Uchaguzi 2020 Uchambuzi wa ilani ya CCM 2020-25 kwenye kupambana na umaskini na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi

Uchaguzi 2020 Uchambuzi wa ilani ya CCM 2020-25 kwenye kupambana na umaskini na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi

Nimeisoma ilani ya CCM kwa undani na nimeisoma ilani ya uchaguzi ya chadema kwa undani zaidi.

Nimeona ilani ya CCM ikizungumzia suaka ajira kwamba serikali itatengeneza ajira zisizopungua milioni nane kupitia mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na viwanda vitakavyojengwa.

Hii ilani angalau imegusia idadi(kiasi) kwa namba kwamba Kuna namna ya kuibana serikali Kama ikishindwa kutekeleza ahadi hiyo kama tunavyijua kuwa ahadi ni deni lakini kwa upande wa pili wametaja dhahiri kwa serikali itakayoundwa itatoa ajira kwa vijana lakini haija dhihirisha ni kiasi gani inategemea kutengeneza jambo ambalo linaleta ukakasi katika utekelezaji wake na ufuatiliaji wake kwa wananchi kwa serikali inaweza kutoa hata ajira laki tano na ikawa iko salama kwani wametaja ajira tu ila sio kiasi gani kitakachosalishwa Cha ajira

Sasa ni sisi tuulizane hii imekaaje katika mktafha wa utoaji ajira Ila mpaka hapo yenye mvuto zaidi ni ya CCM kwa uwazi wake
 
Ile Kauli ambayo Rais amesikika akiirudia mara kwa mara kuwa yupo kutetea wanyonge huidhihirisha kwa vitendo kwa kuwaondolea vikwazo katika maisha ya kila siku nikirejea vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo, utetezi wa maeneo yakufanyia biashara mamachinga, uzinduzi wa awamu ya tatu fedha za kujikimu kwa kaya Maskini maarufu kama TASAF. Hii ni ishara tosha kuwa Rais wetu yupo kwa maslahi ya Watanzania wote kwa hali zao.
 
Nipo napitia Ilani za Uchaguzi Vyama vitatu kwa Siku Kadhaa sasa.
-Ccm
-Chadema
-ACT Wazalendo...
Sawa
CcM F
Cdm ni nii F+ au F- au A?
AcT je ni A au E au nayo F?

Eleweka, hata hivyo nadhani ni chama kimoja tu ilani iko wazi zingine unaweza kutusaidia upload humu. Tunajua hazipo
 
Na Bwanku M Bwanku

Kama tulivyoona kwenye sehemu yetu ya kwanza ya kuichambua Ilani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 ili kila Mtanzania aweze kuielewa na kuifahamu Ilani hii ya Chama tawala hata kwa ambaye hana uwezo wa kuipata. Sehemu yetu ya kwanza tuliangalia kwa mapana kwa kuchambua yaliyomo kuanzia Sura ya kwanza mpaka ya nne. Leo sasa tunaendelea na safari yetu ya kuijua Ilani hii kwa kuendelea na Sura zingine kuanzia ya 5 na kuendelea ili tumalize Ilani nzima yenye Sura 10. Twende pamoja.

SURA YA TANO: *ULINZI NA USALAMA.* Sura hii inaanzia ukurasa wa 155 mpaka 160 wa Ilani hii. Sura hii inaeleza umuhimu wa ulinzi na usalama kama nyenzo muhimu katika kuwezesha wananchi kuishi na kuendeleza shughuli zao za kimaendeleo kiutulivu kabisa. Hapa panaonyesha namna Serikali ya CCM ilivyoendelea kuimarisha umoja, mshikamano, amani na utulivu, jambo lililoifanya Tanzania kuendelea kuwa mfano wa kisiwa na kitovu cha amani kote duniani.

Sura hii imeeleza pia namna Serikali ya awamu ya 5 ilivyoendelea kulinda na kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi na mipaka yake ili kuendelea kuifanya Tanzania kuwa na umoja, mshikamano, amani na usalama wa raia na mali zao hali iliyofanya Tanzania kutajwa kuongoza kwenye eneo la amani na utulivu katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Pia Sura hii imegusa namna Serikali ilivyoendelea kukabiliana na majanga, kuimarisha uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, kuboresha mazingira ya kazi kwa kuwapatia makazi bora, kuvipatia mafunzo ya kitaaluma na kitaalam, vitendea kazi na zana za kisasa na mengine mengi sana kwenye sura hii.

SURA YA SITA: *UTAWALA BORA, UTAWALA WA SHERIA NA MADARAKA YA WANANCHI:* Sura hii imejikita kufafanua adhima ya Serikali itakayoundwa na CCM kuendelea kuboresha utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, demokrasia na haki za binadamu, katiba na utawala wa sheria, Serikali za mitaa, vyombo vya habari, jumuiya za kijamii, jumuiya na asasi za kiraia pamoja na wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi ili kuhakikisha Tanzania inaimarisha mifumo yake ya utawala bora, utawala wa sheria na madaraka kwa wananchi kwa ajili ya maendeleo ya ustawi wa jamii unazingatia misingi ya utu, haki, ushirikishwaji, demokrasia, uwajibikaji, uwazi, utekelezaji, tija, ufanisi, usawa na ushiriki wa makundi yote kwenye jamii.

Sura hii iliyoanzia ukurasa wa 161 hadi 182 imejikita kuelezea namna Serikali itavyoendelea kusimamia na kuweka mkazo mkali wa maadili ya watumishi wa umma ili wananchi waendelee kupata huduma zao stahiki na kulinda rasilimali za nchi ili Taifa liendelee kupata faida lakini kuhakikisha makundi yote ndani ya jamii yanapata huduma, haki na stahiki zao kwa ubora na viwango vinavyohitajika.

SURA YA SABA: *MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA:* CCM inatambua wazi umuhimu mkubwa wa ushirikiano wa nchi yetu na nchi nyingine na fursa yake muhimu katika kuleta maendeleo. Sura hii imebainisha mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye eneo hili kwa miaka 5 tu ikiwemo ufunguzi wa Balozi mpya 8, kuongeza mauzo na biashara ya nje, kuendelea kudumisha diplomasia na urafiki wa nchi zingine, kushiriki shughuli zote za Umoja wa Mataifa na mengine mengi sana. Katika kipindi cha miaka 5, Ilani imeonyesha namna sekta hii ilivyokuwa na mchango mkubwa sana na kuimarika kwa mahusiano ya nchi kikanda na kimataifa ambayo yamekuwa na matokeo chanya makubwa kwenye uchumi na maendeleo.

Sura hii mwisho imeeleza pia kwa mapana namna Serikali itakayoundwa na CCM kwa miaka mitano ijayo itakavyohakikisha mahusiano yetu kikanda na kimataifa yanaendelea kuimarishwa katika maeneo yote, lengo likiwa kuifanya Tanzania inaendelea kuwa mstari wa mbele katika masuala ya kuimarisha amani, uhuru na maslahi ya Taifa katika nyanja za kimataifa ikiwa ni pamoja na kutumia fursa za kiuchumi zitokanazo na mahusiano hayo.

Hapa Serikali itakayoundwa na CCM itaelekeza kuimarisha maradufu diplomasia ya siasa, diplomasia ya uchumi, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, Umoja usiofungamana na upande wowote, Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika, mambo mtambuka ya kidiplomasia na Jumuiya zote nyingine za Afrika na Kimataifa ambayo yataifanya nchi yetu kuendelea kuheshimika kote duniani na kuvuna faida za kiuchumi kwa maendeleo ya Taifa letu.

Sura hii inachimbua sana namna Serikali itakavyoendelea kuiangalia na kuichukua sekta ya mambo ya nje kama daraja muhimu la kusukuma uchumi na maendeleo ya Tanzania. Sura hii inaanzia ukurasa wa 182 mpaka ukurasa wa 186. Tuishie hapa kwa leo.

Sehemu nyingine ya tatu na ya mwisho tutamalizia kuangalia na kuzichambua sura zingine tatu zilizobaki kwenye safari yetu ya kuijua na kuitambua Ilani ya CCM ya 2020 hadi 2025. Sehemu hiyo tutamalizia sura tatu zilizobaki kwenye sura ya nane, tisa na kumi ambazo ni Mazingatio maalum ya Ilani ya Zanzibar, maeneo mengine ya kipaumbele na Chama Cha Mapinduzi.

Ahsante[emoji1545]
images%20(9).jpg
images%20(8).jpg
 
Ama kwa Hakika ni Ilani nzuri kabisaaa.

October 28th sote kwa pamoja tukamchague JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom