JK,
Huwa nikisom "huyu mzee," tayari nishajua hapa pana shari.
Sijafahamu uhusiano wa maktaba ya mtu mwingine awaye yule na Maktaba yangu.
Waandishi wa Nyerere Biography wameitaja Maktaba yangu kuwa ni kati ya maktaba tatu bora walizopata kuziona wakati wanatafiti maisha ya Julius Nyerere.
Maktaba ya Dr. Salim Ahmed Salim, Hashim Mbita na yangu.
Kuhusu kufanya rejea ya vitabu nimefanya sana hapa jamvini.
Pitia niliyoandika hapa utaona.
Kuhusu wanazuoni wengi tunafahamiana Ali Mazrui, Ahmed Mouhiddin, Hamza Njozi, Jonathan Glassman, James Brennan, James Giblin, Khalil MohamedTimamy, Ibrahim Noor Shariff, Abdul Shariff, Kai Kresse wengi, wengi sana.
..asante kwa jibu lako.
..lakini nadhani hukunielewa, labda sikujieleza vizuri.
..niliposema " mzee huyu " nilikuwa namemlenga Jpm.
..kwamba Jpm ni mzee asiyejiongeza, na anayepuyanga tu ktk mazungumzo yake.
.. Mohamed Said, mimi nakikubali kipaji chako, na nauheshimu mchango wako.
..Pole kwa usumbufu niliousababisha.