Elections 2010 Uchakachuaji HAUPO! - NYARAKA HIZI HAPA NI FAKE

Status
Not open for further replies.
TISS wanajua mahakamani watatolewa nock out bse Slaa ana ushaidi ndo maana wameamua wajibu via waandishi wa habari.
Ata EPA WALISEMA walimwambia mropokaji.
Sijawai ona TISS wanajitetea kwa waandishi wa habari toka nizaliwe yaani nowdays imekuwa taasisi ya kawaida sana
Its common sense mtu akikuzushia sifa unaenda mahakamani kwa TISS imekuwa kinyume mahakama kwao ni waandishi wa habari very unprofessional and ridiculous
 

Nimekusoma na nimekuelewa vizuri, hapo kwenye nyekundu labda tuiweke hivi, Usalama wa taifa kwa sasa ni chombo kilicho wazi na kinajulikana na kipo mwa mujibu wa sheria, lakini kazi zake ni za siri, Usalama wa taifa haimpeleki mtu mahakamani (Kumbuka kesi ya uhaini watu wa usalama walifanya kazi kubwa sana lakini kwenye kushtaki halikuwa suala lao), bali watafanya uchunguzi na mwisho issue inakuwa handled police, na wala Usalama sio taasisis ya kukurupuka kwenye vyombo vya habari na ndio maana hawana msemaji wa UWT, tatizo Slaa kawachoma mkuki wa ukweli na jamaa wamepoteza mwelekeo na kutokujua ni nini cha kufanya, kama Slaa alikuwa na hoja, hao jamaa wangemwita na kuchunguza madai yake kama ni kweli basi wangedili na waliohusika kwa sheria zao na kama Slaa ni muongo wangeipeleka kesi police na hatimae mahakamani
 
Usalama wa Taifa imeoza, haina maadili na ni aibu sana kwa Taifa letu. Sio chombo cha sisi Watanzania kujivunia tena. Hata wafanyakazi wake wakionekana mtaani wanatakiwa watembee vichwa chini na si kifua mbele kama zamani walipokuwa wanaheshimika na kutetemekewa na kuonekana kama akina James Bond. Sasahivi wakipita wanaonekana ni wachakachuaji tu!

Chombo hiki enzi za mwalimu kilikuwa na sifa sana na maadili kwa kulinda usalama wa wananchi, lakini sahivi kinalinda usalama wa JK na CCM.

Tatizo chombo hiki kiko chini ya ofisi ya rais, mnadhani wamtetea nani?

Ushauri wangu ni kama mkurugenzi wa usalama anaipenda nchi yake ingawa alishinikizwa na boss wake, nadhani ingekuwa busara akajiuzuli. Angalau nafsi yake itakuwa na amani kidogo kwa dhambi aliyolazimishwa kuutendea umma wa wa Watanzania kwa shinikizo la boss wake JK. Na pia hata Mungu atamwonea huruma.

Otherwise na wewe, na usalama wa CCM na kuchakachua mna tuhuma ya kujibu, pamoja na NEC, jeshi na TAKUKURU na vibaka wengine wote mlioshiriki kwa aina moja au nyingine kukandamiza haki za wananchi na kutotimiza wajibu wenu.
 
Usalama wa Taifa imeoza, haina maadili na ni aibu sana kwa Taifa letu. Sio chombo cha sisi Watanzania kujivunia tena. Hata wafanyakazi wake wakionekana mtaani wanatakiwa watembee vichwa chini na si kifua mbele kama zamani walipokuwa wanaheshimika na kutetemekewa na kuonekana kama akina James Bond. Sasahivi wakipita wanaonekana ni wachakachuaji tu!

Chombo hiki enzi za mwalimu kilikuwa na sifa sana na maadili kwa kulinda usalama wa wananchi, lakini sahivi kinalinda usalama wa JK na CCM.

Tatizo chombo hiki kiko chini ya ofisi ya rais, mnadhani wamtetea nani?

Ushauri wangu ni kama mkurugenzi wa usalama anaipenda nchi yake ingawa alishinikizwa na boss wake, nadhani ingekuwa busara akajiuzulu. Angalau nafsi yake itakuwa na amani kidogo kwa dhambi aliyolazimishwa kuutendea umma wa wa Watanzania kwa shinikizo la boss wake JK. Na pia hata Mungu atamwonea huruma.

Otherwise na wewe, na usalama wa CCM mna tuhuma ya kujibu, pamoja na NEC, jeshi na TAKUKURU na vibaka wengine wote mlioshiriki kwa aina moja au nyingine kukandamiza haki za wananchi na kutotimiza wajibu wenu.
 
Kama baadhi ya wachangiaji walivyosema ni ngumu kwa mahakama zetu kutoa haki, na waTZ wameshapigwa mkwala kuwa upinzani unataka kumwaga damu, kwa hiyo hata Dr. Slaa akizungumza vipi bado kunawatanzania watasema huyu anataka kuleta fujo(uelewa wa watz ni mdogo sana hata wale wa mijini, akina malaria sugu ni wengi). Ninachoona mimi ili swala nikulipeleka kwa wafadhili tu.
 
Lala kijana lala naona usingizi unakuuma!!!!!!!!!
 

Sidhani kama unaelewa taratibu za kisheria.

Mtu akinituhumu kwamba mimi ni mwizi, kisha mimi nikakataa, bado kisheria sijajisafisha. Natakiwa kufungua kesi ya kusafisha jina langu mahakamani. Vinginevyo mtu huyo aende katika vyombo vya habari na kukanusha usemi wake.
Sisi wananchi wa Tanzania tunatakiwa, kwa hali na mali, kuwashindikiza UWT NEC na CCM kwenda Mahakamani kumshtaki Dr Slaa, Vinginevyo WANAKUBALI KWAMBA TUHUMA NI ZA KWELI NI MAHARAMIA, WAMEIBA KURA.

Dr Slaa aende Mahakamani kufanya nini??
 

Mheshimiwa Masauni,

Inaleta maana hebu unganisha na hii kuanzia Pretoria, Tunduma, Karatu, hadi vyombo vya habari...na kutishiana mahakamani!!!

https://www.jamiiforums.com/results-m...ka-huko-2.html
 

Mkuu umenena nazito!

Umeseama yote yanayotakiwa kusemwa!!
 
Wachangiaji wote naungana nao...NEC ndo wakulaumiwa kwani hadi sasa wanaulizwa iweje wapiga kura halali waliojiandikisha ni 20millions lakini waliopiga kura ni 8millions tu......!hawana majibu....that means data zao ni inconsistence kabisa...kama hivyo ndivyo even matokeo walotoa sio ya kweli hata kidogo na hakuna haja ya kuwa na daftari la kupiga kura...data zao zote zipo kirushwa rushwa...mimi ni mtaalamu wa mambo ya computer na mawasiliano ya simu...utumiaji wa TEKNOHAMA ktk uchaguzi ni mzuri lakini kwa nchi kama ya Tanzania,ambayo kwanza ndo inaamkia katika TEKNOHAMA,mda wa reserch lazima upewe kipaumbele kwanza....na pia ni rahisi sana KUCHAKACHUA MATOKEO kupitia TEKNOHAMA kuliko wengi wanavyofikiri...
 

Alichofanya Dr slaa ni kuwashitakia kwa wananchi kupitia media kwamba usalama wa taifa ndo waliofanikisha wizi wa kura ili wananchi watoe hukumu. kwa maana nyingine wananchi ndo mahakama.
 

Uelewa wa WaTanzania si mdogo hata kidogo kama ulivodaid.uelewa wa waTanzania ni mkubwa lakini ndani yake kuna udhaifu wa UNYONGE na KUKOSA MATUMAINI. Watanzania wanaelewa kila kitu, wana uwezo wa kudadisi ili kupata undani pia ni watu wasiotaka kuburutwa.

Ttatizo kubwa linalotukabili Tanzania ni uhalalishwaji wa mtandao mkubwa wa Uharamia unaojumuisha Vyombo vyote vya dola, idara zote za serikali na mashirika ya umma pamoja na ofisi zetu zote za balozi.

Mtandao huu mkubwa wenye baraka zote kutoka Ikulu kwa MH Rais umekuwa ukitoa Baraka kwa mitandao midogo ya uharamia inayohusika moja kwa moja kuwabugudhi wananchi na kuwagandamiza kupitia serikali za mitaa, mahakama za mwanzo pia ofisi za CCM matawini na vitongojini na hata baadhi ya Mashirika ya kidini na NGO huko vijijini. KMfano mwananchi wakawaida ni nadra kutofautisha Ofisi ya CCM na Kituo cha Polisi,Si kwa kutoelewa bali kwa kushindwa kutofautisha utekelezaji na namna wote walivyo na mamraka ya Kipolisi. Mwnanchi wa Kawaida hawezi tofautisha Mamraka ya kisheria waliyo nayo Polisi na Watendaji wa CCM.
Mindao yote ya kiserikali iko funded na Wizi wa fedha za uendeshaji wa shughuli za kiserikali na kuwaibia wananchi moja kwa moja kutoka
mifukoni mwao.


CCM pamoja na kupata ruzuku ya mabilioni kila mwezi chanzo kikubwa cha mapato yao ni KUIBA kutoka hazina kuu ya serikali.

CCM hawawezi kuiba Bila kutumia watumishi wa serikali, watumishi wa serikali hawawezi kushiriki kuiba bila au kutiwa shinikizo na kibano aukuahidiwa kunufaika kwa namna moja au nyingine na wizi huo.

Mkubwa akisha iba mdogo naye anaiba kwa njia ileile hapo ndipo kigugumizi cha kila kiungo mwilini huanza kutokana na idadi ya wenye uwezo wa kumfunga paka kengere ianzapo kutoweka.

Siku zote Wanashitakiwa na kufungwa wezi wa kuku mbuzi na Mafenesi katika mashamba ya Wezi wakubwa wa fedha ya Umma na wezi wale walio nje ya mtandao.
Ukiona mtu anafikishwa mahakamani kutoka serikalini au ndani ya chama kwa wizi mtu huyo anafanywa Kondoo wa kafara tu au ameiba nje ya mtandao wa kiharamia.

Hii ni Domino Effect, Wizi ni jambo lililokusudiwa tangu awali lakini matokeo mengi tunyaonayo si jambo lililokusudiwa mwanzo ni jambo ambalo limewaponyoka. Hawawezi na pia hawajui namna ya kuzuia Domino effect hii kwa sababu ya uchafu mwingi nafsini na akilini mwao unawanyimao uwezo hamu nia na kasi ya kuvunja Domino Effect.
Zaidi wanaelewa kwamba wale wenye uwezo wa kukomesha Uharamia huu wana uwezo pia wa kuangamiza himaya zao za udharimu.Himaya zao za uhalifu zikiangamizwa nafasi zao uwepo wao na heshima walizo jijengea kwa Kiburi cha uharamia vyote vitatoweka.

Dawa pekee ya Kulinda himaya hii ya KIIBILISI ni kukumbatia aina zote za uovu, uoza na uharamia kwa gharama ya kodi atozwayo Mtanzania na uhai wake.

Watanzania kadhaa less than 5% wamefaidika moja kwa moja na wizi wa kimtandao kiasi cha kuamini kwamba huo ndo utaratibu wa kujikimu katika maisha. Pamoja na uelewa mkubwa wa Maharamia hawa wanajaribu kulinda mfumo uwapao mapato bila kutoa jasho wala kubughudhiwa. Hili kundi la 5% linajumuisha Watumishi wengi wa serikali na mashirika ya umma na wafanya biashara ambao mara nyingi hawana choice.

Kwa ushawishi mkubwa wa kundi hili la 5% kila mtu wengi wa Watanzania hupiga njozi na kuamini siku moja wao pia watafaidika na mtandao wa wizi. Labda ni jambo lenye manufaa kulinda mtandfao wa uhalifu.

Kauri za Dr Slaa za kubomoa Mtandao na kuunda utaratibu mpya ni tishio kwa hili kundi la 5% ndiyo maana kundi hili halioni taabu na halisiti kutawanya hofu iliyo ndani ya nafsi zao kwa Watanzania wote. Watu wa mtandao wa uovu wanajua fika kwamba Dr Slaa akishinda wao kama Maharamia wa kitaifa watanyolewa kavu na himaya yao itavunjika vipande. Wanajua kabisa kwamba asilimia 95% ya watanzania watafaidika na kuvunjika kwa himaya zao, kwa nini wasiwageuzie kibao wananchi na kuwaambukiza hofu waliyonayo kwa hasara yao wananchi wenyewe??

Huu ugumu wa serikali kuchukua hatua ndilo jambo tupaswalo kulichambua kisayansi na kuweka bayana na kinaga ubaga na kutoa shinikizo la nguvu kwa watendaji wa serikali kutoa majibu ya mswali yetu au kuachia ngazi.

Mashushsu wa MOSAD wameweza kulinda nchi yao Israel dhidi ya njama zote za mahasimu wao kwa kuimarisha utaalamu wa KuTrail Fedha inayoingia na kutoka kwa kila mtuhumiwa, kitaifa na kimataifa.
Ukitaka kukamata wahalifu wote ndani na nje ya serikali Tanzania fuata mtiririko wa fedha kabla na baada ya kitendo cha uovu.


Rais Kikwete anatabasamu na kusema" Ongezeko kubwa la Magari Dar ni dalili za maendeleo" Ujumbe wa moja kwa moja kwa waliofaidika na mtandao wa kiharamia "kumbukeni kwamba mtandao wa kiovu ndo ulowapa uwezo wakununua sehemu kubwa ya magari haya mnaweza kuuwa chanzo cha magidai yenu??
 

Ndugu yangu umenena sahihi kabisaaaa!
Mimi ninaishi Arusha! Nilikuwepo kwenye mchakato woooote wa uchaguzi wa jimbo la Arusha mjini. Siku ya kutangaza matokeo, Batilda Buriani alikataa kusainin matokeo akidai hawezi kusaini hadi Lowassa aje. Ni kweli baada ya saa kadhaa kupita, Lowassa alifika hapa mjini ktk ukumbi wa manispaa/halmasahuri na kuingia hadi pale ndani tulipokuwepo. Punde kabla hajaingia ndani, wananchi waliokuwepo pale nje walimzomea sana. Kule ndani, alijaribu saaaaanaaa kumshawishi Lema Godbless achukue kiasi fulani cha pesa ili akubali na atangaze kuwa yeye (Lema) ameshindwa ubunge, Lowassa alifika hadi 900M. Lema akamwambia toka hapo nje waambie hao wananchi waliokusanyika kuwa unanipa hizi pesa wakikubali then njoo ndani tusaini. Lema akapiga simu kwa Ndessamburo na Mbowe nao wakaja. Punde matokeo yakatangazwa. Lakini ktk magazeti ya leo Lowassa anakanusha kuwa hakuhusika na jaribio la uchakachuaji wa matokeao ya Arusha. Hivyo basi naungana na wewe ndugu yangu kuwa hawa jamaa in how hata ukiwakuta Red-handed, watakaaaa tu. (watasema It wasn't me!).
Kuna Afisa Usalama mmoja (jina ninalihifadhi) aliporwa bastola na vibaka maeneo ya Shevers (eneo maarufu kwa vyangudoa) hapa Arusha.
haya yoote naweza kuyathibisha in the court of law.
 
Wanausalama wa Taifa (TISS) kwa kujua kujenga hoja juu ya propaganda nina wa-adore kweli kweli.
naamini wewe umetumwa kama wenzio. kwa taarifa yako, hapa jukwaani siyo watu wepesi unavyofikiria. kila nukta tunaisoma na kuielewa zaidi ya text.
Najua mnalipwa pesa nyingi sana ndo maana hamuoni machungu na machozi ya watanzania wavija jasho mnaowakandamiza.

 
Aisee, hawa jamaa inabidi sasa watembee na bodyguard maana maisha yao yapo hatarini ktk kuilinda nchi na ccm
 
asnthe sana ndugu...tunapata shida sana kupigania ukweli na haki zetu za kikatiba kutoka kundi la watu wapenda madaraka kama kina lowassa....kuhusu hawa afisa usalama wetu ni wanatia aibu!!!!!ona huyo kaporwa na bunduki yake tena akiwa shivers!!!
 
Dr slaa atafute umaarufu kwanani ? Hivi ninani asiye mfaham slaa mpaka aangaike kutafuta umaarufu? Nahic umelogwa na bibi yako!!

heheeeeee e=heeeeee we slaaaa damu, umaarufu kwisha....... kama si umaarufu anaytafuta jemedari asiekubali shindwa jemedari gani CCM daima
 
I think I was wrong, walotajwa kwenye hii kitu wangeangalia hii FAKE thing mapema wangepata majibu ya kumjibu Slaa alipotoka na barua hii... Wengine waliniuliza SOURCE! Niliamua ili watu wapate muda wa kupiga kura bila kukata tamaa basi iondoke (japo ujumbe ulishafika).

Nadhani kwa maandishi yako mkuu hapo unamaanisha nilikuwa nampigia kampeni Slaa waziwazi; ni jambo la kawaida kudaiwa UNATUMIWA au USHALIPWA etc... I normally take it
 
Haya uchaguzi umeisha, mwaga ukweli sasa :lol:
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…