Uchambuzi: Bomba la mafuta ya wizi Ungindoni, Kigamboni

DC alikuwa na haraka ya kuripoti ukitilia maanani uteuzi wa Ma DC ndio unafuata.Alitaka apate point ndio maana unaona ni kama amekurupuka hivi na kuifanya taarifa nzima ionekane kama haikuandaliwa vyema. Au hawana uhakika.
Na hili no tatizo kwa viongozi wengi na baadhi ya watanzania, Yeye kama kiongozi wa wilaya bado angeweza kupata credits zake bila kwenda public namna hiyo, maana pamoja na yote, details za hiyo habari zinatia doa nchi sana ukizingatia tunapambania dili ya bomba la mafuta ghafi toka Uganda, na kama nilisikia vyema ni kuwa Mseven anategemea pia kushusha mafuta masafi kurudi Uganda kwa matumizi yao.

Vitu kama hivi, viongozi wazalendo wenye uelewa mpana wa maslahi ya nchi, pamoja na kuwa kuna uhujumu mkubwa umefanikiwa kuubaini, lisongeshe suala kama hilo kwa mifumo ya kiserikali, sio lazima kwenda public namna hiyo, yaani mnataka kuita wawekezaji hapo hapo mna expose watakavyoibiwa tena inaonekana wataibiwa kimfumo?

It's a shame... Viongozi wajitafakari sana kutumia hizo camera kila mahala wanakwenda just for publicity tu...

NB: sijatetea wizi uliofanyika, ila nimetoa mtazamo kuhusu kurushwa kwa taarifa hiyo public, ukizingatia tunategemea kuhodhi bomba refu la takribani km 1000 kwa ajili ya jirani zetu Uganda.
 
Kazi iendelee... Naam Mkuu, maneno kuntu kabisa. Sihitaji kuongeza chochote maana haya uliyoyaandika yamejitosheleza...
Ingekuwa enzi zile tusingemwona DC bali tungelimwona Mkuu wa kaya mwenyewe na media kibao...
Huyu DC atatishwa sana lakini je hao waliokuwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na mkoa walikuwa wapi miaka yote miwili?
Je ikiwa hivi ndivyo inabidi maeneo mengi yakaguliwe hata ikibidi ardhi ipinduliwe ili haya "mahujumu na majambazi" yote yabainike na hatua stahiki zichukuliwe isiishie kutaifisha mali zao walizodhulumu tu...
Wengi wana majumba na magari ya kifahari je ni kwa mshahara upi na miaka mingapi ya utumishi wao?
 
Hili bomba ni wazi bado linahujumiwa na pengine litaendelea kuhujumiwa kama hatua stahiki hazitachukuliwa
 
Hili bomba ni wazi bado linahujumiwa na pengine litaendelea kuhujumiwa kama hatua stahiki hazitachukuliwa
Huu ndio ukweli mchungu wenye kuleta ukakasi kwa watumishi wa umma wenye nia ovu...
Wajisahihishe na wamulikane ili kuondosha hii hali...
 

Inaelekea yale aliyokuwa anahubiri Jiwe yalikuwa hayaendani na matendo yake hivyo hata wale wasaidizi wake waliokuwa wanaona yale aliyokuwa anafanya nao wakawa wanafanya vile vile!!! Mfano mdogo ni jinsi alivyokubali kampuni ya Barrick kupunguziwa madai toka us$191 billion mpaka us $300million tena zilipwe kidogo kidogo!!!

Yeye mwenyewe ndio aliyetuaminisha kuwa Barrack alikuwa wanatuibia maliasili yetu kwa kusafirisha mchanga usiochenjuliwa nje ya nchi halafu yeye huyo huyo akaja badirika na kuruhusu mchanga kupelekwa nje!!! Kuna mambo mengi yanayoibuka sasa yanayoashiria kuwa mwendazake alikuwa anatulisha matango pori!!
 
Nimekasirika hata nashindwa kutoa comments.
 
Bado wapo watakaokuja na plan za PhD,

Mwenye nyumba namhurumia especially kama yeye hakujua nini kinaendelea zaidi ya kufurahia kodi.

Hizo hesabu zako nazikataa, nina wivu, zimeashum ni kwamba kila siku meli zinapakua mafuta na hao wezi kila siku wanawasha mitambo ya kunyonya mafuta.
Wenye biashara za mabasi na malori na visima binafsi vya mafuta, kwenye yard wakaguliwe hawa kwanza.

Hapa naamini vijiniasi vibaharia vya TRA, TPA, TPDC viuza info vilikuwepo na vinahusika. Unakuta tutoto tudogo tunamiliki mambo makubwa. Kuna vijitu vya IT. Haya tuendelee kusikilizia mengi tutayajua.

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Umemaliza mkuu, hiyo biashara ilikuwa ya kimkakati, na wao walitakiwa waende kimkakati. Issue kama hiyo sidhani hata DC ni size yake. Sijamsikia PM wala zagazaga zingine kuongelea... bungeni ndio kabisa wanajadili Simba na Yanga mara mbunge alievaa suruali. Nnjii Hii ni shida kweli kweli
 
Kuna muvi nliwahi cheki ya namna hii kila nikipita pale BOT nawaza kutenda dhambi
 
Mostly ni inside job.. Sidhani kama ni coincidence ama la lakini baada ya hili tukio the next day mafuta yakapanda juu.. Sijui kama kuna uhusiano ama la

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…