Uchambuzi huru kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba, 2020

Uchambuzi huru kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba, 2020

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
15,923
Reaction score
40,246
Heshima kwenu wana jf

Tukiwa tunakamilisha zoezi la kupata wagombea kutoka kwenye vyama vyetu vya siasa, si vibaya kufanya tathmini za haki na kistaarabu kuhusu mwenendo na matazamio ya uchaguzi ulio mbele yetu.

Hoja yangu ya kwanza ni mwamko wa wapiga kura, kwangu naona kama vile hamasa imepungua au pengine ni mapema sana kufikia maoni haya.

Pili nawaza mustakabali wa wahanga/majeruhi walio katiwa umeme na wajumbe kutoka vyama vyote, lakini zaidi ni wale walioacha nyadhifa zao, je wanaweza kupata suluhu nyingine katika teuzi za nafasi za kisiasa.

Si vibaya tukatoa maoni, bila uchochezi.
 
Umejuaje kuwa hamasa imepungua?
Umefanya utafiti?
Ndiyo umefanya umefanya eneo lipi na lipi kwa muda gani?
Tuanzie hapa
Iko wazi sana, kwa bahati nzuri mwaka 2015 nilikuwepo sehemu ambayo nipo leo, hivyo naona kwa macho na kusikia kwa masikio
 
Iko wazi sana, kwa bahati nzuri mwaka 2015 nilikuwepo sehemu ambayo nipo leo, hivyo naona kwa macho na kusikia kwa masikio
ninachoweza kusema NI Tukae na Tusubiri..Muda Uwe hakimu wetu.....
Japokuwa Kila nikikaa Kujadili na Jamii inayonizunguka Kuhusu Uchaguzi .. Wengi Tunatamani Uchaguzi Uwe was Huru na Haki...Hivyo inatosha...
 
Ni matumaini ya kila mpenda demokrasia kwamba uchaguzi uwe huru na wa haki
 
Jiwe anaogopa sana siasa na amejitahidi sana kuzima shamrashamra za kisiasa anataka apitishwe bila kupingwa kama alivyolazimisha ccm kumpitisha. Ila Umma utaongea Oktoba.
 
Back
Top Bottom