PostGE2025 UCHAMBUZI: Maswali 10 Muhimu Kuhusu Ripoti ya Tume ya Jaji Chande

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hivi akisema ni mali yake ni kuwa hatutakaa tuisome public?
 
Hivi akisema ni mali yake ni kuwa hatutakaa tuisome public?
Anaweza kutuzuia tusiisome public lakini hawezi wazuia jumuia za kimataifa pindi zikihitaji nakala ya ripoti, hapo ndiyo ule msemo "unalinda bahari watu wasiogelee coco beach lakini watu wanaenda ogelea kijichi"
 
Nchi inazamishwa Shimoni na Wahuni Watanganyika tunaangalia tu.😭😭😭😭
 
Natoa report yangu ila namshukuru Mama Mia kwa kazi nzuri anayofanya 😥.
Tumelogwa?
WTTFFP with this people!
 
Bado sijaelewa...

Tume imedhibitisha kuwa
1. Yale hayakuwa maandamano bali vurugu
2. Vurugu zilipangwa na kuratibiwa

Kwa kifupi, vitendo vilivyofanywa na vyombo vilikuwa sahihi.

Sasa haya maridhiano, ni kati ya nani nani?

Polisi na Raia?
Raia na Raia?
Serikali na Raia?
 
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Wale wazee mtu hawezi kutegemea kama wanaweza kufanya jambo kama lile lakini ndiyo wameshalifanya.
 
"The absent of evidence is not an evidence that something doesn't exist. " Samuel Jackson
 
Ripoti ya Tume ya Uchunguzi imefichua picha ya kutisha ya ghasia zilizopangwa kwa ustadi mkubwa tarehe 29 Oktoba 2025. Si machafuko ya kawaida, bali shambulio lililoratibiwa na kutekelezwa katika mikoa kadhaa. Mashahidi wameeleza jinsi vijana walivyohifadhiwa na kufunzwa kwa siku 28+ katika misitu, majengo na kambi za siri. Hii inaonyesha mpango mkubwa uliowazidiwa. #SautiZaWananchi
#TumeYaUchunguziReport
Ripoti Ya Uchunguzi
 
1. Kwa hiyo tuseme serikali ni dhaifu.? Kama watu wanaweza kupanga, kuunda vikundi na kufundisha vijana kupindua serikali kwa miezi bila vyombo vya dola kujua maana yake serikali imeshindwa kufanya kazi yake ya ulinzi wa nchi.

2. Hadi sasa hakuna hata mtu mmoja aliyekamatwa kwa tuhuma za kugawa fedha, kufundisha vijana na nk. Je serikali inawaogopa hao watu. Yaani imebaki tu kusema kuna watu, walifanya A, B, C wako wapi?

3. Kama vyombo vya ulinzi na usalama vilishindwa kufanya kazi yake mbona haviwajibishwi?
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu sana, wanasema uongo ili kuwalinda wauaji. Uongo huu unadhalilisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuwa watu wanaweza kupanga hadi kutekeleza uhalifu huo bila kubainika. Hii tume ya ******* sana.
 
Kwahiyo hiyo ripoti mlikaa mkaipangilia kiustadi kabisa iwafikie watu na akili zao au mazezeta wasiojua kupambanua mambo?!
 
Vyombo vya usalama vilijua,ila vimeona waache wajitokeze kutoka huko walikojificha ili wanyooshwe iwe fundisho .
 
Katika andiko loooote point ya kuhoji ni no 2 pekee

Hapo hata mimi nataka uwajibikaji maana naamini kuna traitor na moles ndani ya vyombo vya ulinzi na hasa usalama wa Taifa (TISS)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…