Zanzibar 2020 Uchaguzi Zanzibar joto kali

Zanzibar 2020 Uchaguzi Zanzibar joto kali

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Ungetegemea mjadala ukawa umejikita katika viashiria vinavyoweza kuiangamiza Zanzibar.

Mathalan kuna joto la nyuzi za juu linaingia visiwani, joto ambalo linaweza kuwasha moto na moto huo ukateketeza. Mjadala wa kifanyike nini Wapemba wanaonyimwa vitambulisho vya ukazi warejeshewe haki yao ili waweze kupiga kura.

Hapana hili si muhimu.

Hapana uwezekano wa Wapemba kuandamana tena kama 2001 inaweza kudhibitiwa tutaonyesha kabla joto lililoingia visiwani kiasi ni mwenda wazimu tu ndiye atakaethubutu kufunga madirisha yake upepo mwanana wa Bahari ya Hindi usiingie nyumbani kwake.

Umuhimu upo kwengine si katika hili joto kali ambalo litababua ngozi za waja wa Allah ambalo kama wana kosa lolote ni kule kuipenda nchi yao na kutaka wao waheshimike na haki itendeke.

Wanaamini joto litawatisha. Wanaamini wao hawawezi kuuawa. Unapokuwa na fikra kama hii ubongo unakataa kufanya kazi yake vizuri.

Ubongo unatawaliwa na kibri. Kibri ni nguo ya Allah. Maalim Haruna alikuwa akifika hapa huuliza kwani Allah anavaa nguo?

Akijua kuwa wanafunzi wake tukielewa lakini Sheikh Haruna alikuwa ‘’artist,’’ anasomesha kwa ufundi wa kila kitu hata kulichekesha darsa.

Akipenda kusherehesha sifa za Allah na hii ilikuwa fursa hawezi kuiacha ipite. Turudi kwake Joto Kali. Swali lakujiuliza je itakapokuwa joto halikuwatisha je?

Nini matokeo yake?

Walisimama masahaba viwanja vya Badr na kuangalia ukubwa wa jeshi la makafiri na mbwebwe zao ndani ya jeshi lililosheheni silaha kali na wapiganaji hodari.

Ngoma na midundo ya vita ikisikika waziwazi. Kulikuwa na sheikh mmoja Dar es Salaam ikifika 17 Ramadhani anatoa mhadhara wa umuhimu wa kuijua historia ya Vita Vya Badr.

Alikuwa hawezi kujizuia khasa pale anaposoma dua ya Mtume SAW aliponyanyua mikono kuomba nusra kwa Waislam. Joto hili lishajiangalia wao wenyewe linakotokea asili yake na kabila yake?

Joto limenyanyua kichwa na kuwatazama hata kwa fikra wale (Allah apitishie mbali) wanyonge wasiokuwa hata na uchelewa mkononi watakaotoka kulikabili joto?

Hawa ni nani?

Hawa ni dini gani?

Na sisi joto ni dini gani?

Litakapomalizika joto na pakawa kimya.

Nini kitakuwa kimebakia?
 
Joto kali lakini lukuvi kwa maneno haya kaishalizima, jeshi letu ni imara
 
Ungetegemea mjadala ukawa umejikita katika viashiria vinavyoweza kuiangamiza Zanzibar.

Mathalan kuna joto la nyuzi za juu linaingia visiwani, joto ambalo linaweza kuwasha moto na moto huo ukateketeza.

Mjadala wa kifanyike nini Wapemba wanaonyimwa vitambulisho vya ukazi warejeshewe haki yao ili waweze kupiga kura.

Hapana hili si muhimu.

Hapana uwezekano wa Wapemba kuandamana tena kama 2001 inaweza kudhibitiwa tutaonyesha kabla joto lililoingia visiwani kiasi ni mwenda wazimu tu ndiye atakaethubutu kufunga madirisha yake upepo mwanana wa Bahari ya Hindi usiingie nyumbani kwake.

Umuhimu upo kwengine si katika hili joto kali ambalo litababua ngozi za waja wa Allah ambalo kama wana kosa lolote ni kule kuipenda nchi yao na kutaka wao waheshimike na haki itendeke.

Wanaamini joto litawatisha.

Wanaamini wao hawawezi kuuawa.

Unapokuwa na fikra kama hii ubongo unakataa kufanya kazi yake vizuri.

Ubongo unatawaliwa na kibri.

Kibri ni nguo ya Allah.

Maalim Haruna alikuwa akifika hapa huuliza kwani Allah anavaa nguo?

Akijua kuwa wanafunzi wake tukielewa lakini Sheikh Haruna alikuwa ‘’artist,’’ anasomesha kwa ufundi wa kila kitu hata kulichekesha darsa.

Akipenda kusherehesha sifa za Allah na hii ilikuwa fursa hawezi kuiacha ipite.

Turudi kwake Joto Kali.

Swali lakujiuliza je itakapokuwa joto halikuwatisha je?

Nini matokeo yake?

Walisimama masahaba viwanja vya Badr na kuangalia ukubwa wa jeshi la makafiri na mbwebwe zao ndani ya jeshi lililosheheni silaha kali na wapiganaji hodari.

Ngoma na midundo ya vita ikisikika waziwazi.

Kulikuwa na sheikh mmoja Dar es Salaam ikifika 17 Ramadhani anatoa mhadhara wa umuhimu wa kuijua historia ya Vita Vya Badr.

Alikuwa hawezi kujizuia khasa pale anaposoma dua ya Mtume SAW aliponyanyua mikono kuomba nusra kwa Waislam.

Joto hili lishajiangalia wao wenyewe linakotokea asili yake na kabila yake?

Joto limenyanyua kichwa na kuwatazama hata kwa fikra wale (Allah apitishie mbali) wanyonge wasiokuwa hata na uchelewa mkononi watakaotoka kulikabili joto?

Hawa ni nani?

Hawa ni dini gani?

Na sisi joto ni dini gani?

Litakapomalizika joto na pakawa kimya.

Nini kitakuwa kimebakia?
Uchaguzi wa ZANZIBAR , ccm imeshashinda, bwana mwinyi mkuu anasubiri kuapishwa tu.
 
IMG_6240.JPG
 
Lissu hotuba yake kwa Wazanzibar ilikua chungu upande wa muungano.
 
Kipanga,
Ikiwa CCM watashinda baada ya kila Mzanzibari anaestahili kupiga kura ataruhusiwa kupiga kura, kwa maana ya uchaguzi kuwa huru na wa haki hili litakuwa tukio la ajabu sana.
Nani kakwambia sisi ccm tunategemea uchaguzi huru na haki.

Sisi kura tutawaibia na hamuwezi kutufanya chochote.
 
Kyalosangi,
Hivyo hapo chini ndiyo vitabu Mh. Lissu amewataka Wazanzibari wavisome.

Waandishi wa vitabu hivi wote nawafamu vyema.
Hotuba ya Mh. Lissu ni ya kufikirisha sana.View attachment 1563384View attachment 1563385

..umewahi kujiuliza maktaba ya Jpm ina vitabu gani?

..sijawahi kumsikia huyu Mzee akifanya reference ya kitabu chochote, au mwanazuoni yeyote.

..yeye ni kupuyanga tu na maneno ya hovyohovyo, yasoendana na umri wake, na nafasi yake ktk jamii.
 
JK,
Huwa nikisom "huyu mzee," tayari nishajua hapa pana shari.

Sijafahamu uhusiano wa maktaba ya mtu mwingine awaye yule na Maktaba yangu.

Waandishi wa Nyerere Biography wameitaja Maktaba yangu kuwa ni kati ya maktaba tatu bora walizopata kuziona wakati wanatafiti maisha ya Julius Nyerere.

Maktaba ya Dr. Salim Ahmed Salim, Hashim Mbita na yangu.

Kuhusu kufanya rejea ya vitabu nimefanya sana hapa jamvini.

Pitia niliyoandika hapa utaona.

Kuhusu wanazuoni wengi tunafahamiana Ali Mazrui, Ahmed Mouhiddin, Hamza Njozi, Jonathan Glassman, James Brennan, James Giblin, Khalil MohamedTimamy, Ibrahim Noor Shariff, Abdul Shariff, Kai Kresse wengi, wengi sana.
 
Kaongea weee, mwisho wa siku naski binti wake kamkabidhisha kwa Mzanzibari 😀

Joto kali lakini lukuvi kwa maneno haya kaishalizima, jeshi letu ni imara ,

Bint yake yupo kwa Zanzibari hapo sasa
 
Joto kali lakini lukuvi kwa maneno haya kaishalizima, jeshi letu ni imara ,

Bint yake yupo kwa Zanzibari hapo sasa
Subiri tuone kama ameshalizima au bado siku ya matokeo.

Nimesikia Sirro kasema atahamia Pemba siku ya uchaguzi. Mwambieni kwa uataratibu wetu visiwani ni muhimu kutoa taarifa kwa sheha kama unahamia ili majirani zako nao wajue unapokaa iwe rahisi kuja kukutembelea au kukusaidia unapopatwa na matatizo 🙂
 
JK,
Huwa nikisoma, "huyu mzee," tayari nishajua hapa pana shari.

Sijafahamu uhusiano wa maktaba ya mtu mwingine awaye yule na Maktaba yangu.

Waandishi wa Nyerere Biography wameitaja Maktaba yangu kuwa ni kati ya maktaba tatu bora walizopata kuziona wakati wanatafiti maisha ya Julius Nyerere.

Maktaba ya Dr. Salim Ahmed Salim, Hashim Mbita na yangu.

Kuhusu kufanya rejea ya vitabu nimefanya sana hapa jamvini.

Pitia niliyoandika hapa utaona.

Kuhusu wanazuoni wengi tunafahamiana Ali Mazrui, Ahmed Mouhiddin, Hamza Njozi, Jonathan Glassman, James Brennan, James Giblin, Khalil MohamedTimamy, Ibrahim Noor Shariff, Abdul Shariff, Kai Kresse wengi, wengi sana.
Joka Kuu angalia picha niko na Prof. James Giblin University of Iowa US.
Screenshot_20200909-132504.jpg
 
Back
Top Bottom