Suala lipo wazi, yanga ni wana faida ya viungo, ukiacha na aucho na mudathiri ambao kinafasi ni viungo, kuna pacome, max na aziz ki ambao hawa kiuchezaji wana faida kubwa kwenye kiungo, ukiwa nao ni kama una viungo wengine wa kati, ambapo mwisho wa siku ikawa yanga midfielders wa5 vs wawili wa simba, yanga walituoverload simba pale kati
Kuwadhibiti hao si jambo jepesi jepesi kiuhalisi(kwa sababu simba haina midfielders wazuri, ukimtoa ngoma, ambaenae hawezi kumudu mziki wa watu wa5)
Robertinyo at least angecheza 4-4-2 diamomd formation, watu wa soka wananielewa nikisema diamond formation.
Dm angekuwa ngoma
LCM akawa mzamiru
RCM akawa kanoute.
Mzamiru na kanoute kidoogo wangeweza kuleta fujo pale kati, japo si CM nzuri zinakosa sifa nyiingi, hasa kutuliza timu na kupiga pasi sahihi na uchaguzi wa sehemu sahihi wa kupiga pasi, ila wangeleta fujo fujo, ngoma angeweza kuoperate kiurahisi kidogo.
Juu yao kwenye attacking midfielders angesimama chama.
Na kwanini chama si saidoo, chama anauweza wa kucheza na timu na kuichezesha timu, anauwezo wa kukomandi timu icheze vipi haswa akiwa na mpira mguuni.
Juu kabisa akamtumia aidha phiri na kibu au phiri na baleke(ila phiri asikosekane, kwanini, kwa sababu phiri anauwezo wa kushuka chini aka link up timu, akasogea nayo juu kimchezo, so angejikatia eneo lake kama Ls, yaani kuna wakati anakuwa striker anakuwa winger wa kushoto, kisha kibu akafanya fujo zake kutokea kulia)
Hi kidoogo ingeleta nafuu,
Nguvu ya yanga ni pale kati, hili nalizungumza hata msimu uliopita yanga walikuwa wanaweka sana boli chini na hii ni sababu ya midfielders wao wengi ni wazuri, ukitoa ngoma na chama wengine woote pale simba hawapati namba pale yanga(nazungumzia eneo la viungo)