Uchaguzi wa Urais umekwisha na atakayekuwa Rais ameshajulikana tayari. Wapinzani wajipange Tu kwa uchaguzi wa Wabunge na madiwani

Uchaguzi wa Urais umekwisha na atakayekuwa Rais ameshajulikana tayari. Wapinzani wajipange Tu kwa uchaguzi wa Wabunge na madiwani

Ndugu zangu Watanzania,

Maneno haya yanaweza kuwa na maumivu makubwa sana kwa upinzani wa Nchi hii na kuonyesha pengine kuwakatisha Tamaa. Lakini huo ndio ukweli wenyewe na ndio uhalisia wenyewe wa Mambo .

Kwamba mpaka sasa Rais Na makamu wa Rais watakao Ongoza Taifa letu kwa kipindi cha Miaka mitano ijayo mpaka 2030 tayari wanafahamika na tayari DUNIA nzima inawafahamu. Kuwa Ni Mheshimiwa Rais Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan na Makamu wake ni Balozi Daktari Emmanueli Nchimbi.

Hata watanzania kwa sasa wanajua uchaguzi wa Urais Umekwisha na kuishia siku ile CCM kupitia mkutano mkuu wake maalumu ulipopitisha majina hayo na leo kutambulishwa Rasmi katika siku ya kusherehekea na kuadhimisha miaka 48 ya CCM tangia kuzaliwa kwake.

Hii ni kwa kuwa ni CCM pekee ndiyo chama chenye uwezo wa kutoa mtu mwenye uwezo na sifa za kuongoza Taifa letu. Ni CCM pekee itakayoendelea kutoa RAIS na Makamu wa Rais wa Taifa letu Mpaka Mwisho wa Dunia. Ni CCM pekee ndio itakayoendelea kutoa Dira na muelekeo wa Taifa letu .

Kwa hiyo ni muhimu vyama vya Upinzani vikatumia muda huu mfupi uliobakia kuandaa wagombea bora na wanaokubalika na kuuzika kwa wananchi katika nafasi za ubunge na udiwani. Huu ni muda wa kuweka mipango, mikakati ya kuandaa rasilimali watu na Fedha kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Ni muda wa kuandaa timu nzuri na yenye kusheheni watu wenye ushawishi,nguvu , kukubalika na wenye uwezo mzuri wa kujenga hoja watakao tumika kuwanadi wagombea ubunge na udiwani.

Huu ni muda wa kuweka mipango ya kisayansi na yenye utafiti wa kisayansi ya juu ya wapi na mahali gani chama kiweke nguvu za kutosha katika kuhakikisha kuwa maeneo hayo kitafanikiwa kupata wabunge na madiwani wa kutosha .

Ni muda wa kuangalia wapi chama kina nguvu na ngome za kihistoria na namna gani ya kuendeleza na kutumia historia hiyo kupata ushindi kwa kuleta watu wenye sifa na ushawishi. Vyama vya Upinzani ni lazima visahau kabisa na kufuta kabisa habari za Urais kwa sababu huko watakuwa wanapoteza muda na rasilimali tu bila sababu ya Msingi bila kupata matunda.x

Uchaguzi ni hesabu na Siasa ni sayansi na sayansi ina kanuni zake.

Huyu Hapa ndiye Rais wetu ajaye akiwa na Makamu wake ajaye.View attachment 3226171

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
hata kwenye ubunge waende kushiriki tu uchaguzi huo wa ubunge na udiwani kwasabb ni uhuru na haki yao kikatiba,

ila kwa hali halisi ya kisiasa ilivyo,
hakuna mahali au eneo ambalo wanaweza kushinda udiwani au ubunge humu nchini
 
hata kwenye ubunge waende kushiriki tu uchaguzi huo wa ubunge na udiwani kwasabb ni uhuru na haki yao kikatiba,

ila kwa hali halisi ya kisiasa ilivyo,
hakuna mahali au eneo ambalo wanaweza kushinda udiwani au ubunge humu nchini
Tena kwenye jimbo lako ndio wasijaribu kuleta pua zao . Maana utawapiga kipigo cha Mbwa Mwizi.
 
Dalili mojawapo ya mbwa kuelekea kufa ni kupoteza uwezo wa kunusa.Ilhali nyoka wa kijani anayetaka kufa hukimbilia barabarani.

Usiku mwema.It's time for Tundu Antipas Lissu.
 
Habari njema
JamiiForums-879365987.jpg
 
Dalili mojawapo ya mbwa kuelekea kufa ni kupoteza uwezo wa kunusa.Ilhali nyoka wa kijani kufa hukimbilia barabarani.

Usiku mwema.It's time for Tundu Antipas Lissu.
Ondoa uchizi wako hapa
 
Back
Top Bottom