Sami Omary Khamis
Member
- Sep 8, 2020
- 67
- 133
Baada ya mafanikio makubwa ya awamu ya kwanza ya miaka mitano ya Serikali ya CCM katika kupambana na umaskini na kuwawezesha wananchi ikiwemo kusaidia vikundi vya wajasiriamali kimafunzo, kisera na kimikopo, wafanyabiashara wadogo na kuwawezesha vijana pamoja na mpango wa kuwezesha kaya maskini kupitia TASAF, bado Serikali ya awamu ya 5 imepanga kuongeza nguvu zaidi kwa miaka mitano ijayo ili kupunguza umaskini na uwezeshaji wa wananchi.
Sura ya pili ya Ilani ya CCM ya 2020-25, kipengele cha 34 kilichopo ukurasa wa 23 hadi 25 imeeleza hatua zaidi zitakazochukuliwa na Serikali itakayoundwa na CCM kuhakikisha wananchi wanaendelea kuwekewa mazingira mazuri ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kutoa msukumo katika kuhamasisha na kusimamia uanzishwaji na usajili wa vikundi vyenye mwelekeo wa ushirika na makampuni pamoja na kuwawezesha kupata mitaji kupitia mikopo yenye masharti nafuu.
(b) Kufuatilia kwa karibu utoaji wa elimu ya ujasiriamali unaofanywa na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa inakidhi viwango.
(c) Kuwezesha vijana, wanawake na makundi mengine ya wajasiriamali kujiajiri kwa kuwapatia mafunzo na stadi za ujasiriamali na usimamizi wa shughuli za kiuchumi.
(d) Kuimarisha mifuko na programu zinazolenga kuwezesha kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine.
(e) Kuwa na programu maalum za kuwezesha vijana waliomaliza taasisi za elimu ya juu na kati kujiajiri na kuajirika.
(f) Kuanzisha utaratibu wa kuwakopesha vifaa na mitaji kwa masharti nafuu wanafunzi wanaomaliza mafunzo ya ufundi.
Zaidi kwenye Sura hiyohiyo ya pili, Serikali ya CCM kwa miaka mitano ijayo itaendelea zaidi na mkazo kwenye mambo yafuatayo ili kupambana na umaskini na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi:-
i. Kubuni na kutekeleza mikakati ya kuhakikisha kuwa elimu ya ujasiriamali inayotolewa na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi na Asasi za kiraia ina ubora unaokidhi.
ii. Kushirikiana na wadau kuanzisha vituo vya vya uendelezaji wajasiriamali (enterprise development centres) kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwawezesha wananchi kupata ithibati za kimataifa ili kupanua wigo wa fursa za ajira na biashara.
iii. Kuimarisha viwanda vilivyopo na kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vipya vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, samaki na rasilimali nyingine za maji kwa kutumia taasisi za umma, sekta binafsi na vikundi.
iv. Kuboresha kasi ya utekelezaji Awamu ya Tatu ya TASAF ili kuwafikia wananchi maskini katika vijiji/mitaa yote.
TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.