nyalandu apewe muda zaidi wa matazamio badala ya kupewa Nafasi hizi kubwa za maamuzi kwenye kanda yenye Majimbo 29 huku Nyalandu akiwa hafahamiani na kiongozi yeyote wa chama ngazi ya Jimbo /Wilaya wala jiografia za majimbo haya hazifahamu huku ikiwaimesalia takribani miezi sita tu kuingia Uchaguzi mkuu, Mjumbe mmoja toka Singida kask anakotoa Nyalandu aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Muro anasema namnukuu "Nyalandu tangu amehamia Chadema hajawahi kufika kwenye Kata yangu tu kama Mwanachama wa Chadema hivi leo anaomba Kanda yenye majimbo 29 ataweza kama ameshindwa kuzunguka kwenye Kata 21 tu Je hizi Kata zaidi ya 400 ataweza huyu ache uroho wa madaraka asubiri awamu ijayo "
Wachambuzi wa mambo wanamtaja Nyalandu kama Kiongozi mwoga Sana toka Upinzani inasemakana ni kutokana na historia ya maisha yake huko CCM, Nyalandu tangu kuhama kwake CCM miaka miwili iliyopita hakuwahi kuikosoa CCM wala Serikali yake popote kwa maelezo kuwa anataka kufanya Siasa za kistaarabu na Chama kisicho na chembe ya ustaarabu cha CCM Jambo ambalo linazua maswali mengi toka kwa wafuasi wake kiasi ambacho wanatilia hofu Sana aina na utamaduni mpya wa siasa ya Lazaro Nyalandu kwenye chama hiki kinachoombewa kifo na CCM kila uchapo ,
Kunawanaomtazama Nyalandu kama mtu dhaifu Sana kuongoza mapambano hasa kwenye Siasa hizi ngumu za awamu ya tano na hawaamini kabisa kama anaoujasiri wa kumkabili kisawasawa kamanda Mroto wa Dodoma au yule domokaya wa Morogoro, "Nyalandu kwaasili ni mayai Sana hawezi huu mtiti wa Vijijini kaka hii ngoma inamfaa Mbasa tu na Kizota" ,alisema afisa mmoja wa Kanda ya Kati
Nilipotaka kupata mawazo toka Vijijini Nilifanikiwa kuongea na Mwanachama mmoja toka Chilonwa aliyejitambulisha kwa jina la Chitute Msalika namnukuu " Lazaro bado mwepesi mno huku Upinzani kumpa Uenyekiti wa kanda ni kukiua chama chetu, Lazaro asubiri kwanza akomae Upinzani tutampa hata Uraisi wa nchi kama akitaka aache haraka kwanza hajaona Mzee Sumaye haraka zake zilikomfikisha? "
Wakati haya yakiendelea upande wa Mgombea Lazaro Nyalandu upande wa Mbassa wao wanasema kila mwanachama anayohaki ya kugombea nafasi yeyote ndani ya chama na wanamkaribisha Sana Bwana Nyalandu, Mpigadebe mmoja toka Upande wa Mbassa alikuwa na haya namnukuu " Nyalandu anaishi Marekani na Kenya hivi huku Gairo atafika lini? Nyalandu simu yake hapokei, Utasikia anakuandikia " TUMA SMS PLZ " kweli nitume SMS wakati nimezingirwa na wasiojulikana?? Kingine ili umpate anataka umpigie kupitia "Whatsap " hivi Yule Katibu Kata wa Iselamagazi atapata wapi simu ya whatsap?? Mimi nitaendelea kumchagua Mbasa kwanza tayari amenunua kiwanja cha kujenga makao makuu ya kanda, Mbasa bado hana mpinzani kanda,"
Mbasa mwenye misimamo isiyoyumba licha ya kufukuzwa kazi mara tatu bado amebaki kuwa na misimamo ileile kiasi cha kukimbiwa na mke,
Mbasa anasifa ya Upole, Unyenyekevu na utulivu mkubwa kwenye siasa hizi za Upinzani,Nikijana wa chama 100% kitu ambacho kinampa nguvu ya kuendelea kuaminika tofauti na mpinzani wake anayehofiwa kuunga juhudi wakati wowote ,
Wasalaam,
Tukutane trh 01/12/2019