Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Group la Yanga limekaa vizuri sana yeyote anaenda robo! Yaani timu zote 4 zina nafasi ya kwenda robo! Hata kama Al Ahly atagawana point na CR Belouizdad bado nafasi ipo!Mjinga ni yule anaeamini kuwa Yanga hatokwenda robo fainali.
SIO KWA SIMBATyr wydad Casablanca wameamka[emoji23]
Kwenye hiyo picha...Nafasi ya Simba kwenda Robo Fainali imeanza kuwa ngumu
“Nafasi ya Simba kwenda robo fainali imeanza kuwa ngumu zaidi. Simba wameambulia pointi mbili katika mechi zao mbili za mwanzo. Na sasa wana safari ya kukabiliana na Wydad pale Morocco. Mechi mbili zijazo watacheza na hawa jamaa wa Afrika Kaskazini wakianzia na pambano la ugenini ambalo litakuwa la machozi jasho na damu kwa wenyeji.
"Wydad wamepoteza mechi mbili. Moja nyumbani dhidi ya Jwaneng nyingine wamepoteza dhidi ya ASEC Mimosas. Pambano hili dhidi ya Simba watalitumia kwa kujaribu kuwafuta machozi mashabiki wao. Hawatataka kufungwa mechi ya pili mfululizo nyumbani, au mechi ya tatu mfululizo katika kundi. Simba wana kazi.
"Kama Simba wataweza kufanya vema katika mechi mbili zijazo dhidi ya Wydad, huku ASEC na Jwaneng wakipunguzana wenyewe kwa wenyewe inaweza kuwasaidia. Tatizo ni kwa Simba ipi? Hii ya Onana? Benchikha ana kazi kubwa ya kufanya. Tusubiri tuone.” Mchambuzi Edo Kumwembe.
Hatma ya Yanga bado, Yanga watashinda mechi ijayo.
Ndio huyu huyu ....kolo walipewa connection na etooKwenye hiyo picha...
Hapo Ahmed ally alikuwa anasema alikuwa ananyang'anyana na wazingi Onana gani? Huyu mwenye vidreads na machepele mengi yasiokuwa na msaada wowote kwa timu??
Kama Onana mwenyewe ndio huyu anayechezea Simba, basi hao wazungu hawana akili hata kidogo.
Visababu vya kichawiHiyo title nikajua ndani umeshusha sababu za kiufundi mujarabu kwa nini simba imeumaliza mwendo. Kumbe umeishia kutoa sababu za kihisia na kishabiki kama ilivo kawaida yako