A
Anonymous
Guest
Habari mimi ni Mwanachama wa Red Cross Tanzania Mkoa wa Tawi la Chuno, Mtwara, Wanachama wa Red Cross tunashangazwa na uhuni unaofanyika katika taasisi hii katika uchaguzi ulioanza tarehe 22/06/2026.
Mwenyekiti wa Mkoa ambaye hata wanachama hawajui ni mkazi wa Mkoa gani anashirikiana na baadhi ya viongozi wenye nia ovu kuunajisi uchaguzi katika Mkoa wetu wa Mtwara.
Hali hiyo imetokana na nia ya wazi ya Wanachama wa Red Cross kumkataa Mwenyekiti ambaye anasadikika kutotimiza majukumu yake vizuri kwa miaka sita aliyokaa madarakani hajafanya hata kikao kimoja cha kamati ya Mkoa na hata Wajumbe walipokuja kwenye kikao cha kupitia majina ya Wagombea alikimbia kikao.
Pia, Mwenyekiti kwa kushirikiana na wachache kutoka Makao Makuu wameyafuta matawi yote yaliyoonyesha kutomuunga mkono.
Taasisi ina matawi katika wilaya zote na yapo matawi yana vigezo katika Wilaya ya Mtwara, Mtwara Vijijini (Kivava) na Tandahimba (Namikupa na Mchichira) lakini yamehujumiwa.
Wanachama tunahangaika kupambana lakini bado tunazidiwa maarifa na uwezo na Mwenyekiti Hewa kwa miaka 6 hata matawini hawamfahamu kila linapotokea jukumu tunahusika sisi yeye ni wa Vikao tu huko makao makuu basi.😭😭😭
Siku kama tano nyima baadhi ya wanachama wameongea na Radio HFM kulalamika, Mkurugenzi wa Matawi, Mwenyekiti (mlalamikiwa wa figisu), Mratibu wa Wilaya ya Masasi (Mlalamikiwa wa pili) na Mratibu wa mkoa ambaye naye haridhishwi na kinachoendelea kwasababu amejikuta anabeba mzigo wa Mwenyekiti toka alipochaguliwa mwaka 2019 walihojiwa na hadi sasa hivi uchaguzi katika matawi yaliyopewa kipaumbele umefanyika katika mazingira ya ajabu.
Kwa mujibu wa Kanuni tawi linapaswa kuwa na wanachama 30+ lakini huko kuna matawi yamepiga kura wakiwa pungufu, Mkutano wa uchaguzi uwe na zaidi ya nusu ya wanachama lkn Mratibu wa Mkoa amelazimishwa kusimamia hata matawi yenye wanachama 5, 6, 7.