Uchambuzi: Je, nini Robertinho ilibidi afanye ili kukwepa mnara wa 5G

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Salam Wana jf [emoji113][emoji113][emoji23]

Kabla ya mechi robertinho ilibidi aweke msisitizo mkubwa kwenye viungo ( kukaba sana) Ili kusumbuana na viungo wa Yanga

Kosa alilofanya robertinho ni kuruhusu mchezo wa kupishana na viungo wa Yanga ....coz kiasili wachezaji wote wa Yanga Wanakaba wakipoteza mpira .......lkn Chama, Phil.....hawakabi

Mwisho kabisa zilipofika goli 3 robertinho ilibidi atoe timu uwanjani akimbie ...... wanyakyusa tunasema heri nusu Shari kuliko Shari KAMILI

Hamsa [emoji113][emoji113][emoji23]
 
Suala lipo wazi, yanga ni wana faida ya viungo, ukiacha na aucho na mudathiri ambao kinafasi ni viungo, kuna pacome, max na aziz ki ambao hawa kiuchezaji wana faida kubwa kwenye kiungo, ukiwa nao ni kama una viungo wengine wa kati, ambapo mwisho wa siku ikawa yanga midfielders wa5 vs wawili wa simba, yanga walituoverload simba pale kati

Kuwadhibiti hao si jambo jepesi jepesi kiuhalisi(kwa sababu simba haina midfielders wazuri, ukimtoa ngoma, ambaenae hawezi kumudu mziki wa watu wa5)
Robertinyo at least angecheza 4-4-2 diamomd formation, watu wa soka wananielewa nikisema diamond formation.
Dm angekuwa ngoma
LCM akawa mzamiru
RCM akawa kanoute.
Mzamiru na kanoute kidoogo wangeweza kuleta fujo pale kati, japo si CM nzuri zinakosa sifa nyiingi, hasa kutuliza timu na kupiga pasi sahihi na uchaguzi wa sehemu sahihi wa kupiga pasi, ila wangeleta fujo fujo, ngoma angeweza kuoperate kiurahisi kidogo.
Juu yao kwenye attacking midfielders angesimama chama.
Na kwanini chama si saidoo, chama anauweza wa kucheza na timu na kuichezesha timu, anauwezo wa kukomandi timu icheze vipi haswa akiwa na mpira mguuni.

Juu kabisa akamtumia aidha phiri na kibu au phiri na baleke(ila phiri asikosekane, kwanini, kwa sababu phiri anauwezo wa kushuka chini aka link up timu, akasogea nayo juu kimchezo, so angejikatia eneo lake kama Ls, yaani kuna wakati anakuwa striker anakuwa winger wa kushoto, kisha kibu akafanya fujo zake kutokea kulia)

Hi kidoogo ingeleta nafuu,

Nguvu ya yanga ni pale kati, hili nalizungumza hata msimu uliopita yanga walikuwa wanaweka sana boli chini na hii ni sababu ya midfielders wao wengi ni wazuri, ukitoa ngoma na chama wengine woote pale simba hawapati namba pale yanga(nazungumzia eneo la viungo)
 
Fact kabisa....Simba wakipoteza mpira walikuwa wanatembea tu
 
Huo mfumo ungewapa nafasi Yao na Lomalisa KuOverlap na kuleta madhara.
 
Mkuu makaveli10 salam kwako.
Hongera kwa uchambuzi mzuri. Je mkuu makaveli10 haukoona fitness ya wachezaji wa simba ni Questionable? Je hukoona issue ya rotation kwa wacheji wa simba inatakiwa kuwa addressed ili kutengeza Match fitness kwa kundi kubwa la wachezaji? Mkuu tuende mbele na turudi nyuma, je unadhani kutumia formation uliyosema wakati wachezaji wana uchovu wa match ingesaidia chochote?
Ahsante
 
Mpira una mambo mengi saana mkuu,

Sikupingi ndugu yangu, kwangu siwezi sema ni match fitness, sababu madhaifu ya kimfumo ndio yaliyotangulia, siwezi kusema match fitness ama kuchoka, wachezaji wa yanga wengi pia wametumika, kwangu simba walikuwa wanahitaji compactness, kupambana na wale viungo wa yanga pale ndani, ukitizama vizuri utaona kina ngoma ni kama walikuwa wametengwa, flow ya timu kutoka chini ilikuwa inaishia kwa ngoma na kidoogo kanoute, kisha wanabutua mbele (long pass), na si kwa gamr hii tu ni game nyingi mnoo simba wanacheza hivyo watizame, labda kocha abadilike tizama hata game ijayo ya simba.
 
Angepress hard kwenye kushambulia halafu awanyime Yanga Uhuru wa kucheza kama alivyofanya kwenye Simba 2-0 Yanga. Kuwaacha Yanga wachezee mpira kwa uhuru vile ipo siku hamsa itazaa hamsa mwezie[emoji1787]
 
Wangemuhonga Refa. Sijui kwanini wamesahau this time hadi tunadhalilika kiasi hiki
 
Makolo, mnahitaji kusajili wachezaji wa maana. Kwa team mliyonayo sasa hivi, nje ya first eleven, ni mchezaji mmoja tu au wawili ndio wanaweza kuleta impact uwanjani. Wengine wote magarasa.

Matokeo yake, mmekua mkiwatumia wachezaji walewale kila siku, kila mechi bila kufanya rotation kwa sababu benchi hakuna watu. Mbaya zaidi, wachezaji hao mnaowachezesha kila siku, umri umeenda sana. Matokeo yake ni exhaustion ya kufa mtu.

Game ya jana ilikua ni total domination, sio physically wala technically. Tuliwakamata kila sehemu!

NB: Wakati Gamondi anahudhuria mechi zenu mlimkashifu, mkamualika aje na mazoezini. Laiti mngejuaaaaa!
 
Hii kweli ingeleta faida kwa mnyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…