Uchaguzi wa TLS 2024: Boniface Mwabukusi ashinda Urais, apata kura 1274

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

UPDATE: Mwabukusi ashinda Urais TLS kwa kura 1274

mwabukusi.jpg

Jumla ya kura: 2218
Kura zilizoharikika: 3

1. Boniface Mwabukusi - 1274
2. Sweetbert Nkuba - 807
3. Kapteni Ibrahim Bendera - 58
4. Paul Kaunda - 51
5. Emmanuel Muga - 18
6. Revocatus Kuuli - 7
UPDATE saa 4:40 usiku: Baadhi ya mawakili warekodiwa wakiimba wana imani na Mwabukusi, tukio lililofanya na wengine waliokuwa ukumbini watoke kwenda kuangalia kuna nini. Za ndaniiiii ni kuwa Mwabukusi kachukua kijiji. Tusubiri taarifa rasmi ya Kamati maana mpaka sasa hola!


=====

UPDATE saa nne usiku: Tundu Lissu atoa shukrani kwa mawakili wenzake kwa sapoti waliyompa kipindi chote alichokuwa kwenye matatizo (baada ya kushambuliwa na watu wasiyojulikana. Atoa hoja kuhusu wamasai wa Ngorongoro kupelekwa Tanga, ambako kutokana na sheria za ushaguzi mtu hatakiwi kupiga kura tofauti na kituo ambacho alijiandikisha. Je, hatma yao itakuaje pindi itakapofika wakati wa uchaguzi?

Pendekezo lake (Lissu) ni kwamba uongozi unaokuja uchukue suala hili na kuangalia namna ya kuingilia kati

1722625592731.png

UPDATE saa Saba Mchana: TLS waomba radhi kupitia ukurasa wao wa X baada ya kupost kuwa zoezi la upigaji kura limeisha wakati mawakili wakiwa wanasubiri karatasi za kupigia kura ziongezwe.

Kusoma zaidi kuhusu taarifa hii soma hapa: TLS waomba radhi kwa post yao waliyoweka mtandao wa X kuhusu zoezi la kupiga Uchaguzi wa Rais TLS kumalizika

======

UPDATE saa sita mchana: Ukurasa wa X wa TLS wamepost kuwa uchaguzi umeisha, lakini upande mwingine taarifa ni kuwa karatasi bado zinazubiriwa kuongezwa ili zoezi la kupiga kura liendelee kwa wale ambao bado hawajapiga kura.

Zaidi kuhusu taarifa hii soma hapa: Ukurasa wa TLS X umesema zoezi la kupiga kura limeisha, upande mwingine wanasema wanasubiri karatasi za kupiga kura ziongezwe, ukweli ni upi?

===

UPDATE majira ya saa tano asubuhi: Zoezi la kupiga kura limesimama baada ya karatasi kuisha, mawakili wanasubiri karatazi ziletwe ili zoezi liendelee.

Zaidi kuhusu hili soma hapa: Uchaguzi wa Rais TLS: Karatasi za kupigia kura zimeisha, mawakili wanasubiri karatasi nyingine ziletwe ili zoezi liendelee

====

Leo ndio leo, ni kivumbi na kijasho, hatma ya Urais TLS kugundulika leo.

Uchaguzi wa Rais wa TLS uliokuwa unasubiriwa kwa hamu, kufanyika leo Agosti 2, 2024. Je nani ataibuka mshindi kati ya wagombea hawa sita?


Kama ulikosa mdahalo wa wagombea hawa pita hapa Mdahalo wa Wagombea Urais Chama cha Mawakili Tanzania Bara (TLS) mwaka 2024

1. Capt. Ibrahim Mbiu Bendera
2. Paul Revocatus Kaunda
3. Sweetbert Mkuba
4. Boniface Mwabukusi
5. Emmanuel Agustino Muga
6. Revocutus Lubigili Kibwe

Kwa kufatilia kwangu naona upinzani mkubwa upo kati ya
Sweetbert Mkuba na Boniface Mwabukusi.

Je, unadhani mshindi atatoka kati ya hawa wawili au tutapata mshangao wa kufunga mwaka kwa asiyetarajiwa kabisa kuibuka mshindi?

Usikae mbali na uzi huu kupata updates zote za yanayoendelea kwenye uchaguzi huu.
 

Attachments

  • 1722629950224.png
    1722629950224.png
    497.6 KB · Views: 3
Kwa zile shangwe, makofi Kwa Mwabukusi.

Labda Dola iingilie Kati na jambo ambalo litakua ni la kijinga.

Nadhan MFUMO ujifunze kuwakumbatia watu wenye Uwezo mkubwa wa IQ ili Watusaidie.

Watu aina ya Mwabukusi, Lissu, Mpina, ni watu wa Haki Sanaa, watu wa Mungu...wanapopata nafasi yoyote, wanachowaza ni Maendeleo ya Taifa.
 
Hahaaa...eti nabii
Ndiyo ni Nabii Sababu anaosimamia Kweli na HAKI kusimama katika nchi.

Huyo ni mtumishi wa Mungu. Kumbuka Daudi alikuwa mfalme pia alikuwa Nabii. Huwezi kutetea maskini wasio na chochote Cha kukulipa ,ukajiweka katika hatari bila kusukumwa na Roho wa Mungu ndani Yako.

Nabii Mwabukusi njia njia nyeupeeer!!
 
Nioana kwenye Tweeter (X) ya Maria kuwa Mawakili wa Zanzibar wamepelekwa Dodoma kwenda kupiga kura za Rais wa TLS.

On top of that wamelipiwa flight tickets kuwapeleka probably na mambo mengine ambayo hatujui. Hivi Mawakili wa Zanzibar ambao nao wana chama chao huwa wanasajiliwa upya na TLS au huwa wanakuwa admitted automatically?

Kwa hili kweli jamaa wamepania kuwa Mwabukusi hachukui. Jicho letu kwa wanasheria wetu Kama nao wananunulika, then hakuna sababu ya kuwalaumu Wanannchi wa Kawaida.

Nawasilisha.
 
Nioana kwenye Tweeter (X) ya Maria kuwa Mawakili wa Zanzibar wamepelekwa Dodoma kwenda kupiga kura za Rais wa TLS.

On top of that wamelipiwa flight tickets kuwapeleka probably na mambo mengine ambayo hatujui. Hivi Mawakili wa Zanzibar ambao nao wana chama chao huwa wanasajiliwa upya na TLS au huwa wanakuwa admitted automatically?

Kwa hili kweli jamaa wamepania kuwa Mwabukusi hachukui. Jicho letu kwa wanasheria wetu Kama nao wananunulika, then hakuna sababu ya kuwalaumu Wanannchi wa Kawaida.

Nawasilisha.
Anayepiga kura ni mwanachama na anakaguliwa anapoingia ukumbini,mzanzibar asiye mwanachama atapigaje? Yamkini ni wanachama

Fatuma karume ni mzanzibar lakini amewahi kuwa Rais wa TLS
 
Ndiyo ni Nabii Sababu anaosimamia Kweli na HAKI kusimama katika nchi.

Huyo ni mtumishi wa Mungu. Kumbuka Daudi alikuwa mfalme pia alikuwa Nabii. Huwezi kutetea maskini wasio na chochote Cha kukulipa ,ukajiweka katika hatari bila kusukumwa na Roho wa Mungu ndani Yako.

Nabii Mwabukusi njia njia nyeupeeer!!
Nakubali Mwabukusi ni Mtumishi wa Mungu, tena Mungu aliyehai.
 
Back
Top Bottom