mrxtz2026
JF-Expert Member
- Jan 24, 2026
- 609
- 1,314
Uzi huu ni wa uchambuzi na Tathmini ya Final Submission Ya kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Antipas Lissu (TAL) Vs Jamhuri.
Katika Hatua hii ya Kesi "Final Submission".
LISSU akijitetea mwenyewe kwa kufanya Finalizing ya Ushaidi, hoja na Kukosoa Miendendo ya Kesi, Kukosoa Mashaidi wa mashtaka na Mengineyo mengi.
Katika Final submission hiyo Linaibuka swali la Kisheria ambalo ndilo lilozaa Uzi huu.
Je, maneno yanayodaiwa kusemwa tarehe 3 Aprili 2025 yanaweza kumtia hatiani hasa kwa mujibu wa Kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code. hili kutimiza vipengele vyote vya kosa la uhaini na kama ndiyo, Jamhuri imevithibitisha kwa ushahidi unaotakiwa kisheria?
LISSU anaonyesha sehemu zote za Sheria za Nchi kwamba Hakuna Sheria unayosema ni Kosa kusema maneno haliyosema. Hoja iliyobaki sasa ni Kuhusu Kifungu cha 39(2)(d), kwamba Je maneno Yale yanaingia kwenye Kifungu hicho.?
1. KIFUNGU CHA 39(2)(d) KINASEMA NINI HASA?
Kifungu cha 39 cha Penal Code kinahusu moja ya makosa mazito zaidi katika mfumo wa sheria ya Tanzania. Chini ya 39(2)(d), hoja si kwamba mtu alisema jambo ambalo serikali haikulipenda, Yaani maneno ya Kisiasa yanaweza kukuumiza wewe mpinzani wa Kisiasa lakini je Yana Nguvu ya kisheria.
Sheria inataka kitu maalumu zaidi:
Nia ya kutenda kitendo cha uhaini + Namna nia hiyo ilivyodhihirishwa + Kitendo kinachokidhi matakwa ya sheria. = "Uhaini unakuwa umethibitishwa".
Na kwa sababu hii ni kesi ya jinai, swali halipaswi kuwa:
Je, maneno ya Lissu yanaweza kutafsiriwa kama tishio?
Bali:
Je, Jamhuri imethibitisha kila kipengele kinachounda kosa linalodaiwa, kwa kiwango kinachotakiwa katika kesi ya jinai?
Kifungu cha 39(2) kinahusu mtu mwenye allegiance kwa Jamhuri ya Muungano ambaye anatengeneza nia ya kufanya matendo fulani ya uhaini na anaidhihirisha nia hiyo kwa maandishi, uchapishaji, au overt act/deed.
Katika 39(2)(d), mojawapo ya matendo yaliyotajwa ni:
Intimidation of the Executive, the Legislature or the Judiciary of the United Republic.
Na sheria inaunganisha hilo na requirement ya kuonyesha nia kupitia writing/printing au overt act/deed.
Hapa ndipo tofauti muhimu inapoanzia, kwa sababu Kuna tofauti kati ya:
A. Kusema jambo kali dhidi ya Serikali;
B. Kutaka Serikali ibadilike;
C. Kutaka uchaguzi usifanyike;
D. Kushawishi watu wasishiriki uchaguzi; na
E. Kutengeneza nia ya kuishurutisha/kuitisha Executive, Legislature au Judiciary kwa namna ambayo sheria imeifanya kuwa treason.
Mambo yote Hapo juu si vitu vinavyoweza kuchukuliwa kuwa kitu kimoja bila uchambuzi, Ushaidi, na Sheria inavyosema.
2. “STOP THE ELECTION” SI AUTOMATICALLY “INTIMIDATE THE GOVERNMENT”
Moja ya sehemu nzito sana ya kesi hii ni kama ifuatavyo.
Kwa mujibu wa taarifa za kesi, maneno yanayodaiwa ni pamoja na:
"Tutazuia Uchaguzi" | “we will stop the election”
"Tutavuruga Uchaguzi" | “we will disrupt this election”
"Tutaamasisha uasi" | “we will mobilise rebellion”
Jamhuri inayaunganisha maneno hayo na nia ya kutishia Serikali. Lakini hapa kuna chain of reasoning ambayo Mahakama inapaswa kuichunguza:
Maneno → Maana iliyokusudiwa → Nia → Kitendo kinachokusudiwa → Target → Intimidation ya taasisi iliyotajwa na 39(2)(d).
Kama kiungo kimoja hakipo, swali linakuwa kama chain nzima imethibitishwa.
Kwa mfano:
“Tutazuia uchaguzi.” | “we will stop the election”, Hilo linaweza kuwa kauli ya kisiasa, Lakini ili liingie kwenye Kifungu cha 39(2)(d) cha Pinal code, lazima ionyeshwe kwa nini kauli hiyo, katika mazingira hayo, ilikuwa manifestation ya nia ya kufanya moja ya matendo yaliyotajwa na kifungu hicho.
Hapo ndipo ushahidi wa mazingira yote ya mkutano unakuwa muhimu.
Pia Hili linaweza kuonekana kama technicality ndogo, Lakini si lazima iwe ndogo.
Katika kesi ya jinai, hati ya mashitaka inapaswa kumpa mshtakiwa taarifa inayomruhusu kuelewa:
“Ninashitakiwa kwa kufanya nini, dhidi ya nani, lini, wapi na kwa namna gani?”
Hii ndiyo logic inayohusishwa na section 132 ya Criminal Procedure Act, inayohitaji charge kutoa particulars zinazohitajika kumpa accused taarifa ya kutosha kuhusu nature ya offence.
Na kuna precedent ya Freeman Aikael Mbowe & Others v Republic, ambako Mahakama ilijadili tatizo la charge kutotaja jamii/persons waliolengwa na kauli zinazodaiwa kuwa za jinai.
3. HOJA YA “UMMA” NI NZITO KULIKO INAVYOONEKANA
Lissu amepinga matumizi ya neno “the public” katika information.
Kwa mujibu wa Pingamizi lake amedai kuwa kifungu 39(2)(d) kinarejea “any person or group of persons,” wakati charge yake inatumia “the public.”
Kwa hiyo swali la msingi ni:
“The public” ni nani hasa?
Kwa sababu kama target ni:
• wananchi wote Tanzania,
• wapiga kura,
• wanachama wa CHADEMA,
• waandikishaji wapiga kura,
• Tume ya Uchaguzi,
• Serikali,
• viongozi wa Serikali.
hizo ni categories tofauti kabisa na kila moja inaweza kubadilisha namna ya kutafsiri nia.
Ukisema alikuwa analenga kushawishi Umma (the public) kwamba ni Wananchi wote maana yake hata
• Rais,
• Polisi,
• MwanaJeshi,
• Jaji,
• Mwanasiasa,
• Fundi vitatu
• Boda Boda au
• Mtu mwengine yeyote ni mwananchi, na hapo ndipo ugumu unapotokea kwamba haiwezekani kuchukuwa watu kazaa Kuthibitisha kuwa walichochewa kufanya Jambo Fulani Wakati unaongelea Jambo la Wananchi Wote, Hili linaibuka hoja Je, watu Hao Wana Mamlaka ya Kuthibitisha Uhalali wa Wananchi wote kushawishiwa.?
Kwa Maoni yangu Watu wale wa vificho awatoshi Kuthibitisha kwamba hata Mimi, au Mtu mwengine yeyote alishawishiwa Kwa maneno ya LISSU maana Hilo Neno (the public) ni Pana Sana Ndio maana Kifungu cha 39 cha Panel code kimesema kundi la watu, au Mtu na sio Umma wote. Kwasababu Kisheria Kuthibitisha Umma wote ulishawishika na maneno Yale ni ngumu Sana, "Kama uhamuzi utakuwa Neno (the public) ni sahihi Basi Nchi Nzima iulizwe kwamba ilishawishika Kuhusu maneno ya LISSU aliyoyatoa", Mimi sikotayari kuthibitishiwa kwamba nilishawishika au la Kwa Mtu wa kificho.
4. “OVERT ACT” NDIO MOJA YA VITA KUBWA ZA KISHERIA
Hapa ndipo kesi ya Hatibu Gandhi v Republic inakuwa muhimu.
Kesi hiyo ya Court of Appeal ni moja ya authorities zinazojadili treason na umuhimu wa overt act. Rekodi ya hukumu inaonyesha kuwa kesi hiyo ilihusu mashtaka ya uhaini yaliyohusisha watu wengi na matendo maalumu yaliyodaiwa kuwa overt acts.
Hoja iliyowasilishwa na Lissu ni kwamba:
Mere words do not amount to overt act on a treason charge, isipokuwa maneno hayo yenyewe yanaelezea au kuhusiana moja kwa moja na treasonable conduct.
Hii si hoja ya kupuuzwa, kwa sababu Court of Appeal ndiyo mahakama yenye mamlaka ya kuweka tafsiri inayofunga Mahakama za chini.
Lakini pia kuna jambo la muhimu sana:
Tusifanye kosa la kusema:
“Court of Appeal imesema maneno hayawezi kabisa kuwa uhaini (Maneno matupu hayavunji mfupa).”
Hiyo ni broad kuliko tunavyoweza kuthibitisha.
Tunachopaswa kuchunguza ni:
• Ni mazingira gani Hatibu Gandhi ilizungumzia?
• Ni nani alikuwa accused?
• Ni overt acts zipi zilikuwepo?
• Ni uhusiano gani kati ya maneno na vitendo ulionekana?
Hapo ndipo precedent inakuwa na maana.
5. KESI HII INAWEZA KUWEKA PRECEDENT MPYA
Hili ni jambo ambalo Lissu mwenyewe amesisitiza.
Kesi za zamani zilizotajwa ni pamoja na:
Grey Likungu Mataka and Others
na Hatibu Gandhi and Others v Republic.
Lissu anasema kesi yake ni tofauti kwa sababu inatumia 39(2)(d) Intimidation of the Executive, Legislature or Judiciary badala ya aina za treason zilizohusika kwenye kesi za zamani.
Kwa hiyo, swali linaweza kuwa kubwa kuliko Lissu alivyosema:
Ni mpaka gani kati ya political speech na treasonous conduct katika Tanzania ya sasa?
Hili ni swali ambalo linaweza kugusa:
• viongozi wa vyama vya siasa mbali mbali,
• wabunge,
• wanaharakati,
• waandishi,
• wananchi,
• mikutano ya kisiasa,
• social media,
• livestream,
• kampeni za uchaguzi.
Ndiyo maana tafsiri ya kifungu hiki inaweza kuwa na athari kwa miaka mingi kama LISSU anaendelea kuniambia Mahakama kwamba wanabeba mzigo wa kihistoria.
Maoni yangu hata Kwa baadae Tunapaswa kuweka wazi kabisa kwenye katiba Kuhusu "Mipaka ya Demokrasia ya Kisiasa na Kejeri za Kisiasa", Maana maneno yanaweza kutolewa kama Kejeri za Kisiasa Alafu zikaonekana za kijinai na baadae Wapinzani Ndio wanaathilika zaidi na wengine wanaachwa Kwa kisingizio cha "Neno lililotokea ni Kejeri ya Kisiasa". (Upendeleo wa Upande mmoja juu ya Maswala yanayofanywa na wanasiasa wote)
6. SAKATA LA JAMBO TV "NANI ALI-PUBLISH".?
Hapa kuna hoja nyingine yenye uzito. Prosecution inasema maneno hayo yalichapishwa/published.
Lakini Lissu amepinga kwamba yeye ndiye aliyefanya publication hiyo.
Kwa mujibu wa Ushaidi wa PW17 alikuwa mfanyakazi wa Jambo TV aliyekuwa kwenye tukio na akashiriki katika kurekodi na livestreaming. Lissu anasema ushahidi wa PW17 unaonyesha kuwa wafanyakazi wa Jambo TV ndio waliorekodi na kurusha video hiyo.
Hapa kuna swali rahisi lakini la kisheria:
Nani alifanya act of publication?
Si:
“Video ilikuwa online?”
Bali:
“Jamhuri imethibitisha kwamba accused ndiye aliyefanya publication inayodaiwa na charge?”
Hiyo distinction ni kubwa.
Kwa mfano, Mtu anatoa hotuba mbele ya kamera.
1. Journalist ana-record.
2. Journalist ana-upload.
3. YouTube ina-host.
4. Watu wana-share.
5. Kisha polisi wanaona video.
Hatuwezi moja kwa moja kusema Speaker = publisher bila kuonyesha legal basis na evidence inayounganisha speaker na act of publication.
Lissu anadai hata prosecution witnesses walitoa ushahidi unaoonyesha Jambo TV ndiyo iliyofanya livestream/upload.
7. PW17 NI SHAHIDI WA KIPEKEE WA HALI YA MKUTANO
Hii ni sehemu ambayo ningependekeza tuichambue kwa umakini sana.
Kwa mujibu wa taarifa ya kesi, kati ya mashahidi 17 wa Jamhuri, Lissu amesisitiza kwamba PW17 alikuwa miongoni mwa mashahidi muhimu kwa sababu alikuwa kwenye mkutano wenyewe.
Na kwa mujibu wa Lissu, baadhi ya maafisa wa polisi waliotoa tafsiri kuhusu nia hawakuwa kwenye mkutano.
Hapo tunapata tofauti kati ya:
Direct evidence
“Nilikuwepo. Nilimsikia. Niliona kilichotokea.”
na Inference
“Nilisoma/kuona video, nikatafsiri maneno haya kuwa yanaonyesha nia fulani.”
Inference inaweza kuwa ushahidi Lakini swali la mahakama linakuwa, Inference hiyo imejengwa juu ya facts gani?
Hapa ndipo credibility, consistency na corroboration vinakuwa muhimu.
8. MASHAHIDI 17 SI SAWA NA “USHIRIKISHO WA USHAHIDI”
Hili ni jambo ambalo watu wengi hulikosea hasa Katika kesi za jinai:
17 witnesses ≠ automatically strong case.
Lissu aliwahi kurejea principle kutoka Bhatt vs Republic, kwamba si wingi wa ushahidi pekee unaotosha; lazima ushahidi uwe na substance na credibility.
Kwa hiyo tunapaswa kuuliza:
• Kwa nini ni muhimu?
• Shahidi aliona nini?
• Kutenganisha direct evidence na inference alikuwa wapi?
• Kuamua uwezo wake wa kujua alijua vipi?
Source of knowledge
• Alisema nini awali?
Consistency
• Alisema nini cross-examination?
Reliability
• Ushahidi wake unaungwa mkono na nini?
Corroboration
• Anathibitisha element gani ya 39(2)(d)?
Legal relevance
• Hapo ndipo kesi inachambuliwa kisheria zaidi.
9. “SERIKALI ILITISHWA NA KUTISHIKA?” HII NI HOJA YA AJABU KWA UZITO WAKE
Lissu amejenga hoja kwamba kama prosecution inasema nia ilikuwa intimidation of the Government, basi lazima kuwe na ushahidi unaoonyesha hiyo alleged intimidation.
Ameelekeza kwenye section 10(2) na kusema matokeo yanayodaiwa yanapaswa kuthibitishwa.
Lakini hapa ningetaka tuwe makini sana.
Kuna tofauti kati ya:
"Intent to intimidate na actual intimidation".
Hii ni distinction ya kisheria ambayo Mahakama inapaswa kuitatua.
Kwa hiyo hoja yenye nguvu zaidi si kusema:
“Rais hakutoa ushahidi, kwa hiyo kesi imekufa.”
Hiyo ni conclusion ya haraka.
Hoja sahihi zaidi ni:
Ikiwa actual intimidation ni element ya offence inayoshtakiwa, prosecution ilipaswa kuonyesha kwa ushahidi element hiyo. Kama si element, prosecution haihitaji kuthibitisha actual psychological reaction ya kiongozi fulani na Mahakama italazimika kuangalia wording ya statute na authorities.
Hapo ndipo tunakuwa wachambuzi, si mashabiki wa upande fulani.
10. KUTOKUITWA KWA RAIS SI AUTOMATICALLY ADVERSE INFERENCE
Hili nalo linahitaji usawa.
Lissu aliomba Rais Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Makamu wa Rais Philip Mpango, na aliyekuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watoe ushahidi kuhusu kama Serikali ilitishwa na kutishika. Mahakama haikuruhusu baadhi yao kuitwa.
Lakini kisheria hatupaswi kuruka moja kwa moja kusema:
“Kwa kuwa Rais hakuitwa, basi Serikali haikutishwa.”
Badala yake:
Swali ni kama mtu huyo alikuwa material witness kwa element inayopaswa kuthibitishwa.
Kama ndiyo, kisha upande uliokuwa na nafasi na wajibu wa kumleta hakumleta, Mahakama inaweza kulazimika kuchunguza principle kuhusu failure to call material witnesses, Lakini adverse inference si automatic.
Kwenye Hili Inategemea:
• umuhimu wa shahidi,
• upatikanaji wake,
• nani alikuwa na burden,
• ushahidi mwingine uliopo, na
• mazingira ya kesi.
11. HOJA YA “NO REFORMS, NO ELECTION” INATAKIWA ITENGANISHWE NA UHAINI
Hii ni sehemu ambayo mjadala wa kisiasa unaweza kutuchanganya.
Kudai:
“No Reforms, No Election” ni political position.
Swali la mahakama ni tofauti:
Je, utekelezaji wa hiyo position ulihusisha kitendo cha jinai kinachokidhi 39(2)(d)? Kwa sababu mfumo wa sheria unatakiwa kutenganisha:
"political dissent na criminal conduct".
Hiyo ndiyo sababu charge lazima iwe precise.
Kama political slogan inaweza kuwa treason bila prosecution kuonyesha additional criminal element, basi boundary kati ya political speech na criminal conduct inaweza kuwa pana sana na kama kila kauli kali ya kisiasa inaweza kutafsiriwa kuwa intimidation, basi maana ya “intimidation” yenyewe inahitaji kuwekwa wazi.
12. HAPA NDIPO ARTICLE 18 YA KATIBA INAINGIA
Katiba ya Tanzania inalinda uhuru wa maoni na mawasiliano chini ya Article 18, pamoja na haki zinazohusiana na kupata/kutoa taarifa kwa mujibu wa sheria.
Lakini Article 18 si immunity dhidi ya criminal law.
Hivyo tunapata balancing exercise:
Upande mmoja:
Freedom of expression + political speech
Upande mwingine:
Protection of constitutional order + national security + criminal law, Kisheria Mahakama inapaswa kutafuta mpaka wa kisheria kati ya hayo mawili na hapa kuna principle kubwa hasa Pale Sheria ya jinai inapotumika kwenye political speech, precision ya statutory offence inakuwa muhimu zaidi, si kidogo.
Kwa sababu punishment ya criminal conviction ni tofauti kabisa na kukosolewa kisiasa.
13. KESI HII INA “DANGER OF INTERPRETATION” AMBAYO NI KUBWA KULIKO MSHTAKIWA
Naomba Tufikiria scenarios kazaa hapa.
Scenario A
Mwanasiasa anasema:
“Serikali hii lazima iondoke, Haina Hadhi ya kuwa madarakani, Lazima tuiondoe Kwa Nguvu zote, na maneno Mengineyo kama hayo.” Je, ni treason?
Hapana, kauli hizo peke yake haziwezi kujibiwa bila kujua context na statutory elements.
Scenario B
Mwanasiasa anasema:
“Tutaondoa Serikali kwa kutumia silaha.”
Hapo kuna factual/legal circumstances tofauti kabisa.
Scenario C
Mwanasiasa anasema:
“Tutazuia uchaguzi.” Bado tunahitaji kujua:
• kwa maandamano ya amani?
• kwa boycott?
• kwa force?
• kwa intimidation?
• kwa kuzuia polling stations?
• kwa kuvamia Tume?
• kwa kutumia silaha? au ni political pressure?
Maneno yale yale yanaweza kuwa na legal significance tofauti kulingana na context na conduct.
Hii ndiyo sababu mahakama haipaswi kuchambua sentensi kama dictionary exercise pekee.
14. HOJA YA “OVERT ACT” INAWEZA KUWA KIINI CHA KESI NZIMA
Tukichora kwa mfumo:
INTENTION
↓
MANIFESTATION
↓
OVERT ACT / DEED / WRITING / PRINTING
↓
TREASONABLE CONDUCT
↓
ELEMENTS OF 39(2)(d)
↓
PROOF BEYOND REASONABLE DOUBT
Swali kubwa ni:
Ni kitendo gani halisi, tofauti na maneno yenyewe, Jamhuri inasema kilikuwa overt act ya uhaini?
Kwa sababu kama jibu ni “Alisema…”
basi Mahakama inabidi ishughulikie moja kwa moja relationship kati ya words na overt act chini ya 39(2)(d), pamoja na Hatibu Gandhi.
Lakini kama Jamhuri inasema “Alisema + akaandaa mkutano + akaandaa watu + akatoa maelekezo + watu wakaanza kutenda…” basi kesi inabadilika.
Kwa hiyo contextual conduct ni muhimu sana.
15. HOJA YA MKUTANO KUITISHWA NA NANI NI NZITO
Katika Transcript ya final submission, Lissu alisisitiza kwamba information ilidai yeye ndiye aliyeitisha mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025. Kisha akaunganisha hilo na section 49 kuhusu kitendo kinachowezesha offence na akasema hakuna hata mmoja kati ya mashahidi 17 wa prosecution aliyethibitisha nani aliitisha mkutano.
Hii ni hoja nzuri ya kuchunguza, lakini tusikimbilie conclusion.
Tunapaswa kuuliza Kama prosecution iliweka “Lissu called the meeting” kama sehemu ya overt act Je.!
• Ilibainishwa kwenye charge?
• Ilishahidiwa na nani?
• Kuna documentary evidence?
• Kuna emails/letters/messages?
• Nani ali-organise logistics?
• Nani aliwaalika attendees?
• Nani aliamua agenda?
• Nani aliamua livestream?
Na kama defence witness John Mnyika alitoa ushahidi kwamba mkutano uliitishwa na Secretariat ya CHADEMA na Lissu pamoja na John Heche walikuwa waalikwa, basi huo ni conflicting evidence ambao Mahakama inapaswa kuupima, si kuchukua upande mmoja automatically.
16. KESI HII INA SWALI MOJA KUBWA SANA:
JE, JAMHURI IMETHIBITISHA UHALIFU AU IMETHIBITISHA TAFSIRI YA KAULI?
Hii ndiyo sehemu ningependekeza iwe mhimili wa uzi huu kwa sababu prosecution inaweza kuthibitisha Lissu alisema maneno. Lakini bado kuna hatua nyingine:
Maneno hayo yana maana gani?
Halafu:
Nia yake ilikuwa nini?
Halafu:
Nia hiyo inaangukia wapi ndani ya 39(2)(d)?
Halafu:
Aliidhihirishaje nia hiyo?
Halafu:
Kuna overt act gani?
Halafu:
Je, prosecution imethibitisha kila element beyond reasonable doubt?
Hapo ndipo criminal trial inapoishia.
17. NA HAPA NDIPO “BURDEN OF PROOF” INAPOKUJA
Katika criminal case:
Accused hatakiwi kuthibitisha innocence yake, Burden kuu iko kwa prosecution kuthibitisha charge Ndiyo maana hata kama defence haiwezi kueleza vizuri kwa nini maneno hayo hayakuwa treason, hilo lenyewe halitoshi kwa conviction.
Swali ni:
Jamhuri imefanya kazi yake? Hii ndiyo principle inayofanya reasonable doubt kuwa muhimu.
Si kwamba:
“Lissu ameonekana ana hoja nzuri.”
Bali:
“Baada ya ushahidi wote, je Mahakama inaweza kwa confidence ya kisheria kusema kila element ya offence imethibitishwa beyond reasonable doubt?”
18. KWA NINI KESI HII NI MUHIMU KWA TANZANIA?
Kwa sababu Mahakama inaweza kuhitajika kuweka mipaka ya mambo yafuatayo:
Political speech
vs.
criminal incitement
vs.
intimidation
vs.
treason
vs.
overt act.
Na mipaka hiyo ikiwekwa katika judgment, inaweza kutumika kwenye kesi nyingine.
Hivyo Lissu aliposema:
“You are setting the law for the future.”
hakuwa anaongelea rhetoric tu.
Kisheria, precedent inaweza kweli kuwa na effect kwenye tafsiri za baadaye ingawa uzito wa precedent utategemea mahakama iliyotoa uamuzi na masuala yaliyokuwa mbele yake.
19. MWISHO
Hapa naomba Niseme kwamba Sisemi kwamba “Lissu ameshinda kesi.” Hatujui hilo bado, Hatujui hilo kabla ya judgment.
Badala yake tuseme:
“Kuna maswali kadhaa ya kisheria na kiushahidi ambayo judgment italazimika kuyajibu.”
Na hayo ndiyo maswali yenye uzito:
• Je, information imeweka offence kwa particulars zinazotosha?
• Je, Neno “The public” ni target halali chini ya wording ya 39(2)(d)?
• Je, maneno yaliyodaiwa ni manifestation ya treasonous intention?
• Je, mere words zinaweza kuwa overt act chini ya precedent iliyopo?
• Ni overt act gani hasa prosecution imeprove?
• Je, Lissu ndiye aliyepublish material inayodaiwa?
• PW17 anaunga mkono au anadhoofisha narrative ya prosecution?
• Je, intention to intimidate inahitaji actual intimidation/result kuthibitishwa?
• Je, failure to call particular witnesses ina legal consequence katika mazingira haya?
• Je, prosecution imeunganisha political objective ya “No Reforms, No Election” na offence mahsusi ya 39(2)(d)?
• Je, ushahidi wa police inference una uzito gani ukilinganishwa na direct evidence ya mtu aliyekuwepo kwenye mkutano?
• Je, kila element imefika kiwango cha proof beyond reasonable doubt?
Swali la uchambuzi ni hili:
Kama mtu mwingine ambaye si mwanasiasa wa upinzani angesema maneno hayo hayo, je, sheria hiyo hiyo, vifungu hivyo hivyo, precedent hizo hizo na kiwango hicho hicho cha ushahidi vingetumika?
swali la pili ni:
Kama Mahakama itaamua kwamba maneno ya kisiasa yanaweza, bila overt conduct inayojitegemea, kuunda kosa la uhaini chini ya 39(2)(d), mpaka wa kisheria kati ya uhuru wa kujieleza na uhaini utakuwa umewekwa wapi?
Hapo ndipo hii kesi inapoacha kuwa “Lissu dhidi ya Jamhuri” tu, Inakuwa kesi kuhusu maana ya uhaini katika sheria ya Tanzania, mipaka ya political speech, na kiwango ambacho Serikali lazima ifike kabla ya kumpeleka mwananchi kwenye kosa lenye adhabu kali kiasi hiki.
Nawasilisha Uchambuzi na Tathmini yangu, ni mimi mrxtz2026