PostGE2025 UCHAMBUZI: Maswali 10 Muhimu Kuhusu Ripoti ya Tume ya Jaji Chande

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Jaji Chande.png
Hatimaye Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imetoa ripoti yake baada ya kufanya uchunguzi kwa siku 153.

Tume hiyo iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman, ilikuwa na wajumbe wanane ambao ni: Dkt. Stergomena Tax, Jaji Mkuu mstaafu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Balozi Ombeni Yohana Sefue, Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Said Ally Mwema, Balozi Paul Meela, Balozi David Kapya, Balozi George Madafa, na Balozi Radhia Msuya.

Awali, tume hiyo iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan mnamo Novemba 20, 2025, ilipewa siku 90 za kufanya kazi. Hata hivyo, ilipofika Februari 20 ikaomba kuongezewa siku 42, na ilipofika Aprili 2 ikaomba tena kuongezewa siku 21, ambazo zilikamilika Aprili 23, 2025, na ripoti kukabidhiwa.

Japo baadhi ya vyama vya siasa, ikiwamo CHADEMA na ACT-Wazalendo, pamoja na baadhi ya wanaharakati walishatoa msimamo wa kutoitambua tume hiyo, tunaweza kuitazama na kuichambua ripoti yake kwa kujiuliza maswali kumi yafuatayo:

1. Vichocheo vya Ghasia na Kauli za Kisiasa

Wakati Jaji Chande anataja vichocheo vya maandamano, alisema kulikuwa na kauli za baadhi ya wanasiasa ambazo zilikuja kugeuka kuwa kaulimbiu za waliokuwa wanafanya ghasia. Baadhi ya washiriki walikiri kutumia kaulimbiu kama vile:

  • “No Reforms No Election”
  • “Oktoba Tunatiki”, “Oktoba Tunatoka”
  • “Tumedhamiria uchaguzi hautafanyika”
  • “Samia Must Go”
  • “Tunataka kuikomboa nchi yetu”
  • “Hakuna uchaguzi chini ya Serikali hii”
  • “Tutahakikisha nchi haisimami mpaka Serikali iondoke”
  • “Hakutakuwa na Uchaguzi bila mabadiliko ya mfumo”
  • “Serikali hii imepoteza uhalali wa kuongoza nchi”
  • “Mchakato wa kuwapata wagombea umekiuka taratibu, urudiwe”
Swali: Kwa nini Tume inaamini kwamba hivi vilikuwa vichocheo? Kulikuwa na kipimo gani kwamba haya ni maandalizi ya ghasia na sio majigambo tu ya kisiasa?

Hapo wapo wanaoamini kwamba hata kauli za Rais Samia zilikuwa na uwezekano wa kuchochea ghasia. Mathalani, kauli yake maarufu: "Tumejipanga vyema kuilinda nchi hii. Kwa hiyo hakutakuwa na nywinywinywi wala nywinywinywi. Naomba watu tokeni, amshaneni kampeni mpige kura." Au ile aliyoitoa Oktoba 22, 2025, kwenye kampeni Leaders Club: "Nataka niwaambie, maandamano yatakayokuwepo ni ya watu kwenda vituoni kupiga kura, hakuna maandamano mengine. Hakuna tishio la usalama litakalokuwepo. Anayesema ni Amiri Jeshi Mkuu." Je, Tume imepima vipi mizani ya kauli hizi zote?

2. Kupangwa na Kuratibiwa kwa Ghasia

Jaji Chande alisema matukio ya ghasia za Oktoba 2025 yalipangwa, yaliratibiwa, yalifadhiliwa, na kutekelezwa na watu waliopata mafunzo.

Swali: Je, hii inamaanisha kwamba Vyombo vya Ulinzi na Usalama havikuwa na taarifa za mipango hii yote? Mbona tuliambiwa kuwa Jeshi la Polisi limejipangwa na lina vifaa vya kisasa? Ina maana hata Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) haikuwa na taarifa wala kuweka mikakati ya kudhibiti ghasia hizo kabla hazijatokea?

3. Uwepo wa Kambi 28 za Mafunzo

Jaji Chande alisema kulikuwa na kambi 28 za maandalizi ya ghasia hizo.

Swali: Yaani kuwe na kambi 28 halafu TISS wasijue, Polisi wasijue, na JWTZ wasijue? Hapa Jaji Chande anataka kuonyesha udhaifu wa vyombo vyetu vya usalama au anadhani kwa kusema hivyo ataongeza uzito wa ripoti yake? Kama nchi inaweza kuwa na watu wanaotengeneza kambi na kufundisha uasi bila Serikali kujua chochote, maana yake hatuko salama tena.

Kitu kinachoshangaza zaidi, anasema moja ya kambi ilikuwa umbali wa mita 10 tu kutoka kituo kimoja cha Polisi jijini Dar es Salaam. Ndiyo kusema vyombo vyetu vilizembea kiasi hicho? Mbaya zaidi, hatataji kambi hizo ziko wapi na ziligundulika lini. Hili linaibua hisia za mashaka na uvumi.

4. Ufadhili wa Shilingi 10,000 hadi 50,000

Tume imeeleza kuwa waandamanaji walipewa ujira wa kati ya Sh. 10,000 hadi Sh. 50,000. Hata hivyo, haikusema Tume ilibaini fedha hizo zililipwa kwa njia gani. Je, zililipwa taslimu? Kwa miamala ya simu? Benki? Ushahidi wa malipo hayo uko wapi?

Swali: Jaji Chande alisema watoa taarifa ndio waliosema. Je, Tume ikaamini tu maelezo ya watoa taarifa bila kudai ushahidi wowote? Kama Jaji Mkuu mstaafu, anawezaje kukubali madai mazito kama haya bila kuweka ushahidi bayana?

5. Majina ya Waratibu na Wasimamizi Kufichwa

Tume iliyotumia siku 153, imeshindwa kuweka wazi majina ya watu walioratibu na kufadhili vurugu hizo. Jaji Chande amejitetea kwamba hawawezi kutaja wanaotuhumiwa kuratibu au waliotekeleza mauaji, kwa kuwa wangetakiwa kuwaita ili kusikiliza upande wao.

Swali: Walishindwaje kuwaita hao watu ili kuthibitisha madai hayo? Inamaana Tume imekusanya taarifa tu na kuzipachika bila kuzithibitisha popote? Je, mtu akisema Tume imetengeneza hisia zisizo na mashiko atakuwa anakosea?

6. Waliohusika na Mauaji ya Wananchi 518

Ni kina nani waliohusika kuua wananchi 518? Hapa pia Jaji Chande alikwepa lawama akisema tume yake haipo kwa ajili ya kutaja watu.

Swali: Hao watu walijiua wenyewe? Au waliuawa na waandamanaji wenzao? Kama sio Polisi waliokuwa na silaha za moto, ni nani mwingine?

Wakati Jaji Chande akikwepa kutaja ukweli huu, ikumbukwe kuwa Desemba 2, 2025, Rais Samia akizungumza na wazee wa Dar es Salaam, alisema nguvu iliyotumika ilistahili, kwani isingetumika waandamanaji wangepindua Serikali yake. Kwa kauli hiyo, alionekana kuhalalisha matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji (yakiwamo mauaji) ili mradi tu Serikali isipinduliwe. Hata alipokuwa akipokea ripoti hii Aprili 23, Rais alisema kama si kazi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama, hali ingekuwa mbaya zaidi.

7. Uhalali wa Nguvu Iliyotumika

Kama ilivyoelezwa kwenye swali la sita, kuna mkanganyiko mkubwa.

Swali: Kwa nini Tume imeshindwa kufafanua na kutoa tamko la kisheria kama nguvu kubwa iliyotumika dhidi ya raia ilikuwa sahihi, halali, na yenye uwiano (proportional)?

8. Suala la Uwajibikaji

Pamoja na uchunguzi wote huo uliogharimu muda na kodi za wananchi, Tume haijaona mtu wa kuwajibika.

Swali: Si Polisi, si Wanajeshi, si Maofisa wa Serikali, na wala si wanasiasa wanaodaiwa kuratibu hizo ghasia waliopendekezwa kuwajibishwa. Kama hakuna anayewajibishwa, je, hii ilikuwa ni Tume ya kujifariji tu?

9. Pendekezo la Kuunda Chombo Kingine

Jaji Chande ameshauri kuundwe chombo kingine cha kufanya upelelezi ili kuwabaini wahalifu.

Swali: Kwa nini Tume yake haikukamilisha kazi hiyo ili uwajibikaji ufanyike moja kwa moja? Kitendo cha kupendekeza kuundwa kwa chombo kingine ni dalili ya kuchelewesha uwajibikaji na kuficha ukweli halisi kuhusu matukio hayo.

10. Umiliki wa Ripoti na Kuficha Ukweli

Rais Samia amenukuliwa akisema ripoti hiyo "ni mali ya Rais," akionya watu wasije kudai umiliki wake.

Swali: Je, kwa kufanya hivyo, anaficha mambo ambayo Watanzania wangependa kuyajua na kujifunza ili maafa haya yasitokee tena? Nini hasa kinafichwa kwenye ripoti ambayo imetokana na kodi za wananchi walioumia?

Hitimisho

Kama kweli taifa hili linataka maridhiano ya dhati, ukweli ndiyo utakaoliponya. Ukweli huo unapaswa kuwa kama upanga ukatao kuwili, usioangalia sura wala cheo cha mtu. Kutokana na mapungufu ya wazi ya ripoti hii, ukweli huo utapatikana tu kwa kuundwa kwa Tume Huru ya Kimataifa isiyofungamana na upande wowote.
 
Mkuu umechambua vizuri sana. Kwa ufupi ni kwamba aliyeunda tume ni mtu batili , tume ni batili na ripoti yake ni batili. Hata tunapoijadili hapa tunafanya ubatili pia.
 
Kama kweli taifa hili linataka maridhiano ya dhati, ukweli ndiyo utakaoliponya. Ukweli huo unapaswa kuwa kama upanga ukatao kuwili, usioangalia sura wala cheo cha mtu. Kutokana na mapungufu ya wazi ya ripoti hii, ukweli huo utapatikana tu kwa kuundwa kwa Tume Huru ya Kimataifa isiyofungamana na upande wowote.
Hapa umemaliza kila kitu mkuu. Sitii neno lolote.
 
Ripoti hii ya Jaji chande na wabobezi wake naipa grade: F-
 
11) watufahamishe walee jamaa waliovaa jezi za yanga na wenzao wanakaa wapi?
 
Sijui ni kwa uzembe au makusudi huyu judge mstaafu kamkabidhisha mama yao rasmi kwenda kujibu ICC nani aliyewaua hata hao 518 tu japo kapunguza sana! Kabudu anamdanganya sana huyu mama kwamba watu hao ni wachache sana na dunia itapuuza tu! Muda utaongea na mbio za sakafuni huwa zinanasa mwisho wake! Alisema mzigo upo mabegani mwake ni kweli atakuwa accountable soon na chawa watamuachia zigo lake
 
Hii nchi ina laana!! Unashindwa kuamini mtu aliyeongoza hii tume, kwa report uchwara kama ile, iliwezekanaje kwa yeye kuwa jaji mkuu! Kwa report kama ile, kama hukupewa historia yake, ni vigumu kuamini kama imeandaliwa hata na hakimu wa mahakama ya mwanzo!!
Report nzima ni upuuzi inayotakiwa kupuuzwa na kila mwenye akili timamu. Haina chochote cha maana, zaidi ya hadithi zinazokosa uhalisia.
 
Halafu Kuna mtu kaikumbatia, eti "hii ni ripoti yangu"
 
Back
Top Bottom