Monica Mgeni
Member
- Oct 7, 2021
- 82
- 134
Tanzania ni nchi kongwe katika Ukanda wa Afrika na Afrika Mashariki, Tanzania ina mchango mkubwa katika ustawi na usalama wa nchi za Afrika Mashariki na Kenya ikiwepo.
Urafiki wa Tanzania na Kenya ni wa muda mrefu na urafiki huo umechanganyika kwa udugu wa damu kutokana na kuoleana jambo ambalo limeongeza ukaribu wa nchi mbili hizi.
Mtu yoyote mwenye mtazamo wa kuona Tanzania inaweza kuingilia mambo yenye maslahi na Wakenya na kutaka kuyavuruga ni mtu asiyejua chochote kwenye historia za nchi hizi. Kwani Tanzania ndiyo iliingilia kati na kuituliza Kenya kwenye vurugu za uchaguzi wa mwaka 2007. Ikumbukwe kuwa vurugu za mwaka 2007-2008 baada ya kutangazwa Mwai Kibaki kuwa mshindi wa urais, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alipambana kusuluhisha mgogoro huo bila mafanikio lakini ni Tanzania tena kupitia Rais Jakaya Kikwete ndiyo ilimaliza mgogoro huo na majirani zetu wakaanza kuishi kwa amani na utulivu.
Uhusiano wa Kenya na Tanzania hauwezi kutiwa dosari kwa taarifa za wanaopenda machafuko na vibaraka wao, hili ukitaka kuliona vizuri ni utatuzi wa changamoto mbalimbali za kibiashara zilizotatuliwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN ambaye tunaamini kama watanzania ataendeleza ushirikiano na uhusiano wa kindugu uliyopo kati ya Tanzania na Kenya.
Hongera Rais mteule WILLIAM RUTTO, hongera Rais SAMIA SULUHU HASSAN kwa pongezi zako kwa Rais mteule wa Kenya na utayari wako wa kuendeleza gurudumu la upendo na mshikamano kati ya serikali yako na serikali ya Kenya.
Mungu ibariki Kenya🇰🇪 na Tanzania
Mungu ibariki Jumuiya ya Afrika Mashariki.