LGE2024 Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, Hakuna Kiongozi hata mmoja wa Serikali aliyewahi kutoa karipio Juu ya Uovu Uliokuwa Ukitendeka

LGE2024 Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, Hakuna Kiongozi hata mmoja wa Serikali aliyewahi kutoa karipio Juu ya Uovu Uliokuwa Ukitendeka

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Nchi yetu ya ajabu sana, iliyojaliwa kuwa na viongozi wa ajabu pia, viongozi wanaobariki maovu alimradi maovu hayo yawe ni dhuluma ya kuwanufaisha CCM.

Fikiria, waziri Mchemgerwa ndiye mwenye jukumu la kutengeneza kanuni za uchaguzi, akatengeneza kanuni za hovyo kabisa, ikiwemo ile ya kifungo cha 50, ya kuwalinda wasimamizi na wasimamizi wa uchaguzi watakaofanya uovu siku ya uchaguzi. Kanuni hizi za hovyo zinafahamika kwa wote, LAKINI Rais Samia kimya!! Makamu wa Rais Dr. Mpango kimya!! Waziri Majaliwa kimya. Ina maana hawa viongozi wakuu wote wamebariki hizi kanuni za kulinda uovu?

Imethibitika bila shaka yoyote kuwa TAMISEMI ya Mchengerwa imeandikisha mpaka majina ya watoto wadogo wa shule ili wayatumie kuoba kura. RAIS SAMIA, DR. MPANGO na Majaliwa, kimya!!!

Wakati wa uteuzi, zaidi ya 80% ya wagombea wote wa vyama vya upinzani walienguliwa. Baadaye wamewarudisha baadhi, lakini bado 65% hawakurudishwa. RAIS SAMIA, MPANGO na MAJALIWA kimya!

Je, haya yote yanaashiria kuwa huo uovu uliokuwa ukifanywa na wasimamizi wa uchaguzi una baraka zao au una maagizo yao?

Kama ndivyo, kwa nini Rais Samia anawahadaa Watanzania kuwa anaamini kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki, wakati kanuni za kusimamia siyo za haki, mchakato wa uandikishaji haukuwa wa haki, na uteuzi haukuwa wa haki?
 
Samia anajihisi yupo salama sana na uraisi wake. Ngoja mwakani ndiyo atajua kwamba ccm ina wenyewe
 
Weka sheria ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa Ili tujadili Kwa uelewa wa pamoja 🐼
 
Back
Top Bottom