Ratiba ya magufuli katika kuijenga nchi mpya tanzania anaanza kama ifuatavyo: -
1. Kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi mafisadi wote bila kujali nafasi walizowahi kutumikia serikalini
2. Kufufua viwanda vyote vilivyokufa na mashirika ya umma yaliyobinafisishwa na hayafanyi kazi vyema, kuyaunda upya na kupiga kazi.
4. Wakulima kupewa matrekta kwa vikundi vitakavyosajiliwa. Pia kupewa pembejeo za kilimo na kutafutiwa na kupata uhakika wa masoko yao - hakuna kukopwa mtu.
5. Wafanyakazi kuongezewa mishahara.
6. Kuboreshwa kwa shule zote za zamani na mpya kupewa madawati, vitendea kazi, nyumba za walimu na kujengewa miundombinu bora.
7. Hospital zetu kuboreshwa na kuhakikisha madawa yanapatikana, vitanda vya kutosha kwa wagonjwa na wahudumu wa afya kuwa na maslahi bora.
8. Askari kuboreshewa miundombinu yao ya kazi, mishahara na nyumba.
9. Kuboresha maslahi ya wavuvi na wafugaji ikiwemo dhana bora za kutendea kazi.
10. Kuboresha maisha ya wachimba madini wadogowadogo kwa kuwapa mitaji na masoko.
11. Na menineyo mengi kuboreshwa.