Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

swali kwa magufuli, atafumuaje mfumo wa chama asichokifahamu? (kumbuka hajawahi kushika wadhifa wowote ndani ya CCM)
 
N her wafukuzwe wote ambao c waadilifu kazn kwani kuna watanzania wengi tu ambao hawn kaz
 
Kiongozi wetu tunategema yote mazuri kutoka kwako, hongera sana kwa mikakati yako.
 
AHADI ZAKE NI MARUDIO YA KUANZIA 1985 - 2010.MATATIZO YAPO PALEPALE
“Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,amlofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
...anasema eti atapunguza kodi (PAYE) kwenye mishahara ya wafanyakazi.pombe anatuona wajinga ni aje? waziri muandamizi katika serikali ya sasa inayokata kodi kubwa katika mishahara yetu atuambie kwanza ameshawahi japo kuandika andiko kuishauri serikali ya Jakaya kuhusu kupunguza kodi katika mishahara zetu?

hizi ahadi za ujanja-ujanja na hadaa hawa maccm wataacha lini?

Msiwape kura.
 
...anasema eti atapunguza kodi (PAYE) kwenye mishahara ya wafanyakazi.pombe anatuona wajinga ni aje? waziri muandamizi katika serikali ya sasa inayokata kodi kubwa katika mishahara yetu atuambie kwanza ameshawahi japo kuandika andiko kuishauri serikali ya Jakaya kuhusu kupunguza kodi katika mishahara zetu?

hizi ahadi za ujanja-ujanja na hadaa hawa maccm wataacha lini?

Msiwape kura.

Hapo tatizo liko wapi, amesema atapunguza na hilo ana uwezo nalo. Ana uwezo huo
#HapaKaziTu
 
Tanzania ya magufuli itakuwa ya
1.uadilifu
2.uchapakazi
3.uwajibikaji
4.maendeleo
5.haki sawa
6.ukuaji wa uchumi

Mgombea huyo mwenye kauli mbiu hapa kazi tu.magufuli amekuwa mtu wa kazi katika wizara alizo kaa hivyo kumfanya awe na sifa za kuiongoza tanzania 2015-2020 ....

Viva magufuli
 
Posted today 08:33

Hii si asubuhi kweupe peee sasa hiyo ndoto unayoota saa hizi haina tafsiri pole sana!
 
tanzania ya magufuli itakuwa ya
1.uadilifu
2.uchapakazi
3.uwajibikaji
4.maendeleo
5.haki sawa
6.ukuaji wa uchumi

mgombea huyo mwenye kauli mbiu hapa kazi tu.magufuli amekuwa mtu wa kazi katika wizara alizo kaa hivyo kumfanya awe na sifa za kuiongoza tanzania 2015-2020 ....

Viva magufuli

tanzania ni ya watanzania.lowassa chaguo la wengi
 
Tanzania ni ya Watanzania siyo ya mtu mmoja ni bora aseme Tanzania nitakayoongoza nataka iwe hivi....
 
Ukirudi tena hapa utueleze zile bil.zaidi ya 200 zilizo potea wizara ya ujenzi ziko wapi,rejea ripoti za CAG/PAC
 
Back
Top Bottom