Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Ha ha ha! Chezea hapa kazi tu, Tumeshamuelewa sana Magufuli, kura atapata za kutosha mpaka kupitiliza kuliko wanavyofikiri, huo ndo ukweli acheni kujitoa fahamu, EL ndo nani.... Ha ha ha ha! acha nicheke mie, yaani kiulaini kabisa ikulu njia nyeupe kwa JPM.

Hujitambui mbumbu na ndio maana unafata mkumbo,nchi hii jamani,toka kikwete anaingia madarakani,umeme shida,hospital majanga,rushwa ndo usiseme hadi hivi magufuli anaende kuongea yaleyale aliyoyasema kikwete lkn bado majitu yanadanganyika yaani mazoba hayataisha Tanzania hii.
 
Hizi ni kejeli na hadaha kweli Magufuli anaongea kwa dhati kabisa na kwa kumuogopa Mungu kuhusu hv viwanda kuanzishwa kwa mikoa ya Manyara, Arusha,Dodoma na mingine aliyoahidi?

Kweli mwanasiasa ni wakumuogopa maana ni uongo wa mchana kweupe. Watanzania wasasa tutaja laumiwa na vizazi vijavyo maana bado hatujielewi na hatujafunguka.

Nakukumbusha kumchagua Magufuli ni kuichagua CCM ile ile na machozi yatakua yaleyale.Tusubiri tutajuta mara 100 maana sisi ni wasahalifu kama Nyumba.

# Kumchagua Magufuli ni kuichagua CCm
 
Mambo yote anayoyaongea ni anawahadaa wananchi, mathalan kulalamika juu ya ukosefu wa umeme Kwani haelewi mambo ya serikali yake? Asituhadae, kusema ni wakati wa mabadiliko nk nk hii ni mbinu ya kuwachanganya wananchi mawazo na wasielewe ubovu wa ccm.
kwani kuna kitu gani hawajui lowassa na sumaye kuhusu tatizo la umeme nchini? tena hao ndo waanzilishi wa matatizo ya umeme nchini. au leo kwa sababu wako upinzani mnajifanya hamnazo?
 
so waliopita kwa miaka yote ya utawala wa ccm walikuwa na madeni?...au ?
 
CCM nasikitika kusema ukweli kuwa ni usanii tu, anvoshangaa madawa hospt.,mikopo ya wanafunzi vyuoni,umeme,maisha bora kwa kila mtz.,barabara zake zenye mashimo kabla ya mwaka nk. Binafsi nawashangaa watz. wadanganyika kirahisi.Hatutoboi kwa hali hii. Tutaendelea kulialia tu hadi mwisho,sema nawaonea huruma watoto na wajukuu zetu. Ee Mwenyenzi Mungu tusaidie.
 
Sisi watanzania tusalimiane sisi watanzania...

M leo sina mengi ila kuna jambo linaleta ukakasi kichwani kwangu lazima tuliangalie kwa jicho kubwa zaidi...

Mära nyingi wapiga kampeni wa CCM wamekua wakisifia kwamba wanaweza kuongea hadi dakika arobaini kwenye mkutano!

Sasa swali ni je hivi kuna mtanzania ambaye bado anahitaji kusikia maneno mengi yasiyo na utekelezaji ambayo tumekua tukiayasikia kwa takirbani miaka 54 sasa?
 
Wapo wake zao wengi tu hata humu.ila mwaka huu watasaliti ndoa zao.
 
CCM ni ile ile Oooo ni ile ileee,,, nakapenda kawimbo hako,,,,
 
ahadi za maghufuli ni ulaghai mtupu hazina jipya. maghufuli anaongea sana lakini anaongea mambo yaleyale..
 
Ukimsikiliza Magufuli akijinadi kwenye majukwaa anaeleza atakachofanya pindi atakapopewa ridhaa na wananchi.

Lakini napata ukakasi na ahadi zake, kwani imsonekana kutotekelezeka na hasa suala la mahakama ya mafisadi kwani nimemeona akiwapigia debe baadhi ya mafisadi wa Escrow akiwaambia wananchi kwamba watu hao ni safii na wametutengenezea katiba safi.

Ikifikia hapo napata wasiwasi na utekelezwaji wa ahadi za Magufuli.
 
1. Serikali itakuwa ya Magufuri ndivyo anavyodai. Tangu lini serikali kwa katiba yetu akapewa mtu? Kwamba anakusudia kuvunja katiba?
2. Anaonyesha dalili zote za udikteta. Yaani umimi ni mwingi, watu wa umimi mwingi uhodhi shughuli badala ya kuwa team work huwa one man show. Mawazo yake hupenda yawe ya wengine na huupenda umashuhuri na kuabudiwa. Hivyo mwisho hugeuka kuwa madikteta wa kutupa, ref. Idd Amin the great.
3. Kila mkutano anatia ahadi mpya kama tatu. Kama mikutano yake itafikia 250 hivyo atakuwa na ahadi 1,000 mbali ya zilizomo ktk ilani ya ccm.
4. Amekiacha chama kama chama. Hakitaji na sababu kinanuka. Je idhini ya kututawala atakabidhiwa ccm au Magufuri?
5. Ana jiona yeye ni msafi wakati yeye sio msafi mfano suala la nyumba za serikali, ubora wa Barabara na maamuzi ya nepotism kwake. Kupeleka taa za kuongozea magari kitongojini mjini Chato its nepotism at its best.
5. Nk, nk nk
 
KUNA kulia na kusaga meno, Kiongozi huwa anaonekana kwa asili mfano, Nelson mandela/Ghandi/
 
Anatakiwa kuzuia ufisadi siyo kuunda mahakama ambayo itazidi kula kodi zetu.Mahakama zipo,majaji wapo
 
Back
Top Bottom