makoko jumanne
JF-Expert Member
- Apr 20, 2015
- 584
- 164
Mgombea urais kupitia ccm john pombe Magufuli ameapa kula sahani moja na wale wote watakaokuwa wanadhulumu wanyonge kwa kuwa Serikali yake iko kwa ajili ya kuwanyanyua wanyonge wote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Christopher Gamaina
AHADI za kuanza kuwalipa wazee wote pensheni na kulinda maslahi ya watu wenye ulemavu wakiwamo wenye ualbino zilizotolewa na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, zimepokewa kwa furaha na makundi hayo ya jamii.
Dk. Magufuli anayesisitiza kuwa anaomba urais si kwa majaribio bali kwa sababu amedhamiria kwa dhati ya moyo kuutumikia umma wa Watanzania bila ubaguzi wowote, alitoa ahadi hizo wakati akihutubia mkutano wa kampeni jijini Mwanza, wiki iliyopita.
Tutaanza kuwalipa wazee pensheni, wazee wamefanya kazi kubwa katika nchi hii, lakini pia tutalinda maslahi ya watu walemavu wakiwamo albino ili wasiuawe katika nchi hii, aliahidi mgombea huyo wa urais huku akisisitiza kuwa kwake ni kazi tu.
Hata hivyo, Dk. Magufuli hakufafanua kiwango cha pensheni kitakacholipwa na Serikali yake (kama atachaguliwa kuwa rais) kwa wazee wala aina ya maslahi yatakayozingatiwa kwa watu wenye ulemavu nchini.
Wakizungumza na Raia Mwema kwa nyakati tofauti wiki hii, viongozi wa mashirika ya wazee na watu wenye ulemavu mkoani Mwanza walimpongeza Dk. Magufuli kutokana na ahadi hizo wakisema utekelezaji wake utawapunguzia changamoto za uchumi na usalama.
Mratibu wa masuala ya wazee katika Shirika la Maperece linalotetea haki za wazee wilayani Magu mkoani hapa, Julius Mwengela, anasema ahadi ya kuanza kuwalipa wazee wote pensheni imeibua matumaini mapya kwa kundi hilo la jamii nchini.
Ahadi hiyo ni nzuri, ila ninachoomba iwe ya kweli, isiwe ya kuwahadaa wazee na mwisho wa siku kuwakatisha tamaa. Naomba waziri wa wizara husika atakayeteuliwa na Dk. Magufuli kama atashinda, aitekeleze kwa vitendo, alisema Mwengela ambaye pia ni Mhasibu wa Shirika la Maperece.
Mwenyekiti wa wafuatiliaji wa wazee wagonjwa majumbani katika Wilaya ya Magu, Hermenegild Mganga, alimpongeza mgombea huyo wa urais akisema huo ni mwanzo mzuri kwa Serikali kuwathamini wazee na kushughulikia changamoto zinazowanyima haki zao katika jamii.
Hiyo ahadi ni nzuri kama itatekelezwa kwa vitendo, ninampongeza Magufuli kwani hiyo ni sehemu ya kufanyia kazi changamoto zinazowakabili wazee tulizopeleka katika kila chama cha siasa kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu, anasema Mganga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kata ya Magu Mjini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (Shivyawata) Mkoa wa Mwanza, Alfred Kapole, anaitazama ahadi ya kulinda maslahi ya kundi hilo la jamii kama majibu ya kilio chao cha muda mrefu.
Nimepokea vizuri ahadi ya kulinda maslahi ya watu wenye ulemavu iliyotolewa na mgombea urais, Dk. Magufuli, hiyo ni sehemu ya majibu ya kilio chetu cha kila siku cha kudai haki za walemavu, anasema Kapole ambaye ni mlemavu mwenye ualbino.
Mwenyekiti huyo wa Shivyawata Mkoa wa Mwanza ameahidi kushirikiana na wenzake kuandika barua ya kumpongeza Dk. Magufuli na wananchama wa CCM waliomchagua kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyanganyiro cha urais.
Katika kuonyesha kuwa tumefurahishwa na ahadi ya kulinda maslahi ya walemavu, tutamwandikia Dk. Magufuli barua ya kumpongeza na kuwaonyesha Watanzania kwamba hawakukosea kumchagua kugombea urais, anasisitiza Kapole.
Lakini kwa upande mwingine, Kapole alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Serikali itakayopundwa na Dk. Magufuli (kama atachaguliwa) kuangalia uwezekano wa kuvipatia ruzuku ya fedha vyama na mashirika ya watu wenye ulemavu na majengo ya kuendeshea shughuli zao.
Awanadi wagombea ubunge Ilemela, Nyamagana
Katika hatua nyingine, Dk. Magufuli aliwaomba wakazi wa Jimbo la Ilemela kumchagua Angelina Mabula (CCM) kuwa mbunge wao na wakazi wa Jimbo la Nyamagana kumchagua Stanslaus Mabula (CCM) ili washirikiane naye kuchochea maendeleo ya majimbo hayo.
Nichagulieni Angelina Mabula kuwa mbunge wa Ilemela na Stanslaus Mabula kuwa mbunge wa Nyamagana, ukipenda kufuli lazima upende na funguo zake, ukipenda mtumbwi lazima upende na kasia zake, alisema Dk. Magufuli na kuendelea:
Angelina Mabula, namfahamu sana, alikuwa DC (Mkuu wa Wilaya) Muleba, baadaye Butiama alikozaliwa Mwalimu Julius Nyerere, kisha akahamishiwa Iringa, lakini kwa mapenzi makubwa ya Ilemela, ameacha hiyo kazi nzuri ili aokoe Jimbo la Ilemela kimaendeleo, ninaomba ndugu zangu wa Ilemela mmlete Angelina.
Kuna watu wanasema hawawezi kuongozwa na mwanamke, naomba kama kuna mtu hapa hakuzaliwa na mama anyoonshe mkono (hakuna aliyenyoosha), na kwa bahati nzuri nimeweka makamu wangu ni mwanamke, kwa hiyo tusiwadharau wanawake wanapotaka kutuongoza, na mimi ninajua Angelina anatosha.
Dk. Magufuli waliwadokeza wananchi kuwa kabla ya kuanza kuhutubia mkutano huo, Angelina alimwomba akichaguliwa alikumbuke jimbo la Ilemela kwa kuidhinisha fedha za kugharimia ujenzi wa barabara ya Sabasaba Buswelu kwa kiwango cha lami.
Katika kujibu ombi hilo, Dk. Magufuli alisema jambo hilo linawezekana kwa kuwa tayari mwaka huu Sh bilioni zaidi ya 800 zimeshatengwa kwa ajili ya Mfuko wa Barabara.
Pia mgombea urais huyo aliahidi kuidhinisha fedha za kugharimia ujenzi wa daraja la kisasa kutoka Kigongo hadi Busisi ndani ya Ziwa Victoria akifafanua ahadi hiyo ataitekeleza ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Nataka Mwanza iwe ya kwanza kujengewa daraja refu na mipango hiyo itaanza mwakani, alisisitiza Dk. Magufuli na kuongeza kuwa daraja la juu la waenda kwa miguu (flyover) kama lililojengwa eneo la Mabatini litaanza kujengwa eneo la Furahisha jijini Mwanza wakati wowote kwa kuwa bajeti yake imeshatengwa.
Mwanza tusifanye makosa kwa kuchagua watu ambao wakienda bungeni wakati wa bajeti za maji, barabara, afya, elimu na nyinginezo wanatoka nje huku wakiwa wameshachukua posho zao, alisema Dk. Magufuli na kuongeza:
Wakitoka nje waliobaki wanagawana bajeti hizo, wakirudi wanakuta zimeisha, wao wakiingia bungeni ni kutoka, chagueni watu ambao wanabaki bungeni mpaka mwisho, changueni wabunge ambao wanawabana mawazi mpaka mahitaji ya wapigakura wao yanapatikana.
Aidha, Dk. Magufuli alimsifu Stanslaus Mabula akisema alipokuwa Meya wa Jiji la Mwanza alimwomba fedha za kugharimia ujenzi wa barabara za lami na za mawe maeneo ya milimani, na kivuko cha MV Temesa kinachofanya safari ziwani kati ya Nyegezi na Mwanza Mjini. Leo tena nimekaa hapa amenichomekea barabara nyingi, alisema.
Alipopewa nafasi ya kuzungumza mkutanoni, Angelina Mabula alimwambia Dk. Magufuli Naomba nikuhakikishie kwamba sitakuangusha, nikuhakikishie maendeleo yatakwenda kwa kasi kama jinsi wewe usivyotaka mzaha katika kazi, maana kwako ni kazi tu.
Kwa upande wake, Stanslaus Mabula alisema Nawaombea madiwani kura na mimi mwenyewe, Dk. Magufuli tusaidie kupata maji, kupima viwanja kwa gharama nafuu, kuboresha mazingira ya biashara. Nawaomba Watanzania mmpe kura Magufuli, tumeanza na Mungu, tumemaliza na Mungu, ee Mwenyezi Mungu inshalah tusaidie tuvuke salama.
Pamoja na mambo mengine, Dk. Magufuli alisema atakuwa rais wa viwanda na rafiki wa wafanyabiashara wadogo, wa kati, wakubwa. Tunataka wafanyabiashara wakubwa wawekeze katika viwanda, tutakuwa na umeme wa uhakika kuviendesha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, alisisitiza.
Nataka pia Uwanja wa ndege wa Mwanza uwe wa kimataifa ili watu kutoka mataifa mbalimbali watue hapa kwa ajili ya biashara, wafanyabiashara wa hapa watainuka, nataka uchumi wa Mwanza uinuke, alisema na kuongeza:
Vile vile, nataka tuwe na viwando vya samaki, nyama, maziwa na nguo ili kuinua uchumi, kwani sasa hata wakulima wamekata tamaa ya kulima pamba, tutaboresha bei ya pamba, tutakuwa na ufugaji wa samaki.
Tutanunua meli mbili kubwa za kutoka Mwanza kwenda Bukoba na Musoma. Naomba mniamini, nitumeni nikafanye kazi, kwangu mimi ni kazi tu. Nitakuwa rais wa vyama vyote kwa sababu maendeleo hayana vyama, mimi kwangu ni kazi tu.
Nataka Watanzania twende mbele, tuna dhahabu, tuna tanzanite, tuna kila kitu. Nataka tufanye kazi, nataka nchi iendele mbele, nataka Watanzania waishi kwa raha, nataka Watanzania waishi kwa amani.
Wanyarawanda, Warundi walichezea amani, Somalia, Sudan Kusini, Kenya, Libya pia walichezea amani machafuko yakatokea watu wakafa. Leo Libya haikaliki. Nenda Syria, walishindwa kulinda amani yao.
Amani ni muhimu sana. Siku moja ya uchaguzi isije kutupelekea pabaya. Ningependa kuwa rais wa Tanzania yenye amani, ili nitekeleze ahadi zangu. Tutangulize Mungu atuepushie balaa ya kutokuwa na amani, tuitunze amani yetu.
Wanyarwanda wanakimbilia huku (Tanzania), Warundi wanakimbilia huku, sisi (Watanzania) tutakimbilia wapi? Tanzania ndiyo imekuwa kimbilio la watu wote, Tanzania ndiyo imekuwa kisiwa cha amani.
Oktoba 25, tukapike kura kwa amani, kamwe tusichonganishwe na wanasiasa, mabadiliko yanakuja na mabadiliko ya kweli yataletwa na Magufuli. Ninawaomba wana Mwanza, ninawaomba Watanzania wote tutunze amani yetu kama mboni ya jicho.
Ninaomba ndugu zangu hili suala la amani tusilifanyie mzaha ili litupeleke pazuri. Kila sehemu nilipokwenda wanasema rais ni Magufuli, wengine ni wasindikizaji kama wasindikiza harusi, alisema Dk. Magufuli katika mkutano huo uliovunja rekodi ya kuhudhuriwa na watu wengi zaidi jijini Mwanza
Raia Mwema
Mwaka huu mtaweweseka hadi ubongo. ...lowasa ndiye rais ajae wa JMT huyo magufuuri aende kuanzisha pushupu klabu
Hata sasa hivi elimu ya msingi ni bure, lakini ni afadhali isingekuwa bure maana michango iliyopo inazidi bure.