Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ungetegemea mjadala ukawa umejikita katika viashiria vinavyoweza kuiangamiza Zanzibar.
Mathalan kuna joto la nyuzi za juu linaingia visiwani, joto ambalo linaweza kuwasha moto na moto huo ukateketeza. Mjadala wa kifanyike nini Wapemba wanaonyimwa vitambulisho vya ukazi warejeshewe haki yao ili waweze kupiga kura.
Hapana hili si muhimu.
Hapana uwezekano wa Wapemba kuandamana tena kama 2001 inaweza kudhibitiwa tutaonyesha kabla joto lililoingia visiwani kiasi ni mwenda wazimu tu ndiye atakaethubutu kufunga madirisha yake upepo mwanana wa Bahari ya Hindi usiingie nyumbani kwake.
Umuhimu upo kwengine si katika hili joto kali ambalo litababua ngozi za waja wa Allah ambalo kama wana kosa lolote ni kule kuipenda nchi yao na kutaka wao waheshimike na haki itendeke.
Wanaamini joto litawatisha. Wanaamini wao hawawezi kuuawa. Unapokuwa na fikra kama hii ubongo unakataa kufanya kazi yake vizuri.
Ubongo unatawaliwa na kibri. Kibri ni nguo ya Allah. Maalim Haruna alikuwa akifika hapa huuliza kwani Allah anavaa nguo?
Akijua kuwa wanafunzi wake tukielewa lakini Sheikh Haruna alikuwa ‘’artist,’’ anasomesha kwa ufundi wa kila kitu hata kulichekesha darsa.
Akipenda kusherehesha sifa za Allah na hii ilikuwa fursa hawezi kuiacha ipite. Turudi kwake Joto Kali. Swali lakujiuliza je itakapokuwa joto halikuwatisha je?
Nini matokeo yake?
Walisimama masahaba viwanja vya Badr na kuangalia ukubwa wa jeshi la makafiri na mbwebwe zao ndani ya jeshi lililosheheni silaha kali na wapiganaji hodari.
Ngoma na midundo ya vita ikisikika waziwazi. Kulikuwa na sheikh mmoja Dar es Salaam ikifika 17 Ramadhani anatoa mhadhara wa umuhimu wa kuijua historia ya Vita Vya Badr.
Alikuwa hawezi kujizuia khasa pale anaposoma dua ya Mtume SAW aliponyanyua mikono kuomba nusra kwa Waislam. Joto hili lishajiangalia wao wenyewe linakotokea asili yake na kabila yake?
Joto limenyanyua kichwa na kuwatazama hata kwa fikra wale (Allah apitishie mbali) wanyonge wasiokuwa hata na uchelewa mkononi watakaotoka kulikabili joto?
Hawa ni nani?
Hawa ni dini gani?
Na sisi joto ni dini gani?
Litakapomalizika joto na pakawa kimya.
Nini kitakuwa kimebakia?