Kama baadhi ya wachangiaji walivyosema ni ngumu kwa mahakama zetu kutoa haki, na waTZ wameshapigwa mkwala kuwa upinzani unataka kumwaga damu, kwa hiyo hata Dr. Slaa akizungumza vipi bado kunawatanzania watasema huyu anataka kuleta fujo(uelewa wa watz ni mdogo sana hata wale wa mijini, akina malaria sugu ni wengi). Ninachoona mimi ili swala nikulipeleka kwa wafadhili tu.
Uelewa wa WaTanzania si mdogo hata kidogo kama ulivodaid.uelewa wa waTanzania ni mkubwa lakini ndani yake kuna udhaifu wa UNYONGE na KUKOSA MATUMAINI. Watanzania wanaelewa kila kitu, wana uwezo wa kudadisi ili kupata undani pia ni watu wasiotaka kuburutwa.
Ttatizo kubwa linalotukabili Tanzania ni uhalalishwaji wa mtandao mkubwa wa Uharamia unaojumuisha Vyombo vyote vya dola, idara zote za serikali na mashirika ya umma pamoja na ofisi zetu zote za balozi.
Mtandao huu mkubwa wenye baraka zote kutoka Ikulu kwa MH Rais umekuwa ukitoa Baraka kwa mitandao midogo ya uharamia inayohusika moja kwa moja kuwabugudhi wananchi na kuwagandamiza kupitia serikali za mitaa, mahakama za mwanzo pia ofisi za CCM matawini na vitongojini na hata baadhi ya Mashirika ya kidini na NGO huko vijijini. KMfano mwananchi wakawaida ni nadra kutofautisha Ofisi ya CCM na Kituo cha Polisi,Si kwa kutoelewa bali kwa kushindwa kutofautisha utekelezaji na namna wote walivyo na mamraka ya Kipolisi. Mwnanchi wa Kawaida hawezi tofautisha Mamraka ya kisheria waliyo nayo Polisi na Watendaji wa CCM.
Mindao yote ya kiserikali iko funded na Wizi wa fedha za uendeshaji wa shughuli za kiserikali na kuwaibia wananchi moja kwa moja kutoka
mifukoni mwao.
CCM pamoja na kupata ruzuku ya mabilioni kila mwezi chanzo kikubwa cha mapato yao ni KUIBA kutoka hazina kuu ya serikali.
CCM hawawezi kuiba Bila kutumia watumishi wa serikali, watumishi wa serikali hawawezi kushiriki kuiba bila au kutiwa shinikizo na kibano aukuahidiwa kunufaika kwa namna moja au nyingine na wizi huo.
Mkubwa akisha iba mdogo naye anaiba kwa njia ileile hapo ndipo kigugumizi cha kila kiungo mwilini huanza kutokana na idadi ya wenye uwezo wa kumfunga paka kengere ianzapo kutoweka.
Siku zote Wanashitakiwa na kufungwa wezi wa kuku mbuzi na Mafenesi katika mashamba ya Wezi wakubwa wa fedha ya Umma na wezi wale walio nje ya mtandao.
Ukiona mtu anafikishwa mahakamani kutoka serikalini au ndani ya chama kwa wizi mtu huyo anafanywa Kondoo wa kafara tu au ameiba nje ya mtandao wa kiharamia.
Hii ni Domino Effect, Wizi ni jambo lililokusudiwa tangu awali lakini matokeo mengi tunyaonayo si jambo lililokusudiwa mwanzo ni jambo ambalo limewaponyoka. Hawawezi na pia hawajui namna ya kuzuia Domino effect hii kwa sababu ya uchafu mwingi nafsini na akilini mwao unawanyimao uwezo hamu nia na kasi ya kuvunja Domino Effect.
Zaidi wanaelewa kwamba wale wenye uwezo wa kukomesha Uharamia huu wana uwezo pia wa kuangamiza himaya zao za udharimu.Himaya zao za uhalifu zikiangamizwa nafasi zao uwepo wao na heshima walizo jijengea kwa Kiburi cha uharamia vyote vitatoweka.
Dawa pekee ya Kulinda himaya hii ya KIIBILISI ni kukumbatia aina zote za uovu, uoza na uharamia kwa gharama ya kodi atozwayo Mtanzania na uhai wake.
Watanzania kadhaa less than 5% wamefaidika moja kwa moja na wizi wa kimtandao kiasi cha kuamini kwamba huo ndo utaratibu wa kujikimu katika maisha. Pamoja na uelewa mkubwa wa Maharamia hawa wanajaribu kulinda mfumo uwapao mapato bila kutoa jasho wala kubughudhiwa. Hili kundi la 5% linajumuisha Watumishi wengi wa serikali na mashirika ya umma na wafanya biashara ambao mara nyingi hawana choice.
Kwa ushawishi mkubwa wa kundi hili la 5% kila mtu wengi wa Watanzania hupiga njozi na kuamini siku moja wao pia watafaidika na mtandao wa wizi. Labda ni jambo lenye manufaa kulinda mtandfao wa uhalifu.
Kauri za Dr Slaa za kubomoa Mtandao na kuunda utaratibu mpya ni tishio kwa hili kundi la 5% ndiyo maana kundi hili halioni taabu na halisiti kutawanya hofu iliyo ndani ya nafsi zao kwa Watanzania wote. Watu wa mtandao wa uovu wanajua fika kwamba Dr Slaa akishinda wao kama Maharamia wa kitaifa watanyolewa kavu na himaya yao itavunjika vipande. Wanajua kabisa kwamba asilimia 95% ya watanzania watafaidika na kuvunjika kwa himaya zao, kwa nini wasiwageuzie kibao wananchi na kuwaambukiza hofu waliyonayo kwa hasara yao wananchi wenyewe??
Huu ugumu wa serikali kuchukua hatua ndilo jambo tupaswalo kulichambua kisayansi na kuweka bayana na kinaga ubaga na kutoa shinikizo la nguvu kwa watendaji wa serikali kutoa majibu ya mswali yetu au kuachia ngazi.
Mashushsu wa MOSAD wameweza kulinda nchi yao Israel dhidi ya njama zote za mahasimu wao kwa kuimarisha utaalamu wa KuTrail Fedha inayoingia na kutoka kwa kila mtuhumiwa, kitaifa na kimataifa.
Ukitaka kukamata wahalifu wote ndani na nje ya serikali Tanzania fuata mtiririko wa fedha kabla na baada ya kitendo cha uovu.
Rais Kikwete anatabasamu na kusema" Ongezeko kubwa la Magari Dar ni dalili za maendeleo" Ujumbe wa moja kwa moja kwa waliofaidika na mtandao wa kiharamia "kumbukeni kwamba mtandao wa kiovu ndo ulowapa uwezo wakununua sehemu kubwa ya magari haya mnaweza kuuwa chanzo cha magidai yenu??