Uchambuzi: Kuna Dalili Wakenya Wanakwenda Kumchagua 'Jogoo Mwembamba' (Uhuru Kenyatta)...!

Uchambuzi: Kuna Dalili Wakenya Wanakwenda Kumchagua 'Jogoo Mwembamba' (Uhuru Kenyatta)...!

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,246
Ndugu zangu,
Afrika ukikuta jogoo wawili wanagombana, basi, hapo hapakosi mashabiki. Na kila shabiki aliyesimama kutazama mpambano wa majogoo hao, ujue, kuwa ana jogoo wake anayemshabikia.

Na jogoo anayemshabikia akishindwa pambano, shabiki ataondoka akisononeka. Kuna ambao watakosa hata hamu ya chakula siku hiyo. Kisa? Jogoo wake kagalagazwa!

Na kama jogoo mmoja ni mnene na mwingine ni mwembamba, ujue, kuwa jogoo mwembamba ana mashabiki wengi.

Ukifuatilia mwenendo wa Uchaguzi wa Kenya kuna dalili kuwa Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai anaelekea kwenye kupata ushindi.
Moja ya tafsiri ya jambo hili ni ilivyo kwenye fikra za wapiga kura ambao ni wengi ni watu wa kawaida- kuwa Uhuru anaonewa, hata na mataifa ya nje. Kwamba mambo ya Kenya yao yanaingiliwa pia na wasio Wakenya, tena Wazungu.

Wakenya wana historia ya mapambano magumu ya kudai uhuru kutoka kwa ' Wazungu'- ni tangu enzi za Mau Mau.

Pamoja na utajiri wake, bado Wakenya wengi wa kawaida wanamwona Uhuru kama mtu wanayefanana naye. Ni mwanadamu kama wengine. Hujo nyuma Uhuru amekuwa na historia ya matatizo binafsi pia ya kimaisha, ikiwamo matatizo ya pombe, hivyo ya kifamilia pia. Wakenya wengi wanaishi wakijisikia kuwa wananyanyaswa na kuonewa. Wanamwona Uhuru Kenyatta kuwa ni mtu anayeonewa pia.

Hivyo, yawezekana kuna kura za ' kuonewa huruma' ambazo Uhuru Kenyatta anaweza kuzipata, hata kutoka kwa watu wa kabila la Wajaluo. Wanaojiona ' wanafanana naye'.

Na lingine ambalo laweza kutokea ni ukweli, kuwa katika matatizo mengi wanayoyakabili Wakenya kwa sasa, kuna ambao wanaikumbuka ' Bora ya jana' ya Mzee Jommo Kenyatta. Wanaikumbuka historia. hivyo, kuna Wakenya waliopiga kura za ' nostalgie'- Kura za ' Zilipendwa'.

Kuna Wakenya wengi walimpenda Mzee Jommo Kenyatta. Bado wanakumbukumbu za ' Fuata Nyayo'. Na Uhuru naye anaitwa ' Kenyatta'- Jina lake la pili. Ni mwana wa Mzee wa ' Fuata Nyayo.

Naam, Nyayo zilishapotea. Kuna wenye hamu ya kuzitafuta. Wanaamini Uhuru atawasaidia kuziona. Na tusubiri tuone.

Maggid Mjengwa,
Msamvu, Morogoro
 
Mi naamini uchaguz wa kenya umetawaliwa na ukabila....
Hii issue ya ukabila ni mbaya sana na iliasisiwa na mzee Kenyata.

Ni vigumu sana kulikana kabila lako. Jitazame wewe kwanza, je ikitokea kabila lako linapambana na kabila lingine utasimama wapi?. Ukabila si kumchagua aliye kabila lako. La hasha, waweza kuwa Mpemba ukampigia kura ------ lakini ukabaki kuwa mkabila nambari wani. Odinga anaungwa mkono na mabeberu kutoka nje, hii nayo inamwathiri sana.
 
wacha Wakenya wawakomeshe wanafiki na ICC yao. Wacha Kenyatta na arap Ruto washinde ndio tuone test of the ICC laws itakiwaje a sitting president na vice president kama Fatou Mbesuda atawasimamisha kizimbani. Natamani Kenyatta ashinde nione nguvu za ICC.
 
...Tujikumbushe...

Last edited by a moderator:
Cord wanaanza kupiga mayowe. Nasikia Prof. Anyang Nyong anapiga yowe
 
Wale ambao walikuwa na ufahamu wa kutosha enzi za Kenyatta, ningeomba wanipe ABC za Jomo Kenyatta(babae Uhuru) VS Jaramong Oginga Odinga(Babae Raila)
 
Ni habari mbaya sana kwangu,nilitamani Raila ashinde.

Kwangu mimi, it doesn't matter....whether Uhuru or Raila since nawaona wote hawana maono tofauti dhidi ya TZ unless kama tutanaka kuzungumzia CCM na CHADEMA kwa kile ambacho wengine wanaamini CDM is Raila nd CCM is for Uhuru!
 
................, je ikitokea kabila lako linapambana na kabila lingine utasimama wapi?. ........

Hii ni lugha kama ya ccm kuwa "2015 tutalikomboa jimbo fulani linaloongozwa na CDM!" hao CDM ni wakoloni wa wapi? Taifa gani? Jamani tujitahidi kuwa na lugha laini kwani sisi ni wamoja hata ccm au CDM ikiwa madarakani.

Kwangu, awe Kenyatta au Odinga ni sawa kwani wakenya watakuwa wakenya kama ilivyo Kenya 1 kwao wote.
 
nitafurahi sana kama Kenyatta atashinda na kuwa rais wa kenya
 
Wale ambao walikuwa na ufahamu wa kutosha enzi za Kenyatta, ningeomba wanipe ABC za Jomo Kenyatta(babae Uhuru) VS Jaramong Oginga Odinga(Babae Raila)

Wakristo wanaamini kuwa ukiokoka, dhambi za zamani japo zilikuwa nyekundu zitakuwa nyeupe kama theruji! Kenya imekuwa mpya kwa historia ya sasa, tuangalie historia mpya badala ya kuchimbua chimbua historia zinazorudisha tulikotoka hata zikatuletea kuchukiana!
 
Ni vigumu sana kulikana kabila lako. Jitazame wewe kwanza, je ikitokea kabila lako linapambana na kabila lingine utasimama wapi?. Ukabila si kumchagua aliye kabila lako. La hasha, waweza kuwa Mpemba ukampigia kura ------ lakini ukabaki kuwa mkabila nambari wani. Odinga anaungwa mkono na mabeberu kutoka nje, hii nayo inamwathiri sana.
sio kweli
 
Majjid,

huwa nakukubali sana kwa uchambuzi wako wa masuala mbalimbali lakini kwenye hili uko very shallow, yaani hakuna sababu za msingi wakenya walizotumia kumchagua Uhuru zaidi ya ulizotaja? Hujamt.ndea haki Uhuru wala wakenya waliomchagua/
 
hadi sasa mchauno ni mkali na percentage za UHURU zinazizidi kushuka japo taratibu huku za RAILA zikiwa zinapanda pia pole pole...kutakuwa na duru ya pili hapo kwa mtazamo wangcoz hadi muda huu
UHURU 1,794,283=54.27%
RAILA 1,360,809=40.97%
kila la kheri RAILA
MUNGU bariki WAKENYA
 
Ni vigumu sana kulikana kabila lako. Jitazame wewe kwanza, je ikitokea kabila lako linapambana na kabila lingine utasimama wapi?. Ukabila si kumchagua aliye kabila lako. La hasha, waweza kuwa Mpemba ukampigia kura ------ lakini ukabaki kuwa mkabila nambari wani. Odinga anaungwa mkono na mabeberu kutoka nje, hii nayo inamwathiri sana.

Hilo neno ulilowekea dash dash ni mchaga.........
 
Back
Top Bottom