Uchambuzi: Shirika la ujasusi la Uisraeli Mossad

Uchambuzi: Shirika la ujasusi la Uisraeli Mossad

Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter 10

“I WANT A MIG-21!”

Mwandishi anasema kuwa Mfalme Hasan wa pili wa Moroco alikuwa anapenda maisha ya anasa,na alikuwa anaendekeza umagharibi sana.Hii ilimfanya atengwe nan chi nyingine za Kiarabu,nay eye Mfalme kuhofia kuuwawa na Misri.Kwa Mossad ilikuwa ni fursa ya kupata mshirika katika Ulimwengu wa Kiarabu,hivo haraka sana walijipenyeza ndani ya Serikali ya Moroco ambako walitoa usaidizi wa ulinzi na mafunzo kwa kikosi maalum cha kumlinda Mfalme!
Mwaka 1965 waziri wa mambo ya ndani wa Moroco ambaye alikuwa mtu katili na jeuri sana,mtu aliyeuwawa kila mpinzani wa Mfalme,na mfalme alimwamini sana.Huyu waziri aliwasiliana na Meir Amit ambaye alikuwa mkurugenzi wa Mossad kumwomba amsaidie kumtafuta mpinzani mkuu wa Mfalme Bwana Mehdi Ben-Barka,ambaye sio kuwa mpinzani tu alikuwa adui namba moja wa Ufalme,huyu jamaa alihukumiwa kifo akiwa hayupo,na haikujulikana amejificha wapi,jitihada za Moroco kumpata ziligonga mwamba na sasa waliomba msaada wa Mossad.Mossad ambao wametapakaa duniani kote waliweza kugundua kuwa huyu bwana alikuwa amejificha nchini Uswisi,ambako walimfuatilia kwa muda mrefu na siku moja alienda Paris ambako alitekwa na kisha kupotea kabisa.Kupotea kwake kulikuja kuwa skendo kubwa hasa baada ya serikali ya ufaransa kugundua kuwa Israel ilihusika……..hali hii ilileta sintofahamu kubwa maana ilikuwa kinyume kabisa na utaratibu wa Mossad ikabidi Waziri mkuu aunde tume kuchunguza sakata hili(Wakati huo Amit alikuwa hakubaliki kabisa ndani ya Mossad)
Mkurugenzi wa Mossad alikuwa mtu mwenye akili,aliamua kufanya operesheni Diamond ambayo ilikuja kumpa heshima kubwa sana.Hii ni operesheni iliyotorosha ndege ya kivita aina ya MiG 21,ndege hii ilitengenezwa huko Urusi,ilikuwa na teknolojia kubwa sana,hata magharibi hawakuwa na ndege hii.Kwa Wazayuni ilikuwa jambo gumu lakini ilikuwa lazima walifanye.Wakati huo Urusi ilikuwa imegawa ndege hizi kwa baadhi ya nchi za kijamaa ikiwepo Iraq.Mossad walifanya upelelezi wao wakagundua kuwa wanaweza kutumia mgogoro wa Wakurdi na serikali kujipenyeza ndani ya Iraki,hivo walianza kutoa msaada wa silaha kwa wapiganaji wa Kikurdi ambao walikuwa wanapigana dhidi ya Serikali ya Bagdad!

Mossad walikuja kumgundua Pilot mmoja ambaye hakupendezwa na amri za kuwaua watoto na wanawake wa kikurdi,huyu Pilot aliitwa Redfa,na kwa miaka mingi hakupanda cheo hivo akawa amejaa uchungu mkali.Wataalam wa Mossad wakaanza kumtongoza na kumwahidi fedha nyingi sana pamoja maisha yeye na familia yake.Baada ya muda mrefu wa mazungumzo Piloti akaingia kingi na operesheni ikaandaliwa

Pilot Redfa alichukuliwa na Mossad ambako alifanyiwa mafunzo mbalimbali kwa siri,na wakakubaliana siku ambayo yeye Redfa angerusha ndege MiG 21 kama vile anaenda kwenye majukumu ya kawaida ya kijeshi,akiwa angani alipaswa kuielekeza Israel ambako angetua kwenye moja ya viwanja vya kijeshi.Kabla hajaondoka familia yake yote ilipelekwa Uingereza kisha USA na baadae wangekuja kukutana Israel ambako wangeishi maisha yao yote.Pilot alikubali na siku ikapangwa ambayo nchini Israel ni watu wanne tu walijua kuhusu hili na Redfa alichukua ndege na kuitoroshea nchini Israel……hii ilikuwa na mwaka mmoja tangu mazungumzo yaanze,na miezi kumi kabla ya vita ya siku sita kuanza..Kwa Israel ilikuwa faraja kubwa

Pilot Redfa na familia yake waliishi Israel ila dhambi ya usaliti ilimwandamana ikabidi aombe kuhamia Ulaya angalau asahau.hata huko Ulaya hali iliendelea kuwa mbaya na mwaka 1988 miaka 22 baadae alifariki kwa ugonjwa wa mstuko wa moyo.Mazishi yake yalifanywa na serikali ya Israel
 
Sawa bold Jr
Vipi hiki kitabu hakuna latest chake?
Kitabu.Mossad
Mwandishi. Michael Bar-Zohar na Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter 5
“OH, THAT? IT’S KHRUSHCHEV’S SPEECH …”

Mwaka 1956 mwandishi Victor Grayevski aliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na naibu waziri mkuu kutoka chama cha kikomunisti cha Poland.Victor alikuwa mlowezi wa Kiyahudi ambaye aliingia Poland akitokea Ujerumani,na alipofika alishauriwa abadili Ubini wake ili usiwe na mfanano wa Kiisrael hivo akajiita Grayevski kutoka Shiplman.Baada ya muda alipata kazi ya kuwa mhariri mkuu wa shirika la utangazaji la Poland(PAP)
Mwandishi anasema kuwa Victor alikuwa mdogo wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia,wazazi wake walitorekea Poland,ila baadae sana walikuja kurudi nyumbani kwao huko mashariki ya kati,Siku moja Victor alienda Jerusalem kuwasalimia wazazi wake,na kwa mara ya kwanza alikuta Dunia nyingine mpya kabisa yenye uhuru na sio ule mtindo wa propaganda za kijamaa alizozoea huko Poland na Soviet….hii ilimvutia na aliamua kuhamia nchini Israel moja kwa moja..
Mwandishi anasema siku moja Victor aliamua kwenda ofisini kwa mchumba wake ambaye ni naibu katibu mkuu na naibu waziri mkuu wa chama cha kijamaa cha Soviet ili amwage,akiwa pale ofisini aliona kabrasha kubwa limeandikwa TOP SECRET,alimwuliza huyu Naibu katibu mkuu ambaye alimjibu kuwa ni sehemu ya Hotuba ya Nikita Khrushchev ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama cha ujamaa cha Soviet.Victor alivutiwa sana na kutamani kujua nini hasa kimeandikwa hadi kiitwe Top Secret.Huyu Nikita alikuwa katibu mkuu mwenye maguvu makubwa nay a kutisha.Sasa basi kwenye mkutano mkuu wa chama cha Soviet uliokuwa umefanyika katika ikulu ya Kremli,wageni waalikwa mabibi na mabwana walitolewa nje,na wakabaki wajumbe 1400 kutoka pande zote za Soviet,hapo ndio katibu mkuu Nikita alitoa hotuba kali ambayo ilimwacha kila mtu akiwa mdomo wazi kwa mshangao mkubwa.
Nikita alihutubia kwa masaa manne,ambayo alielezea kwa nukta na kwa ufasaha mkubwa madhambi na uhalifu wote ambao ulikuwa umefanywa na Rais wa Soviet bwana Stalin(Stalin alikuwa anaabudiwa na watu kutokana na ukatili wake,inaaminika aliuwa watu wengi Zaidi nyuma ya Mao wa China).Sasa Nikita alielezea jinsi utawala wa Stalin umeua mamilion ya raia wasio na hatia,inasemekana ukumbi mzima ulilia hadi ikafikia wanajingoa nywele kichwani kwa uchungu,wajumbe wengine walizimia,na wengine walipata mshutuko wa moyo,angalau wajumbe wawili walijiua usiku huo huo kwa uchungu(Yaani wanasikia uchungu hadi unajiua)…..lakini hakuna habari yoyote kuhusu hii hotuba ilichapishwa kwenye vyombo vya habari vya Kisoviet(wakati huo serikali na chama vilishika hatamu)
Mwandishi anasema kuwa Moscow walikuwa na nguvu sana hasa kwenye taarifa ambazo wanataka umma ulishwe,ilifikia hadi CIA wakaweka dau la USD 1mil kwa mwandishi atakayesaidia kupata hotuba hii yote,lakini jitihada hizo za CIA ziligonga mwamba.Sasa Kijana mdogo Victor akiwa ofisni kwa mchumba wake ndio anagundua kuwa hii taarifa ni dhahabu,ni lulu.Ilikuja kugundulika baadae kuwa Nikita alikuwa ametuma sehemu ya hotuba yake hii kwa vyama vya kijamaa huko Magharibi.Sasa Victor alimwomba huyu mchumba wake akasome hii hotuba,na akapewa kwa masharti kuirejesha kabla ya saa kumi jioni,alipoisoma akakuta jinsi Stalin alivokatili maisha ya Warusi wenzake na mataifa mengine,kiukweli Stalin alikuwa mhalifu dhidi ya ubinadamu,alikatili maisha ya watu wengi sana wengi wakiwa Wajamaa wenzake kutoka chama cha kijamaa.Victor akapeleka hotuba hii kwenye ubalozi wa Israel nchini Poland baada ya kuona kuna taarifa muhimu kwa Taifa lake,pale ubalozini wakatoa nakala kisha Victor akawahisha hotuba ofisini kwa mchumba wake kwa muda mwafaka
Pale ubalozini walikabidhi hotuba ile kwa mossad ambao nao baadae ya kuisoma walitoa nakala wakawapa CIA.Hili liliwashangaza sana USA kuwa hotuba ambayo wamewekea dau kubwa na bado hawakufanikiwa kuipata lakini shirika dogo kama Mosad walifanikiwa kuipata.Baada ya wataalam kuichunguza kwa kina walikubaliana kuwa ndio yenyewe hivo CIA wakai leak kwa gazeti maarufu la New York times kwenye Makala yake maarufu ya Juni 5 mwaka 1956.Taarifa hii iliishtua jumuia ya kijamaa Dunia na ilileta mpasuko mkubwa sana,nan chi kama Hungary na Poland zikaanza harakati za kujiondoa kwenye ujamaa
Serikali ya Israel iliamua kumpa Victor kazi nzuri Zaidi kama shukrani kwa kusaidia Taifa lake,ambako aliajiriwa kwenye wizara ya mambo ya nje.Akiwa jijini Tel aviv alikutana na agenti wa KGB ambaye alimshawishi Victor akubali kuwa wakala wao,yeye Victor alienda Mossad akawajulisha kuhusu offer aliyopewa na Mossad walimtaka Victor akubali offer hiyo.Mossad wakamfunndisha Victor na kumpa taarifa mabazo alipaswa kuwapa KGB,kwa miaka kumi nan ne KGB walimwamini Victor na wakala wao akawa anakutana na Victor maeneo mbalimbali ya siri bila KGB kugundua kuwa walikuwa wameuziwa mbuzi kwenye gunia…….KGB walichezewa cheupe cheusi.Moscow waliamini wana mtu wao mwaminifu ndani ya serikali ya Israel na kila taarifa waliyopewa na Victor waliamini ni sahihi kumbe ilikuwa ni taarifa za kupikwa na Mossad….kitaalamu Victor alikuwa anafanya kazi ya double agent
Mwaka 1967 Moscow walimpuuza na kwa bahati mbaya ilikuwa kipindi ambacho yeye Victor aliwapa taarifa za ukweli.Ilikuwa wakati wa vita ya siku sita…wakati huo Misri waliandaa jeshi kuikabili Israel,na Israel ilitaka kuitumia Soviet ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa kwa Misri,hivo Voctor alitumwa awajulishe Moscow kuwa kama Misri ikiondoa vikosi vyake na kuvirudisha nyuma Israel pia haitaingia vitani.Lakini Moscow walipuuza wito huo na wakaitaka Misri iendelee na wao Soviet watawaunga mkono na kuwapa kila aina aina ya msaada.Matokeo ya ile vita yalidhihirisha udhoofu wa silaha za Soviet,Israel ilishinda na kujipanua Zaidi.
Mwandishi anahitimisha kuwa Victor alikuja kupewa Nishani ya heshima na Soviet inayoitwa Lenin.Hii inamfanya kuwa wakala pekee ambaye alitumika nan chi mbili bila kustukiwa,nan chi yake ilimpa nishani ya utumishi uliotukuka…..na ni moja ya watu wanaoshemika zaidi
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter 11

THOSE WHO’LL NEVER FORGET

Kuanzia mwaka 1964 Nchi nyingi za Ulaya zilitangaza msamaha kwa waliohusika na mauaji ya Wayahudi…wakati huo dunia ilitaka kurudi kwenye utulivu,bado kulikuwa na wanachama wengi wa Nazi ambao walisambaa Dunia nzima,kwa hofu na waliendelea na harakati za kujitengeneza upya.Wakati Dunia nzima ikifikiria upatanisho hii msamiati haukueleweka kwa Mossad na Wazayuni kwa ujumla,hivo wao waliendelea kutafuta Wanazi waliobaki,safari hii walikuwa wamepata taarifa za Mnazi mmoja aliyekuwa ametorokea Brazil ambako alikuwa anaishi kwa kutumia jina lake halisi! Huyu bwana anakisiwa kuua watu elfu 30 kwa mkono wake na aliitwa jina la utani Bucha,jina lake halisi ni Herberts Cukurs.
Baada ya mauaji ya Wazayuni wale waliobaki wali document kila kitu ikiwepo idadi ya waliokufa,nani alishiriki kupanga na kuua,na baada ya kuundwa kwa Taifa la Uzayuni,kazi ya kulipiza kisasi ilianza mara moja.Kila mtuhumiwa alikuwa na faili na kila Mosad walipoanza operesheni walikuwa na detail zote kuhusu kuhusika kwake.*Moja ya kipaumbele chao baada ya kuunda Taifa lao ilikuwa Mosi kutafuta waliko wengine,pili kulipiza kisasi*
Mwandishi anasema kuwa Mossad walianza operesheni ya kumtafuta huyu muaji hii kazi alipewa wakala wao mmoja ambaye kabla ya kusafiri alienda Austria ambako aliishi kwa miezi mitatu,akiwwezeshwa kufungua akaunti kadhaa na kisha akahamia Paris kisha ndio alianza rasmi kazi yake kwenda Rio De Jenaio nchini Brazil.Yule muuaji Cukurs alipofika Brazil alijifanya mwokozi wa Wazayuni na aliishi nao kwenye mtaa wao(Mchawi mpe mtoto akulele),,sasa alipolewa ndio alianza kuropoka na kueleza ukweli kuhusu namna alivofurahia kuwaua Wazayuni.Hapo ndio taarifa ilivuja na Mossad wakamtuma mmoja wa watu wake aliyeitwa jina bandia la Kunzle ambaye alipaswa kufika Brazil na kutengeneza mtandao na kukusanya taarifa za kutosha kumtia nguvuni bwana Cukurs
Bwana Cukurs alikuwa pande la mtu,katili,nyamera,na mwenye hisia kali,machale makali,kila alipohisi hatari hakusita kuondoka au kuchukua hatua,sasa baada ya kuona hatari kubwa alihama mji wa Rio de janaio na kuhamia Sao Paulo,huko aliomba ulinzi wa polisi na shirika la ujasusi la brazil,aidha aliorodhesha watu wazayuni ambao yeye binafsi alikuwa na hofu nao,akiwa sao Paulo alianzisha kampuni ya kutembeza watalii pwani.Yule Jasusi wa Kunzle alifika Sao Paulo na kwa kuwa Cukurs alikuwa na biashara halali haikuwa kazi kumpata,alifika moja kwa moja ofisini kwa Cukurs ambako alimkuta ofisini..na yeye Kunzle akajitambulisha kama mfanyabiashara na yupo katika mapumziko,na anahitaji kukodi boat..alikodishiwa na alizungushwa kwa muda kisha wakarrejea jioni.Bwana Cukurs alimkaribisha Kunzle wapate kinywaji,(wajerumani na pombe ni sawa na mgonjwa na uji).Wakiwa wanakunywa Cukurs akaanza kujisifia jinsi alivoshiriki kuwaua watu watu vitani!kunzle alikuwa makini sana kutoonyesha maumivu yoyote wala hisia kali ili Cukurs aendelee kumwagika.Pia aligundua kuwa Cukurs hakuwa na uchumi mzuri hivo kwake ilikuwa kete muhimu ya kutumia kumweka karibu na alimwambia kuwa wanapanga kuwekeza kwenye sekta ya utalii hivo kama Cukurs akiona inafaa waingie ubia.
……Usiku huo Cukurs aliongeza Kunzle kwenye idadi ya maadui zake…
Siku iliyofuatia Cukurs alimpa wazo bwana Kunzle kuwa watembee wote kwenda nje mashambani!wazo hili mwanzoni alisita ila baadae aliamua waende tu,wakiwa njiani Kunzle aligundua kuwa yeye ana Kisu tu wakati Cukurs amebeba bastola,hii ilimtisha maana ni kama alijipeleka kwenye moto,akaanza kufikiri pengine uongo wake kuwa ni mfanyabiashara haukumwingia Cukurs.Huko Shambani Cukurs alitoa bastola na bunduki kisha akalenga shabaha hili limtisha sana Kunzle hadi wanarejea mjini alikuwa amejawa na hofu sana.Baada ya kurejea Kunzle alizunguka na Cukurs mjini na kumpeleka kwenye hotel za kifahari,baada ya wiki moja Kunzle aliaga kuwa anaenda kukutana na mwenzake Uruguay na akamkaribisha Cukurs.Siku ambayo Cukurs alienda Montevideo alibeba camera yake na aliposhuka tu uwanjani akampiga Kunzle picha bila yeye Kunnzle kujua,huyu Cukurs alikuwa nyamera hasa….walikaa kwa muda mchache kisha wakaagana kuwa watawasiliana tena Yeye kunnzle akarudi Ulaya ili waje kupanga namna bora ya kuendesha operesheni!

Cukurs kwa upande wake aliporudi Sao Paulo alienda moja kwa moja kituo cha polisi na kueleza mkasa mzima wa mgeni wake pamoja na kutoa picha zake,akaelezea wasiwasi wake,yule ofisa wa polisi alimsahuri asiende tena Uruguay maana ni hatari kwake.Wiki moja baadae Cukurs alipuuza ushauri wa polisi na kuamua kwenda Montevideo ambako alipokelewa na mwenyeji wake Jasusi Kunzle.Alipokelewa wakaenda kwenye nyumba ambayo wangefikia,ndani ya ile nyumba kulikuwa na Mossad wengine 4 ambao walijipanga kumtia nguvuni,alipoingia tu ndani wakamrukia ili kudhibiti lakini walizidiwa nguvu,huyu nyamera Cukurs akamngata kidole jasusi mmoja (alibaki kilema wa kidole maisha yake yote)!Wazayuni walidharau nguvu ya mwili ya huyu mzee,katika purukushani hii ilibidi wampige risasi ya kichwa maana jamaa alikuwa anawazidi.Hivo Bwana Cukurs akawa ameuwawa,baada ya kumwua wakaweka ujumbe kichwani kwake,kisha wakatoweka “Considering the gravity of the crimes of which Herberts Cukurs was accused, notably his personal responsibility in the murder of thirty thousand men,women, and children, and considering the terrible crueltyshown by Herberts Cukurs in carrying out his crimes,we condemned the said Cukurs to death.The accused was executed on February 23,1965, by ‘those who will never forget.’”
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTER 12

THE QUEST FOR THE RED PRINCE

Mwandishi anasema kuwa Septeamba 5 mwaka 1972 timu ya Olimpiki ya Israel ilivamiwa Jijini Munich ambako kocha aliuwawa baada ya yeye kocha kujaribu kuwazuia wavamizi,ambao waliitwa Magaidi.Watu tisa walichukuliwa mateka…tukio hili lilikuwa mubashara.Dunia nzima ilishuhudia,sasa basi Serikali ya Ujerumani ilikataa pendekezo la Israel la kutaka kutuma kikosi bora kabisa cha makomandoo cha Sayeret Matkal,
Serikali ya Ujerumani iliwaahidi wale watekaji kuwa itawapeleka kokote wanapotaka almradi tu watekaji wawaachie mateka huru.Baada ya majadiliano yaliyodumu siku nzima watekaji waliafiki wazo la kupelekwa wanakotaka,wakaenda uwanja wa ndege,kumbe serikali yan ujerumani ilikuwa imewadanganya uongo wa kitoto sana…walipofika uwanjani walikuta ndege imeegeshwa ikiwa haina rubani,haina wahudumu wala chochote(hawa watekaji walikuwa smart sana,kiongozi wao alisema kabla ya kuondoka lazima aende akajiridhishe kuwa mipango iko sawa)..makubaliano yalikuwa kuwaachia mateka pale uwanjani na wao wakati huo huo kuondoka na ndege wanakotaka.
Wale watekaji walipogundua kuwa wameingizwa mjini,waliamua kuwashambulia mateka na polisi wa Kijerumani na kuuwa kadhaa hapo hapo uwanjani
Hapo ndio Mossad waligundua wana adui mpya anaitwa Black September .Kundi la kigaidi la Black september lilikuwa kikosi hatari ndani ya FATAH na kilifahamika na viongozi wachache akiwepo Yasser Arafat.Kazi kubwa ilikuwa kufanya matukio ya kushutukiza ,mwanzoni Black September walikuwa wanavamia na kulipua mali za Jordan hivo Mossad hawakujishughulisha nao,waliteka ndege ya Jordan wakaipeleka Libya,walilipua jingo la Jordan jijini Roma etc,na walikuja kumwua waziri mkuu wa zamani wa Jordani,katika korido nchini Misri,ni wazi kilikuwa kikosi hatari sana na operesheni zao zilifanikiwa sana
Mossad wakaanzisha operesheni iliyopewa jina Wrath of God. Operesheni hii ililenga kuwatafuta viongozi wa Black September na kuwaua…waliamini kuwa mgonge nyoka kichwani ndio njia rahisi…Massada ni idara ndogo ya operesheni ndani ya Mossad na ndio walipewa jukumu la operesheni hii chini ya jasusi Mike Harari.Makao makuu ya operesheni hii yalifanywa kuwa mji mkuu wa Italia,Rome na ziliundwa timu kadhaa,timu ya utambuzi na timu ya mauaji..yaani wale ambao wangewatambua Black September sio wao ambao wangehusika na kuwaua hii ni kuzuia kabisa hatari yoyote ya Israel kuhusishwa
Operesheni Wrath of God iliendelea baada ya muda sio mrefu Mossad waligundua jamaa mmoja aliitwa Hamshari,alikuwa anaishi paris na ndio alikuwa wa pili kwenye rank ya Black September,baada ya kujiridhisha kuwa huyu jamaa ni muhusika,mmoja wa Mossad alijifanya mwandishi wa habari ambaye anaguswa na swala la palestina hivo akataka kufanya mahojiano na Hamshari,walikubaliana kukutana kwenye mgahawa mmoja,jijini Paris.Huyu mwandishi alikuwa wakala wa Mossad,na wakati akiendelea na mahojiano wakala mwingine aliingia kwenye apartment ya Hamshari akatega mlipuko kwenye simu ya nyumbani kwa Hamshari,baada ya mahojiano Hamshari alifika nyumbani na kwa bahati nzuri mkewe na watoto walikuwa hawajarejea,yule mwandishi feki akapiga tena simu na alipopokea tu ule mlipuko ukalipuka na kumjeruhi vibaya sana bwana Hamshari,ambaye alikuja kufariki siku chache akiwa hospital.
Mtu mwingine muhimu aliyeuwawa na Mossad alikuwa mkuu wa Black September nchini Cyprus ambaye alihusika na maswala yote ya USSR,Block ya Mashariki nan chi nyingine kadhaa barani Ulaya.Wakati huo Cyprus ilikuwa uwanja wa mapambano kati ya Israel na Waarabu kutokana na jiografia yake.Sasa Mossad walimtegea Bwana Abd el Hir aliporejea hotelini kwake usiku,wakamvamia chumbani ambako walikuwa wametega mlipuko hatari,ambao ulimwua bwana Abd El Hir hapo hapo
Kufuatia vifo vya watu wao muhimu Black September walitambua sasa wapo vitani rasmi na Israel.Arafat wakapanga kulipiza kisasi na mara hii walipanga kuteka ndege,ambayo itajazwa milipuko mbalimbali ikalipukie Tel aviv ili iue watu wengi Zaidi.Wakati wakipanga haya Mossad walikuwa wamejaza watu wao wanaowapa taarifa ndani ya vijana wa Kipalestina waliokuwa wanaishi Ulaya.Mipango yote hii ilipangwa nje kabisa ya mashariki ya kati,kutokana na kuwa na fedha Mossad alikuwa na uhakika wa kupata taarifa yote kwa wepesi.Hii ya utekaji wa ndege ilivuja kabla
Mossad walifanikiwa kuuwa yeyote aliyehusika na tukio la Munich ambalo lilikuwa msingi wa operesheni hii,lakini ikabaki bado swala kuwa Bwana Salameh ambaye alikuwa kiongozi Munich yupo wapi?huyu ndie walimtaka kwa gharama yoyote! Bwana Salameh alikuwa Beirut akipanga mipango kadhaa mojawapo ikiwa kuteka ubalozi wa Israel nchini Thailand,mpango huu ulifeli vibaya,baadae akafanikiwa kuwateka wanadiplomasia Nchini Sudan!Balozi wa USA,na kaimu Balozi wa Ubelgiji ambao waliuwawa kikatili sana.Wauaji walikuja kuachiwa siku moja baadae na serikali ya Sudan,licha ya kelel za Dunia nzima
Kufuatia hali kuwa tete mwanamama Golda ambaye alikuwa waziri mkuu wa Israel aliagiza nguvu Zaidi iongezwe,sasa mossad wakaongeza kikosi na April 6 mwaka 1973 maofisa sita wakiwa na paspot za mataifa tofauti waliingia Beiruti! Hawa walikuwa mawakala wa Mossad waliokuja kwa kazi moja tu ya kumwua Salameh ambaye wakati huu alikuwa ameweka makazi hapa!Sasa basi ilibidi Mossad wafanye uvamizi haramu,maana kwa kadri walivochelewa ndio hali ilizidi kuwa mbaya.Walipanga kuvamia makao makuu ya PLO yaliyokuwa Beirut pamoja na makazi ya makamanda wa Black September hii ilikuwa ndio njia fupi ya kuwamaliza,uvamizi huu ulifanywa kwa usiku mmoja na wakati mmoja ambako kwenye makao makuu ya PLO walipiga mlipuko wa kilo 80 na kuiangusha kabisa nyumba yote,hili walifanikiwa kisha watoroka muda huo na chopa! Lakini Salameh alikuwa wapi?
Mwandishi anasema kuwa hawa black sepetemba walikuwa makini sana walikuwa na uwezo wa kutengeneza paspot na document feki..walikuwa wanajibadilisha sura na kuwa na mwonekano wa jinsia tofauti,mfano angeweza kuonekana kama mwanamme,akiingia ndani wakati anasubiriwa anatoka akiwa mwanamke,amevaa wigi au dera..hii mbinu iliwasumbua sana Mossad
Baadae walikuja kupata taarifa kuwa Salameh anaishi Norway wakaweka mtego,siku moja usiku akiwa njiani wakamvamia na kumwua kwa risasi kumi na nne…bahati mbaya kabla ya kutoroka polisi wa Norway wakagundua mauaji na katika msako Mossad wakagundulika!mbaya Zaidi hata yule waliyemuua wakifikiri ni Salameh alikuwa kijana wa Moroco tena aliyekuwa amefika Norway kutafuta kazi ya hotelini,ilibidi Serikali ya Israel imlipe fidia ya dola 400,000 kama kifuta machozi.Miongoni mwa wakala wa Mossad aliyekamatwa alifikishwa mahakamani katika hali ya ajabu akajikuta anampenda mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ndie alikuwa anaendesha mashtaka na baada ya kutumikia kifungo alikuja kuolewa hadi alipofariki kwa kansa 2005
Mwandishi anasema kuwa Black September ilikufa rasmi mwaka 1973,na Salameh akawa ndio mwandani wa Arafat,ndio mtu aliyeaminika Zaidi na Arafat na ilifikia mahali ikaaminika kuwa atakuwa mridhi wake.Mossad waliendelea kumfuatilia hadi 1979 ndio waliweza kumwua Salameh baada ya kutega bomu kwenye gari lake
 
Victor alikuwa mzalendo mwaminifu kwa taifa lake
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro

CHAPTER 13

THE SYRIAN VIRGINS

Mwandishi anasema kuwa mwaka 1971 Utawala wa Syria uliwanyanyasa sana Wazayuni,hali iliyopelekea wanaume wengi kukimbia makazi yao,ikiwa ni pamoja na kutelekeza familia kuokoa maisha yao.Utawala wa Syria uliendela kuwatesa hata wanawake waliobaki nchini humo! Hii ilifanya Mosad kuanzisha operesheni Smicha neno la Kihebrania lenye maana ya Blanket
Lengo la operesheni hii ilikuwa kuokoa wanawake na watoto wa kizayuni waliokuwa wametelekezwa na Waume zao nchini Syria,kisha kuwarejesha Israel,wakiwa hai! Operesheni hii iliongozwa na vijana waliokuwa recruited wengi wakiwa wamekulia Afrika Kaskazini na walizungumza kifaransa fasaha…walibatizwa Cosa nostra….kama wale mafia wa Kitaliano
Mwandishi anasema kuwa hii ndio operesheni ambayo haikumwaga damu,ilifanywa kwa weledi na kwa usiri mkubwa,usiri ulidumu kwa miaka thelathini.Operesheni ilidumu kati ya 1970 hadi 1973 na kwa miaka hii mitatu jumla yawanawake 130 waliokolowa nchini Syria na kutoroshewa Israel kwa njia ya maji bila kumwaga damu
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro

Chapter 14

“TODAY WE’LL BE AT WAR!”

Mwandishi anasema kuwa kijana mmoja mtanashati aliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na binti wa Rais Nasser wa Misri.Kijana huyu aliitwa Ashraf Marwan alikuwa kijana anayependa anasa mno,aliishi maisha yasiyokuwa yake.
Baada ya kumwoa binti wa Rais aliomba kwenda London kuendelea na masomo,akiwa London alikula fedha zote,na akajikuta anakuwa Marioo,alijiingiza kwenye uhusiano wa mapenzi na binti kutoka Kuwait ambaye alimsaidia kupata ela ndogo ndogo,uhusiano mpya ulivuja na serikali ya Misri ikamrejesha Cairo,Rais Nasser alichukia mno na kumtaka Binti yake aachane na mzinzi…binti aligoma ikabidi Bwana Ashraf Marwan atakiwe kubaki nchini Misri na angeenda London wakati kuwasilisha ripoti kwa profesa wake tu!
Mwandishi anasema kuwa wakati Fulani bwana Ashraf alirejea London kuwasilisha ripoti,akiwa London alipiga simu ubalozi wa Israel nchini Uingereza na kujitambulisha kwa majina yake na akaomba kufanya kazi na Israel,baada ya kuchunguzwa wazayuni walikubali na kumpa jina code ya Angel…Mossad walikuja kutoa jina lake halisi mwaka 2004 miaka mingi baadae,inaaminika kuw huyu bwana ndio alikuwa double agent mkali zaidi na ambaye aliweza kuwafurahisha mabwana zake vizuri yaani Israel na Misri
Bwana Ashraf Marwan alikuwa na kinyongo na Baba mkwe wake,akaamua kumwaga mboga baada ya baba mkwe kumwaga ugali.Mossad walimpa kazi na mara moja wakampa ofa ya USD 100,000(kama milioni mia mbili na thelathini tshs) hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 1970.Wakati huu Nasser alikuwa amempa kazi mkwewe katika ofisi ya Rais.Ili kuonyesha kwa mossad kuwa anaweza kupata taarifa muhimu aliwapelekea Mossad muhutasari wa kikao cha Misri na USSR walichokaa January 22,1970,jijini Moscow ambako Misri waliomba wapewe silaha za kisasa na za masafa ya kati,na ndege ambazo zingeweza kufanya shambulizi ndani ya Israel.Baada ya kuchunguza waligundua huu ni muhutasari genuine usiokuwa na chembe ya mashaka!hapa mossad walifurahi kuwa wana hazina mkono mwao
Mossad walitengeneza watu wawili (watu kati) ambao ndio wangepewa taarifa watu ambao walikuwa sleeping agents wao..Bwana Ashraf aliwapa siri za kisiasa,kijeshi na kiuchumi za taifa la Misiri,ni wazi Misiri ilikuwa tupu mbele ya Wazayuni,kila walichopanga kilifika mkononi kilivo
Ashraf Marwan aliigharimu Israel kiasi cha usd 3mill(Dola milioni tatu)
Baada ya kifo cha Nasser baba Mkwe wa Ashraf,aliridhiwa na Sadat,bwana Ashraf alichanga karata vizuri na kujikuta amefanywa msahuri maalum wa rais wa mambo ya usalama,hivo akawa anaambatana na Rais kwenye vikao muhimu vya ndani na vya kikanda,kwa Mossad ilikuwa faida kubwa maana walikuwa na mtu ndani ambaye anatoa taarifa za nchi nyingine za kiarabu,kwa kadri Bwana Ashraf alivoaminiwa na Serikali ya Misri ndivo wigo wa kupata taarifa kwa Mossad ulivoongezeka!
Ashraf akaingia tamaa akaanza kuuza siri kwa wakala wengine wa siri,yaani aliamua kuwa wakala kwa mashirika mengine kwa siri,bila shirika A kutambua….mwandishi anamwelezea kama a real double agent.Kwa mujibu wa CIA aliwatumikia kwa miaka zaidi ya 20.Mwisho kabisa Ashraf aliamua kustaafu mambo ya Espionage…baada ya kustaafu alianzsisha biashara London ikiwepo kununua sehemu ya Chelsea mwanzoni mwa miaka ya 2000,alikuwa mmoja wa Wamisiri waliokuwa na nguvu pale London akiwa pamoja na Baba yake Diana,anayemiliki store maarufu ya Harrods na timu ya mpira ya Fullam.
Kwa kuwa hakuna siri Duniani Misri walikuja kugundua baadae sana kuwa Asharaf alikuwa double agent,hivo wakamlia timing akiwa barazani kwake kwenye jumba la kifahari London wakamwua!(Adhabu ya kuifanyia ujasusi nchi yako ni kifo)
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro


Chapter 15
A HONEY TRAP FOR THE ATOM SPY
Mwandishi anasema kuwa Israel ilikuwa na mradi wa Nyukilia ulioitwa Dimona,ulikuwa mradi wa siri sana ambao ni wachache ndani ya Israel walijua nini hasa kinaendelea.Ili kupata kazi kwenye mradi huu ilibidi kupita hatua kadhaa za clearance kutoka taasisi mbalimbali za usalama nchini humo.Katika hali ambayo haijulikani nini kiliwakuta Wazayuni,wakajikuta wamemwajiri kijana mmoja aliyeitwa Morcdechai Vununu,huyu kijana walikuwa na uhusiano na waarabu kuliko Waisrael wenzake,na alikuwa na mrengo wa kulia….
Mordechai aliajiriwa bila kupita hatua ambazo wengine hupitia,hata baada ya idara ya usalama wa Taifa kupeleka ripoti yake kuhusu Mordechai hakuna hatua iliyochukuliwa.Mordechai aliajiriwa kama technician hapo kwenye mradi wa siri.
Mwandishi anasema kuwa Mordechai alikuwa kijana mpole na mtaratibu hivo hakuna mtu aliyemtilia mashaka hapo kwenye mradi…Siku moja Mordechai aliingia eneo hilo akiwa na camera,akasubiri wakati ambako hakukuwa na mtu ndani akapiga picha kadhaa maeneo mbalimbali ya mradi.Alipanga kichwani kama atahojiwa kuhusu kuingia na kamera eneo ambalo haliruhisiwi angejitetea kuwa aliisahau kwenye begi lake kwa bahati mbaya.Baada ya mwaka mmojaMradi uliishiwa bajeti wakalazimika kupunguza idadi kubwa ya wafanyakazi akiwepo Mordechai
Mordechai aliona sio haki kupunguzwa kazi,hivo alijaa uchungu sana na aliamua kuondoka kabisa Israel,akauza kila alichokuwa nacho,akasafiri kwenda India,Nepal na akiwa huku alikutana na Wabudha akaanza kutafakari kubadili dini,baadae alisafiri hadi Australia,huku alilazimika kuishi kwenye moja ya jengo la kanisa la Kikristo.Akawa anaishi hapo kanisani na baada ya muda alibadili Dini kuwa Mkristo,huwa ni jambo gumu kwa kijana wa Kiyahudi aliyelelewa kwa misingi ya dini ya Uyahudi kubadili dini hasa kuwa Mkristo…Mordechai alivunja huu mwiko akabatizwa na kuitwa John Crossman.sasa basi bwana Crossman akawa anasimulia mambo ya huko Israel hadi kuhusu yeye kufanya kazi kwenye Mradi wa Dimona ambao ulikuwa unategeneza bomu kama atomic kuua Waarabu,yeye akasema asingependa hilo litokee..kwenye hili kusanyiko kulikuwa na mwandishi mmoja wa habari,ambaye aliendelea kumdadisi Crossman,ambaye alikiri kuwa na picha.Huyu mwandishi akamshawishi Crossman atoe hizo picha wauze na watapata fedha nyingi.Mwanzoni Crossman aligoma akihofia dhambi ya Usaliti kwa Taifa lake na hofu ya kuuwawa,ila sasa alikuwa anahitaji fedha kuliko chochote
Baada ya ushawishi wa muda alikubali,walizipeleka kwenye vyombo kadhaa vya habari huko Australia,hata hivo hakuna chombo kilochoamini kama kweli hizo picha ni Genuine .Yule mwandishi alienda London kujaribu bahati yake kwenye gazeti la London Sunday Times,ni moja ya magazeti yanayoaminika kwa habari za Uchunguzi,hapa walipiga bingo hatari ,mhariri aliona ni habari ya maana ila alitaka kujiridhisha,kwenye kujiridhisha habari zikafika Mossad kuhusu hili jambo…moto ukawaka sana ila kwa Israel walishachelewa.
Mwandishi anasema mwaka 1982 hadi 1989 ilikuwa kipindi kigumu sana kwa Mossad…kila walilopanga lilifichuka,kila mti uliteleza
Kwa upande wa Mossad walianzisha Operesheni iliyopewa jina Kaniuk,kwa lengo la kumtafuta Mordechai aka Crossman na kumrejesha Israel na kujaribu kuzuia moto ambao ulikuwa umeanza kuwaka
Kwa upande mwingine London Times walijiridhisha pasina shaka kuwa zile picha ni halisi,wakamkatia tiketi bwan Mordechai kwa ajili ya mahojiano jijini London,kwenye mahojiano Mordechai alielezea kwa kina mradi wa Dimona ambao kuna bomu ambalo lilikuwa linatengenezwa na lilikuwa na uwezo wa kuuwa viumbe hai na kuacha majengo yakiwa intact.London times walimlipa USD 100,00 kwa picha na mahojiano,pamoja na 40% ya mauzo ya gazeti na 25% ya mauzo ya kitabu ambacho kingechapishwa mapema.Na alijulishwa kuwa mmliki wa London Times Bwana Rupert Murdoch alikuwa mmiliki wa kampuni ya Twentieth CenturyFox iliyojishughulisha na kutengeneza filamu,na angepewa sehemu ya haki(Huko magharibi anagalau wanaheshimu wazo la mtu)
Sasa fedha inambadilisha mtu haraka sana,watu wa London times walimshauri awe makini na asitembee pekee yake mtaani,ila sasa jamaa Mordechai alikuwa na ngawira zinamuwasha,akatamani ale raha,na apate kimwana wa kumliwaza na kumtoa baridi,hasa ikizingatiwa ilikuwa msimu wa baridi London,Mordechai alikutana na dada mzuri kwenye moja ya Café hapo london,yule dada lijitambulisha kwa jina la Cindy kutoka New York na alikuwa London kwa mapumziko mafupi,kisha angeenda Rome na baadae kurejea New York,kwa kuwa Mordechai alikuwa na tamaa ghafla akaingia kwenye mapenzi na huyu binti,ingawa machale yalimcheza kuwa sio ila tamaa ikazidi(Tamaa mbele mauti nyuma),kwa siku kadhaa walibusu,na kutembea mtaani wakiwa wameshikana mikono,kama wapenzi,huyu binti alimfanyia kila kitu isipokuwa hakukubali kulala naye,kwa maelezo kuwa ni mapema mno,ila wakienda Rome atakubali maana hapo Rome Cindy atakuwa huru.Huyu Cindy ambaye alikuja kujulikana kuwa ni wakala wa Mossad alimfanyia Udelila bwan Mordechai hadi akakubali kusafiri kwenda Roma,na ni Cindy ndio alilipa tiketi tena alikata business class….Maskini Mordechai hakugundua kuwa alikuwa ameanguka kwa Delila “honey trap” mfumo maarufu wa mawakala wa siri kutumia wanawake/wanaume kufikia malengo yao
Israel haikuwa tayari kufanya operesheni ndani ya UK hasa ikizingatiwa walikuwa nan a uhusiano unaozorota,kufuatia Israel kutumia pasipoti za UK kufanya Ujasusi nchini Ujerumani,Israel ilikiri na kuahidi kutorudia tena,uhusiano wa Mossad na Idara ya Usalama ya Italia ulikuwa mzuri mno,hivo waliamua kwenda Roma
Septemba 30 mwaka 1986 Cindy na Mordechai walitua Roma na shirika la ndege la British airways 504 saa tisa alasiri,walishuka kama wapenzi,na walipokelewa na ndugu wa Cindy(alikuwa wakala mwingine wa Mossad),walipelekwa kwenye apartment,walipoingia tu ndani mlango ulifungwa kwa nyuma na wanaume wawili walimrukia na kumpiga kabali,na alichomwa sindano ambayo alisinzia…ilikuwa ndani ya dakika moja matendo haya yote…. Siku hiyo hiyo alipakiwa kwenye basi dogo na kupelekwa kwenye fukwe ambako boti ya mwendokasi ilikuwa inasubiri na kumrejesha Israel,nchini Israel alihojiwa na kupandishwa kizimbani ambako alikutwa na hatia ya kufanya Ujasusi na usaliti wan chi yake,alihukumiwa miaka 18 gerezani
Kwa watu wengi Mordechai hakuwa jasusi bali raia ambaye hakukubaliana na uongo wa Israel hasa kwenye maswala ya idadi ya silaha hatari ambazo walizimiliki,huku duniani walisema wana mabomu kati ya 10 hadi 20,ilikuja kugundulika baada ya Mordechai kujitoa muhanga kuwa Israel ilikuwa na mabomu hatari kati ya 100 hadi 200(yaani walipunguza sifuri moja)kiwango ambacho hawakuruhusiwa kuwa nacho wakati huo
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro

Chapter 16

SADDAM’S SUPERGUN

Mwandishi anasema kuwa kuna kijana mmoja wa Canada alitwa Bull,ambaye alipata PhD akiwa na miaka 23,alikuwa mtu mwenye akili nyingi mno,ilimfanya kuwa kijana mdogo Zaidi kupata PhD kwenye vyuo vikuu vya Canada
Huyu kijana Bull alikuwa mtaalam wa silaha,na alikuwa na ndoto ya kutengeneza bunduki kubwa Zaidi Duniani.Alipambana kuhakikisha kuwa ndoto yake inafikiwa na aliweza kutengeneza bunduki kwa msaada kutoka serikali ya Canada pamoja na USA,bunduki hii ilikuwa na uwezo wa kwenda mita 36.Hata hivo kutokana na sababu mbalimbali Serikali ya USA iliacha kufadhili mradi huu,hali hii ilimfanya Bull kukosa fedha na kuamua kuendelea kutengeneza bunduki na kuziuza kwa yeyote atakaye,wakati huo huko USA kwenye baadhi ya majimbo bunduki ilikuwa inauzwa kawaida,kama bidhaa
Mwandishi anasema huyu Bull kichwa chake kilikuwa mbele sekunde kadhaa,alikuja kugundua bunduki ingine kali iliitwa GC-45 ilikuwa na uwezo wa range 45km,akawa anauza kwa makaburu Afrika ya Kusini,Angola na maeneo mengine hata yale yaliyokuwa yamewekewa vikwazo na umoja wa Mataifa.Inaaminika kuwa CIA walimuunga mkono kwa siri.Bull alivuka mpaka na kukutana na Sadam Hussein,enzi za vita kati ya Iraq na Iran,Bull alimwahidi Saddam kumtengenezea bunduki bora kabisa pamoja na silaha nyingine.Saddam alikubaliana nae na Bull akaazisha mradi alioita “Project Babylon.”
Bull alipambana hasa maana ni kazi aliyoipenda alikuwa anafanya kwa passion,ndani ya kipindi kifupi akawa na miradi mikubwa miwili ya Al-Majnoon Al-Fao.Miradi ya kuzalisha Bunduki na silaha nyingine,makombora ya masafa ya marefu na masafa ya kati,silaha hizi zingeweza kuipiga Israel kutokea jangwani Iraq
Maendeleo haya ya silaha za kivita na za kisasa za Iraq,yalianza kuwaogopesha majirani hasa Iran,CIA,Mossad na M16 kila mmoja kwa wakati wake alimwonya Bull kuacha hii biashara ila jamaa hakusikia
Mwaka 1990 mtu asiyejulikana alimvamia Bull nyumbani kwake Ubeligiji akiwa na bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti,ambako alimpiga Bull risasi tano akafa hapo hapo,na huu ukawa ndio mwisho wa mradi wa Babylon ambao ungekuwa hatari kwa Taifa la Israel
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro

Chapter 17

FIASCO IN AMMAN

Mwandishi anasema kuwa Mossad walifanya operesheni iliyowaendea vibaya sana katika historia yao. Operesheni hii ililenga kumwua kabisa Bwana Khaled Mashal kiiongozi wa Hamas aliyekuwa anaishi Amman.Kipindi hicho Hamas ndio kundi hatari Zaidi kwa Israel kuliko PLO,Hamas walikuwa wamefanya shambulizi kwenye soko moja Jijini Jerusalem na kuua watu 16 na wengine Zaidi ya 170 kujeruhiwa vibaya.Waziri mkuu Benjamini Netanyau aliagiza Mossad wafanya operesheni ya kimya kimya kuuwa viongozi wa Hamas,na mlengwa mkuu alikuwa Bwana Khaled
Sasa basi Mossad wakajipanga na kupeleka kikosi kazi nchini Jordan ambako walianza kumfuatilia Khaled mienendo yake,wapi anaenda na anakutana na nani,waliingia nchini humowakiwa na pasi za bandia,kama watalii
Kwenye operesheni hii walikubaliana kumwua kwa kutumia sumu ya kibaolojia ambayo isingeacha alama.Hii ni sumu maalumu iliyotengenezwa kwenye maabara yao,na ambayo walimwua nayo yule kiongozi wa PLO(rejea sehemu ya 14).Mossad walifanya maandilizi ya kutosha na kuamua kuwa Khaled angepuliziwa sumu shingoni siku ya Septemba 26 mwaka 1997 akiwa tu ameshuka kwenye gari wakati akipanda ngazi kuingia ofisini kwake.Mara nyingi kutoka nyumbani hadi ofisini Khaled hakuwa na mlinzi alienda pekee yake,palikuwa na umbali mfupi.Mossad hawakupaswa kuwasiliana kwa kifaa chochote cha electronic,simu au chochote kati ya timu iliyokuwa nyumbani kwa Khaled na ile iliyopo kwenye jingo la ofisi yake,ambako alipaswa kumwagiwa sumu,ilikubaliwa kuwa kiongozi wa operesheni atatoa ishara ya kuvua kofia yake kama operesheni isiendelee,pamoja na alama/ishara nyingine za mwili.Siku ya tukio jambo la ajabu lilitokea,Khaled alitoka na watoto wake wawili ili awapeleke shule maana waliachwa na school bus,wale maofisa wa Mossad waliokuwa nyumbani kwa Khaled hawakuweza kuona watoto maana gari ni ya tinted,hivo wakatoa taarifa kuwa jamaa ameondoka,wale walioko kwenye jingo la ofisi wakawa wapo standby kwa kazi moja tu,sasa Khaled aliposhuka kwenye gari lake,ghafla mtoto akashuka akawa anamkimbilia baba yake huku akiita Baba,baba,dereva nae akashuka ghafla kumkimbilia mtoto,wale Mossad wawili waliokuwa na sumu wakawa tayari wameshamfikia Khaled,kiongozi wa operesheni akawa anajaribu kuvua kofia ili kuahirisha operesheni maana walikubaliana kama ikitokea mtu mwingine,mtoto,askari au yoyote akafika eneo la tukio basi operesheni isimame,ili kuzuia madhara ya sumu kupata mtu asiyehusika wala kuwa mlengwa
Kiongozi wa operesheni alikuwa amechelewa maana wale Hit team walishampa mgongo.Wakati Hit team wakiwa tayari kumwagia sumu dereva alifika akiwa anamkimbiza mtoto,ghafla akaona tukio la bosi wake kushambuliwa nae akaanza kupambana kumwokoa bosi,kwenye hii purukushani,wote dereva na Khaled waliwamgiwa ile sumu,Hit team wakaanza kutoka nje ya jengo kwa kasi ya ajabu lakini ikatokea balaa lingine la jamaa mmoja ambaye alikuwa mwanajeshi mstaafu ambaye alianza kuwakimbiza Hit team,hata hivo hakuweza kuwafikia,waliingia kwenye gari lao wakatokomea mtaani…Hit team walihisi pengine namba za gari zimeshikwa,hivo walitelekeza gari kwenye maegesho fulani barabarani,na wao kuanza kutembea barabarani….katika hali ya kawaida kumbe yule mwanajeshi mstaafu alikuwa bado anawafuatilia kwa mguu,na aliweza kuwagundua kwa mavazi yao,hit team walipomwona walipiga yule mwanajeshi ambaye alipiga kelele na ghafla wananchi wakafika,hit team wakajitetea kuwa wao ni watalii na huyo jamaa anataka kuwapora mali zao,sasa raia wakaita polisi ambao wote watatu walichukuliwa hadi kituo cha polisi,pale kituoni wale Hit team wa Mossad walitoa paspoti zao za Canada,polisi walipiga simu Ubalozini maana hadi muda huo waliamini kuwa wale ni watalii,ila ubalozini walijibiwa kuwa hawana taarifa ya raia wa Canada hapo Jordan.
Wale polisi hawakujua kuwa wana lulu mkononi….waliendelea kuwashikilia hawa Hit team Barry na Shawn,na wakawaruhusu kufanya mawasiliano na ndugu zao,hapo moja kwa moja waliwasiliana na wenzao Ulaya kuwajulisha kuwa wametiwa nguvuni(Wakati wa operesheni za mossad,commanding center huwekwa mabara mengine,hasa Amerika au Ulaya).Iliamriwa wale Mossad wengine waende kwenye ubalozi wa Israel haraka sana
Kwa upande mwingine sumu ilianza kula mwili wa Khaled,ambaye alikimbizwa kwenye hospital ya Mfalme.Ilibidi waziri mkuu wa Israel aagize kila kitu kisimame,akaagiza ujumbe mzito uende Jordan kumwona mfalme na kumweleza ukweli wote,ili kuokoa maisha ya wale Hit team,na ujumbe ulielekezwe wampe ofay a kuokoa maisha ya Khaled,hivo ilibidi Israel iingie kwenye mkakati wa kuokoa maisha ya adui yao ambaye muda mchache walipanga kuondoa uhai wake,pale hosptalini madaktari wa Jordan waligoma,kupokea dawa ya kuondoa sumu kutoka Israel hadi wapewe kwanza formula,ambayo Israel hawakutaka kuitoa,hali ya mgonjwa ilizidi kuwa mbaya na ikabidi Mfalme Hussein awapigie simu USA na kuwajulisha kila kitu,USA waliweka presha kwa Israel wakubali kutoa fomula maana hawakuwa na njia,baada ya vuta nikuvute walikubali kutoa fomula na baada ya dawa,Khaled alipata nafuu,na hatimae alipona kabisa!
Ilibidi Israel iwaachie wafungwa 20 wa kipalestina na wengine 20 wa Jordan ili waachiliwe wale hit team wawili waliokuwa wameshikiliwa polisi
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro

Chapter 18
FROM NORTH KOREA WITH LOVE
Mwandishi anasema kuwa July 2007 katika hotel ya Kensington iliyopo London,Mossad waliingia kwenye chumba alichokuwa amefikia ofisa mmoja wa ngazi za juu wa Syria.<ossad waliingia kinyemela kwenye chumba cha hotel,na kwa bahati nzuri yule ofisa alikuwa ameacha laptop yake hapo chumbani,waliwasha kisha wakaweka program maalum ndani ya ile laptop ikiwepo Trojan horse,program hii ilikuwa inakopi mafaili yote na kuyahamisha kwenda makao makuu ya Mossad,kila alichofanya yule bwana Mossad walikipata mubashara
Pale makao makuu ya Mossad Tel Aviv walishangazwa na taarifa walizopata kutoka kwenye laptop ya huyu ofisa,walipata mafaili,picha,michoro ya mradi wa Nyukilia wa Syria uliokuwa unafanywa kwa siri huko Jangwani.Mradi huu ulifanywa kati ya Syria na Korea ya kaskazini
Huu ulikuwa udhihirisho wa taarifa ambazo Mossad walikuwa wamezipata kuwa Syria walikuwa wanajenga kinu cha Nyukilia katika Jangwa la Dir Al zur,huu ulikuwa mradi wa siri sana,ambao ni watu wachache sana waliokuwa wanaufahamu na ni wachache Zaidi waliokuwa wanafahamu eneo la mradi.Kimsingi ndani ya Serikali ya Syria ni watu watatu tu walifahamu uwepo wa mradi huu.Huu mradi ulitekelezwa na wataalam wa Korea Kaskazini chini ya ufadhili wa Iran,nah ii ikawa ngumu Zaidi kwa mtu kutambua
Mwandishi anasema kuwa Syria walikuwa wajanja sana,walifanya usiri wa hali ya juu,iliwachukua Mossad na CIA muda mrefu sana kuja kugundua uwepo wa mradi huu.Wafanyakazi wote kwenye huu mradi hawakuruhusiwa kuwa na simu za mikononi,na eneo lote halikuwa na signal kabisa.Mawasiliano kutoka eneo la mradi kwenda kwingine yalifanywa manualy,(Mkono kwa mkono)pia eneo la mradi lilikuwa na jengo kuu kuu ambalo lilikuwa limetelekezwa..hivo hata rada na satellite hazikuweza kuona chochote cha maana licha ya kupita juu
Israel na USA walishikwa na butwaa yam waka kuwa kuna nchi inaweza kurutubisha Nyukilia bila wao kujua.Kwa Syria kuwa na Nyukilia ilikuwa hatari sana kwa Israel.sasa wakawa wana swali kuwa kama mradi umeanza bila wao kujua je utakuwa kwenye hatua ipi?kwa ushahidi waliokuwa wamekusanya angalau walijua uwepo wa mradi ila hawakujua umeendelea kwa kiwango gani.
Mossad waliwapa kazi kitengo cha Unit 8200 ambacho ni kitengo mahusisi cha vijana wadogo wenye utaalamu mkubwa wa IT,hawa walielekezwa kuingilia mawasiliano ya viongozi wa Syria,Korea na Iran ili kupata taarifa za mawasiliano yao kwa kina.Baada ya kujiridhisha mno Israel iliwasiliana na USA na kwenye kikao kilichofanyika Washington Israel ilitaka shambulio la kijeshi lifanyike,ili kuharibu kabisa mradi wote,kwa upande wa Marekan waligoma enzi hizo Rais wa USA alikuwa Bush ilikuwa mwaka 2007,jitihada za Israel kutaka kuungwa mkono ziligonga mwamba,shambulizi la kijeshi lingekuwa na madhara makubwa katika diplomasia ya kimataifa.Walikubaliana uchunguzi Zaidi ufanyike
Mossad waliwekeza Zaidi ili kupata ushahidi Zaidi ulipatikana ikiwa ni pamoja na sampuli za udongo/mchanga/majimaji ambayo yaliwezesha kugundua kiwango cha uranium,pamoja picha za wahusika hasa Wakorea,picha zilipigwa kwa kutumia Satelite.Lakini pia Israel ilitumia kikosi chake cha Sayeret Matkal kikosi cha weledi wa hali ya juu,ambao walitumia helicopter mbili ambazo hazikusomeka kwenye rada ya Syria,(Anga la Syria ni miongoni mwa anga ambazo zina ulinzi wa hali ya juu sana)chopa ziliruka usiku na bila rada kuziona,walifika kabisa kwenye eneo la kinu na kwa ustadi mkubwa commando alishuka kuchukua sampuli ya udongo,kisha kurejea Israel kwa kasi ya ajabu,ilikuja kugundulika kuwa udongo ule una kiwango kikubwa sana cha Uraniam
Licha ya ushahidi huu bado USA ilikataa shambulio la kijeshi kama Israel ilivoshinikiza,Rais Bush na Waziri Mkuu Olmert wa Israel walibadilishana maneno makali,na mwisho Olmet alijibu kuwa atafanya lolote kulinda nchi yake…… “George,I’m asking you to bomb the compound,” Olmert said. “I cannot justify an attack on a sovereign nation,” Bush replied, ,” Olmert bluntly said. “I’ll do what I believe necessary to protect Israel.” “
This guy has balls,” Bush later said. “That’s why I like him.”
September 5, ndege tano za kivita aiana ya F-15 ziliruka kutoka uwanja wa ndege wa David kuelekea Mediteranian,ndege tatu kati ya zile tano (zote zilikuwa zimejaa makomandoo wenye weledi wa hali ya juu)Zilielekezwa kuelekea mpaka wa Uturuki na Syria na mbili zilielekezwa kurejea kwenye ule uwanja zilikoruka.Zile tatu zikiwa njiani ndio walielekezwa kuwa wako kwenye operesheni maalum na wakelekezwa pale kwenye ule mradi na kutakiwa kuangusha hapo bomu la kilo mia tano(Nusu tani)nbomu liliangushwa kwenye shabaha na kukisambaratisha kabisa kile kinu na mradi wote wa Dir Al Zur,na kwa kuwa mrdi ulikuwa jangwani hakukuwa na madhara ya kiraia
Baada ya shambulizi hilo Waziri mkuu wa Israel alimtumia ujumbe mfupi Rais wa Syria kuwa Israel haina lengo la kuingia kwenye vita na Syria,ila pia haiko tayari kuona Syria ikirutubisha na kumiliki Nyukilia,akamtaka Rais anyamaze kimya.Baada ya kupata huu ujumbe Serikali ya Syria ilitoa taarifa kwa umma kuwa Chopa za kijeshi za Israel zilijaribu kuingia kwenye anga yao,lakini vikosi imara vya Syria vilipambana na Wazayuni wamekimbia kama mbwa koko……
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro


Chapter 15
A HONEY TRAP FOR THE ATOM SPY
Mwandishi anasema kuwa Israel ilikuwa na mradi wa Nyukilia ulioitwa Dimona,ulikuwa mradi wa siri sana ambao ni wachache ndani ya Israel walijua nini hasa kinaendelea.Ili kupata kazi kwenye mradi huu ilibidi kupita hatua kadhaa za clearance kutoka taasisi mbalimbali za usalama nchini humo.Katika hali ambayo haijulikani nini kiliwakuta Wazayuni,wakajikuta wamemwajiri kijana mmoja aliyeitwa Morcdechai Vununu,huyu kijana walikuwa na uhusiano na waarabu kuliko Waisrael wenzake,na alikuwa na mrengo wa kulia….
Mordechai aliajiriwa bila kupita hatua ambazo wengine hupitia,hata baada ya idara ya usalama wa Taifa kupeleka ripoti yake kuhusu Mordechai hakuna hatua iliyochukuliwa.Mordechai aliajiriwa kama technician hapo kwenye mradi wa siri.
Mwandishi anasema kuwa Mordechai alikuwa kijana mpole na mtaratibu hivo hakuna mtu aliyemtilia mashaka hapo kwenye mradi…Siku moja Mordechai aliingia eneo hilo akiwa na camera,akasubiri wakati ambako hakukuwa na mtu ndani akapiga picha kadhaa maeneo mbalimbali ya mradi.Alipanga kichwani kama atahojiwa kuhusu kuingia na kamera eneo ambalo haliruhisiwi angejitetea kuwa aliisahau kwenye begi lake kwa bahati mbaya.Baada ya mwaka mmojaMradi uliishiwa bajeti wakalazimika kupunguza idadi kubwa ya wafanyakazi akiwepo Mordechai
Mordechai aliona sio haki kupunguzwa kazi,hivo alijaa uchungu sana na aliamua kuondoka kabisa Israel,akauza kila alichokuwa nacho,akasafiri kwenda India,Nepal na akiwa huku alikutana na Wabudha akaanza kutafakari kubadili dini,baadae alisafiri hadi Australia,huku alilazimika kuishi kwenye moja ya jengo la kanisa la Kikristo.Akawa anaishi hapo kanisani na baada ya muda alibadili Dini kuwa Mkristo,huwa ni jambo gumu kwa kijana wa Kiyahudi aliyelelewa kwa misingi ya dini ya Uyahudi kubadili dini hasa kuwa Mkristo…Mordechai alivunja huu mwiko akabatizwa na kuitwa John Crossman.sasa basi bwana Crossman akawa anasimulia mambo ya huko Israel hadi kuhusu yeye kufanya kazi kwenye Mradi wa Dimona ambao ulikuwa unategeneza bomu kama atomic kuua Waarabu,yeye akasema asingependa hilo litokee..kwenye hili kusanyiko kulikuwa na mwandishi mmoja wa habari,ambaye aliendelea kumdadisi Crossman,ambaye alikiri kuwa na picha.Huyu mwandishi akamshawishi Crossman atoe hizo picha wauze na watapata fedha nyingi.Mwanzoni Crossman aligoma akihofia dhambi ya Usaliti kwa Taifa lake na hofu ya kuuwawa,ila sasa alikuwa anahitaji fedha kuliko chochote
Baada ya ushawishi wa muda alikubali,walizipeleka kwenye vyombo kadhaa vya habari huko Australia,hata hivo hakuna chombo kilochoamini kama kweli hizo picha ni Genuine .Yule mwandishi alienda London kujaribu bahati yake kwenye gazeti la London Sunday Times,ni moja ya magazeti yanayoaminika kwa habari za Uchunguzi,hapa walipiga bingo hatari ,mhariri aliona ni habari ya maana ila alitaka kujiridhisha,kwenye kujiridhisha habari zikafika Mossad kuhusu hili jambo…moto ukawaka sana ila kwa Israel walishachelewa.
Mwandishi anasema mwaka 1982 hadi 1989 ilikuwa kipindi kigumu sana kwa Mossad…kila walilopanga lilifichuka,kila mti uliteleza
Kwa upande wa Mossad walianzisha Operesheni iliyopewa jina Kaniuk,kwa lengo la kumtafuta Mordechai aka Crossman na kumrejesha Israel na kujaribu kuzuia moto ambao ulikuwa umeanza kuwaka
Kwa upande mwingine London Times walijiridhisha pasina shaka kuwa zile picha ni halisi,wakamkatia tiketi bwan Mordechai kwa ajili ya mahojiano jijini London,kwenye mahojiano Mordechai alielezea kwa kina mradi wa Dimona ambao kuna bomu ambalo lilikuwa linatengenezwa na lilikuwa na uwezo wa kuuwa viumbe hai na kuacha majengo yakiwa intact.London times walimlipa USD 100,00 kwa picha na mahojiano,pamoja na 40% ya mauzo ya gazeti na 25% ya mauzo ya kitabu ambacho kingechapishwa mapema.Na alijulishwa kuwa mmliki wa London Times Bwana Rupert Murdoch alikuwa mmiliki wa kampuni ya Twentieth CenturyFox iliyojishughulisha na kutengeneza filamu,na angepewa sehemu ya haki(Huko magharibi anagalau wanaheshimu wazo la mtu)
Sasa fedha inambadilisha mtu haraka sana,watu wa London times walimshauri awe makini na asitembee pekee yake mtaani,ila sasa jamaa Mordechai alikuwa na ngawira zinamuwasha,akatamani ale raha,na apate kimwana wa kumliwaza na kumtoa baridi,hasa ikizingatiwa ilikuwa msimu wa baridi London,Mordechai alikutana na dada mzuri kwenye moja ya Café hapo london,yule dada lijitambulisha kwa jina la Cindy kutoka New York na alikuwa London kwa mapumziko mafupi,kisha angeenda Rome na baadae kurejea New York,kwa kuwa Mordechai alikuwa na tamaa ghafla akaingia kwenye mapenzi na huyu binti,ingawa machale yalimcheza kuwa sio ila tamaa ikazidi(Tamaa mbele mauti nyuma),kwa siku kadhaa walibusu,na kutembea mtaani wakiwa wameshikana mikono,kama wapenzi,huyu binti alimfanyia kila kitu isipokuwa hakukubali kulala naye,kwa maelezo kuwa ni mapema mno,ila wakienda Rome atakubali maana hapo Rome Cindy atakuwa huru.Huyu Cindy ambaye alikuja kujulikana kuwa ni wakala wa Mossad alimfanyia Udelila bwan Mordechai hadi akakubali kusafiri kwenda Roma,na ni Cindy ndio alilipa tiketi tena alikata business class….Maskini Mordechai hakugundua kuwa alikuwa ameanguka kwa Delila “honey trap” mfumo maarufu wa mawakala wa siri kutumia wanawake/wanaume kufikia malengo yao
Israel haikuwa tayari kufanya operesheni ndani ya UK hasa ikizingatiwa walikuwa nan a uhusiano unaozorota,kufuatia Israel kutumia pasipoti za UK kufanya Ujasusi nchini Ujerumani,Israel ilikiri na kuahidi kutorudia tena,uhusiano wa Mossad na Idara ya Usalama ya Italia ulikuwa mzuri mno,hivo waliamua kwenda Roma
Septemba 30 mwaka 1986 Cindy na Mordechai walitua Roma na shirika la ndege la British airways 504 saa tisa alasiri,walishuka kama wapenzi,na walipokelewa na ndugu wa Cindy(alikuwa wakala mwingine wa Mossad),walipelekwa kwenye apartment,walipoingia tu ndani mlango ulifungwa kwa nyuma na wanaume wawili walimrukia na kumpiga kabali,na alichomwa sindano ambayo alisinzia…ilikuwa ndani ya dakika moja matendo haya yote…. Siku hiyo hiyo alipakiwa kwenye basi dogo na kupelekwa kwenye fukwe ambako boti ya mwendokasi ilikuwa inasubiri na kumrejesha Israel,nchini Israel alihojiwa na kupandishwa kizimbani ambako alikutwa na hatia ya kufanya Ujasusi na usaliti wan chi yake,alihukumiwa miaka 18 gerezani
Kwa watu wengi Mordechai hakuwa jasusi bali raia ambaye hakukubaliana na uongo wa Israel hasa kwenye maswala ya idadi ya silaha hatari ambazo walizimiliki,huku duniani walisema wana mabomu kati ya 10 hadi 20,ilikuja kugundulika baada ya Mordechai kujitoa muhanga kuwa Israel ilikuwa na mabomu hatari kati ya 100 hadi 200(yaani walipunguza sifuri moja)kiwango ambacho hawakuruhusiwa kuwa nacho wakati huo
Nimecheka sana hapa walipopunguza 0
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter 19

LOVE AND DEATH IN THE AFTERNOON

Mwandishi anaanza kwa kumtaja Bwana Imad Mughniyeh,huyu alikuwa guidi hatari sana aliyezaliwa huko Lebanon,vyombo vingi wa usalama vilifahamu jina lake na matendo yake mabaya,ila vilishindwa japo kupata picha yake…alikuwa kama mzimu
FBI waliweka dau la USD 5mil kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake,huko USA alituhumiwa kushiriki yafuatayo,mwaka 1983 alilipua ubalozi wa USA Beirut,watu 63 walikufa hapo hapo,mwaka huo huo alilipua meli ya kivita ya USA huko Beirut watu 58 walikufa,alimteka na kisha kumwua ofisa wa CIA ,aliteka ndege ya Kuwait na kuwaua abiria,aliteka na kuchinja askari wa USA 20 huko Saudi Arabia….kwa Upande wa Israel huyu bwana Imad alituhumiwa kushiriki kulipua Makao makuu ya IDF,alilipua ubalozi wa Israel huko Argentina na watu 50 wakauwawa,alilipua Jewish community center huko Buenos Aires na wazayuni 80 wakauwawa,alishiriki vitendo vingi vya ukatili na mauaji dhidi ya binadamu
Bwana Imad aliacha shule,akajiunga na wapiganaji wengine wa Kipalestina,waliokuwa wameweka kambi kwenye nchi mbalimbali za Kiarabu,na walikuwa wanapata msaada kutoka Iran.Pamoja na ukweli kuwa hakusoma lakini alikuwa na akili kubwa,kwa muda mrefu hakutoa kauli tata,wala hakufanya interview au kwenye redio au kwenye TV yoyote.Mipango yote aliifanya bila kuacha alama,na akiwa makini sana,
Tabia za Imad Mugyniyeh zilikuwa kama za rafiki yake mkubwa Bwana Osama Bin Laden…mara kadhaa alibadili mwonekano wake.Ni yeye aliifanya Hezebollah kutoka kuwa genge hadi kuwa Jeshi imara na lenye weledi wa kutosha /kupambana idara za usalama za mataifa makubwa
Mossad walianza rasmi operesheni ya kumtafuta Imad,mara moja walijaribu kulipua jingo ambalo waliambiwa yupo lakini walijikuta wanamuua mtu mwingine asiyehusika.Ilibidi Mossad watafute wapalestina ambao walikuwa kinyume cha Hezbollah kama wakala wao wa kusaidia kupata angalau pa kuanzia,hatua hii iliwasaidia kutambua kuwa kuna kipindi Imad alienda Ulaya na akarudi akiwa amebadilishwa sura..huyu Imad alikuwa anabadili mwonekano ikiwa ni pamoja na kufanya upasuaji wa uso..>>>Mossad walitumia Intelijensia hii kutafuta Kliniki huko Ulaya ambako huyu jamaa atakuwa amefanyia upasuaji.Jitihada za Mossad zilianza kuzaa matunda,waliweza kupata Klinik ya Siri iliyokuwa chini ya idara ya usalama ya Ujerumani Mashariki,iliitwa STASI,hawa jamaa walikuwa na idara ya kiniki kwa ajili ya kufanya upasuaji na huyu Imad alikuwa amefanyiwa upasuaji mara 30,ikiwepo kubadili uso,kubadili magego,mdomo,meno ,macho.kwa kutumia Rupia walipewa picha mbalimbali za Imad
Mwaka 2008 Mossad walipata taarifa za kuwa bwana Imad angekuwa Damascuss kwenye moja ya matukio muhimu ya jeshi la Syria,hawakujua angewasili kutoka,wapi na akiwa na gari gani,na akiwa na nani,kupata taarifa zake lilikuwa jambo gumu mno,ila iliamriwa kuwa bomu litegwe kwenye gari lake,na lingelipuliwa kwa kutumia simu…yaani bomu linategwa na litafyetuliwa na simu ya mkononi,mara tu aingiapo garini.Mossad walilazimika kurusha jiwe gizani
Wakiwa kwenye maandalizi walipata taarifa kuwa Imad angekutana na Nihad Haidar,huyu alikuwa mkewe wa pembeni,lakini kwa siri sana,kwa miaka Zaidi ya 20 hakuna idara ya usalama iliyotambua uhusiano huu,sasa basi Mosad wakaweka mtego hapa,maana ilikuwa rahisi kumtoa uhai wake..hawakutaka kupoteza muda wala nafasi,alipofika tu kwenye eneo ambalo alipanga kukutana na mpenzi wake,basi Mossad wakalipua bomu la kutega ambalo walilitega hapo,na lilifanya Imad kupoteza maisha hapo hapo!
Na ukawa mwisho wa Komandoo huyu ambaye kichwa chake kilikuwa na dhamani ya usd 5mil
 
Back
Top Bottom