UCHAMBUZI: Kwanini ni vigumu sana kumzima The Bongofleva Music Trade Mark "Diamond Platnumz"?

Oya Tusepe

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2016
Posts
265
Reaction score
870
Salam,

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakishindwa kuelewa kwamba katika jamii yoyote kupata umaarufu na heshima kuna gharama yake, tena gharama kubwa!.

Twende sambamba katika uchambuzi huu ili uweze kuelewa kinagaubaga, ya kwamba ni kwanini ni vigumu kumpoteza kijana Naseeb Abdul na kuizima kabisa nyota yake?

Kwa wanaofuatilia game ya mziki wetu wa Bongo wanaelewa kwamba Diamond si msanii wa kwanza wa kizazi kipya kupendwa sana na mashabiki zake, wapo watu waliowahi kuhusudiwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na kupata mafanikio makubwa mfano tunae bwana Nice Mkenda, Mr Nice na wengine wengi.

Baada ya Diamond Platnumz kupokelewa rasmi na wa Tz wenzake kwenye game ya mziki, upepo wa sanaa nzima ya uimbaji wa Bongo ulibadilika kabisa jambo liliongeza speed ya kazi nzuri zaidi kutoka kwa wasanii wengine..

Pius unajaribu kusema nini?!!..

Anhaa.. Ninachojaribu kusema ni kwamba, unakumbuka video za wanamuziki wa Tanzania kabla ya ujio wa mtoto wa Tandale? Uvaaji je? Uzingativu wa mambo ya Muonekano kuanzia sura mpaka mwili mzima ikiwa ni pamoja na "fitness".. Mbinu mbalimbali za scandel za kibiashara? Attention ya media?.. Mambo haya yalifanya watanzania bila kujali lika kuanza kuwa makini na kufatilia burudani na vitimbwi vya ndani ya nchi yao katika upande wa sanaa ya uimbaji kwa kasi kubwa.

Pius mbona kama sijakupata vizuri?..

Ok ngoja niseme hivi: Hivi unajua kwamba hata mitindo ya uvaaji wa vijana wa kibongo imekuwa influenced pakubwa na kijana Diamond Platnumz? (Kubali au kataa ni juu yako).

Diamond Platnumz amejitengenezea ufalme katika akili za vijana wengi sana wa Tanzaia, wanamsikiliza na wanafanya anachofanya au anachotaka yeye.

Vijana wapya kwenye game wanashindwa kuelewa jambo moja ambalo ni kubwa sana kibiashara, kutengeneza Ngome.

Unapoanza biashara yoyote ile jambo la kwanza unalopaswa kulizingatia sana ni Aina gani ya wateja unaoenda kudeal nao.

Watanzania ni watu wanaowaheshimu sana wale vinara wanaoanzisha mambo makubwa au kuleta mabadiliko.

Fikiria jambo moja.. Hivi ulishawahi kujiuliza ni nini kitatokea endapo atashindanishwa Diamond Platnumz na Juma Nature " kiroboto" nini kitatokea? Amini usiamini Nature ataibuka mshindi.. Kwanini? Kwa sababu watanzania wanawaheshimu waanzilishi.

Kulingana na mambo ambayo Diamond Platnumz ameifanyia nchi ya Tanzania daima mchango wake hautafutika abadan.. Ni mbunifu na ni moja kati ya wasanii wachache unayeweza kusikilza playlist ya nyimbo zake zote bila kuchoka kuanzia asubuhi mpaka usiku, anafanya kazi nzuri.

Fikiria jambo jingine.. Yupo wapi Fundi Rich mavoko? Ommy Dimpoz, Ali Kiba, Asley na wengine wengi wenye sauti za kuvutia? Mbona hawana ushawishi mkubwa kama bwana Nasseb? Kuna makosa.

Diamond Platnumz ni kama Clouds Fm tu.. Ili kuviondoa hivi vitu mchezoni inahitaji muda na kizazi kingine.. Mtu mmoja anayeitwa Warren Buffet àliwahi kusema kila kampuni itaweza kudumu kwenye soko na kuwa stable katika ubunifu wa kawaida kwa muda wa miaka 30 na kama ubunifu hautaongezeka hata zaidi basi kampuni hiyo itafutika na kusahaulika kabisa.. Warren anazungumzia swala la generation.

Nitoe rai kwa vijana wanaojaribu kumchalenji bwana Nasseeb tena kwa kugeza mbinu zake za kibiashara kwamba WAKAE CHONJO na kwa tahadhari kubwa.

Mwisho napenda kutoa ushauri kwa kijana Konde boy kwamba afanye kazi na atafute ubunifu mpya na sio kuiga iga mambo.. Na wala usitafute kuonewa huruma na yeyote. Apambane kutengeneza Ngome yake mpya kwakuwa ni suala na muda mrefu.
 
Diamond ni msanii mwenye nguvu sawa na media na ana fans base kubwa kuliko msanii yoyote Tanzania eti kusema kuna mtu atampindua ataanza yeye kupindua kwanza na ndomaana Kuna media fulani zilijaribu kutaka kumdondosha lakini zikashindwa.
 
Tanzania Siku Hizi Ukiwa Na Vipesa Fulani Au Madaraka .....!!


Unaabudiwa Kinyama.

Ni Nyimbo Za Kukusifu Na Kukuabudu Mwanzo Mwisho.
 
Kwanini watu mnafikiri kuna njama ya kumpindua?

Maana kiukweli,kama yanayosemwa kuhusu njama kwa diamond yangekuwa kweli,basi mondi asingekuwepo leo.

Kuna wajinga walimfuata kwa kusema marehemu aliwabania,sasa ametangulia mbele za haki ila wako vile vile.

Yeye ajue tu,hakuna mtu mwenye nia mbaya na yeye ila wenye nia nzuri wapo.
 
Diamond ni icon na hakuna na hatatokea kama diamond katika hii dunia kwa ujumla na Tanzania pia
 
Ndo mana hujapata like,maana umeongea pumba zilizo changanyikana na mashudu
 
Konde boy unampa ushauri baada ya kutoka?

Naseeb ana influence sana, mpaka ma x wake wote wanamzimia tu

Nahisi kabisa wewe ni mmoja wa x zake, sidhani kama mtoto wa kiume unapata muda wa kuandika uchambuzi uchwara huu
 
kumuangusha chibu ni sawa na kuzuia ngumu kwa kufumba macho, itaingia TU.
 
Zile scandal za kutoka na wema zilinyanyua juu jina LA mond, hata zari nae ka mboost sana.
 
Tatizo la Ali kiba ni kupenda ma shugar mamy sasa hivi angekuwa mbali maana yeye na Mr Blue ni wa kitambo kipindi wana hit Chibu sijui alikuwa wapi.
 
Nyota ya Diamond inategemea mafuvu na wanawake. Ndio maana daima ana totoz na office kwake kuna fuvu
 
Ndo mana hujapata like,maana umeongea pumba zilizo changanyikana na mashudu
Mtu mpaka akupe like,si kwa sababu umeongea nafaka na kiini,ila umeandika kama anacho waza.wewe umepata likes 2 kati ya member laki tano ndani ta jukwaa.

Inawezekana uliiandika hii post ukiwa umebanwa haja.kaangalie tena.
 
Nyota ya Diamond inategemea mafuvu na wanawake. Ndio maana daima ana totoz na office kwake kuna fuvu
Yaani akilizako zinakwambia unapenda nyimbo za diamond kwa sababu ameweka fuvu ofisini mwake? Watanzaniawatanzania ohhh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…