Uchambuzi wa mwanzo wa katiba inayopendekezwa: Tusikubali maslahi binafsi yashinde maslahi ya taifa

Uchambuzi wa mwanzo wa katiba inayopendekezwa: Tusikubali maslahi binafsi yashinde maslahi ya taifa

Joined
Nov 15, 2010
Posts
19
Reaction score
232
Nimeisoma Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, nimeisoma yote, ni bahati mbaya inapigiwa upatu kwamba imebeba mambo ya wananchi, mambo ya wakulima, wafugaji, wavuvi, vijana na kadharika. Jamani hayo ni hadaa, msingi wa muundo umebadilishwa, Tanganyika imevalishwa koti jipya la Muungano, ambalo tusipokuwa makini itaendelea kuishi nalo muda mrefu zaidi. Kigezo cha kukataa serikali 3 hakina hoja zenye mashiko, wanasema Hati ya Makubaliano ilisema serikali 2 hivyo hatuwezi badili, huu ni uongo, mbona Hati ilisema mambo ya Muungano ni 11, mbona wao wameweka 14, uhalali wa kubadili mambo ya Muungano kama Hati haibadiliki wanaupata wapi.? Hii ni double standard. hati haikujieleza kwamba kwa baadhi ya maeneo mwiko kubadili na ruksa kwa mengine, Amka ee Mtanzania.


Unasema katika Sura ya Pili unaanzisha Tume ya Mipango ya Taifa ilhali ukijua Zanzibar wana Tume ya Mipango pia, nashangaa sana. Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa inasema Kutakuwa na Dira, Ohoo, kutakuwa tena, nilidhani inapaswa itamkwe, na kwa asili ya "Programmatic Constitutions" Dira inakuwa ni ujumla wa Lengo Kuu la Katiba Pamoja na Malengo Mahususi kama ilivyokuwa kwenye Rasimu..


Wamefuta kumwajibisha Mbunge, wamefuta ukomo, wamefuta mbunge asiwe waziri, wamefanya ugombea binafsi kuwa mgumu zaidi, wamevuruga Tume ya Uhusiano na Uratibu, wao wamesema Tume hii ni kwa Mambo ya Muungano, hili ni kosa kubwa la kisanifu (design), Mambo ya Muungano yanasimamiwa, yasiyo ya Muuungano yanaratibiwa. Wameweka Baraza la Vijana, vijana wenzangu hii ni hadaa, walio wengi ni wanawake mbona lao hawakuliweka, ninazingatia haki hapa, wanataka kuwahamasisha kwa mambo ambayo katika utalaamu na uandishi wa Katiba hayapo, yamewekwa ili msahau yale waliyofuta.


Wamerudisha wakuu wa Mikoa, wananchi mlisema sana juu ya uwepo wa wakuu wa mikoa na wilaya.. kwa namna walivyo rudi sitashangaa wakiendelea kuwa makada wa vyama vya siasa. Haya maoni ya kuwaweka wakuu wa mikoa katika namna hii wameyatoa wapi.? Maoni hayo mimi sikuyaona Tume ya Katiba kipindi chote nilichokuwepo.


Vyanzo vya mapato ni vile vile kwa serikali ya muungano (Katiba ya 1977) na wakadhani mwarobaini ni kurejesha Tume ya Pamoja ya Fedha ambayo haikuwahi kufanyiwa kazi (kuna sababu kubwa zaidi kuliko kuwa na Tume ya Pamoja ya Fedha), Bahati mbaya Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa imelikosa hili.


Rasimu ya Katiba inayopendekezwa inasema Makamu wa Rais Watatu, Makamu wa Kwanza (Muungano), Makamu wa Pili (Rais wa Zanzibar) na Makamu wa Tatu (Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano)... Jamani watanzania wenzangu, huu UTATU mbona tunapewa kwa mgongo wa chupa, TATU tunaziogopea nini.? Tume ya Pamoja ya Fedha iliwaambia anzisheni akaunti ya pamoja ya fedha, ikawa kigugumizi, leo kipi kitafanya tuweze?


Mnasema Mahakama Kuu ya Zanzibar na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano zitakuwa na Mamlaka sawa (concurrent jurisdiction), hata kwa jina hapo si tunadanganyana.? Hakuna kitu kama Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, kwasababu ninyi mnajua haina Mamlaka Zanzibar sasa kuiweka kwenye Muungano kunani.?


NINAENDELEA NA UCHAMBUZI, KAMA NILIVYOSEMA KAZI NDIO KWANZA IMEANZA.


Kwa taarifa zaidi ungana nami hapa Humphrey Polepole kisha LIKE na tutakuwa pamoja.


Waraka huu sijauhariri.
 
Ni aibu na usaliti wa hali ya juu, wajumbe BMK wanawezaje kufuta na kuchakachua ibara ya 20 ya rasimu ya pili kuhusu Miiko ya uongozi wa Umma? Hivi kweli hawa watu wanalipenda taifa lao???!
 
Hapa ni kutayarisha kitambulisho tu ili nipige kura ya HAPANA....

Ingekuwa vema kama kuna uwezekano wa kuwaadhibu hao waliopo huko kwa ajili yao wanaodai ni kwa ajili yetu
 
Mlitaka kutengeneza katiba yenu na mzee warioba lakini sasa ndiyo basi hii ni katiba ya watanzania hatutaki katiba ya walevi kama wewe na warioba.
 
Wamenikera sana hawa watu,fikra hafifu,fikra za matumbo yao,
Kuumpa raisi madaraka mengi,tulisha kataa,mawaziri kuwa wabunge tulikataa.
Ulikataa bila hoja lakini wengine wenye hoja walipenda iwe hivyo.
 
Hii katiba ni ya kupiga chini tu. Kulikuwa na uzi hapa wa kuhusiana na makanisa kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo kwa kuchakachua maoni ya Watanzania. Hivyo mmoja wa maaskofu kuyataka makanisa yote nchini yawaambie waumini wa madhehebu mbali mbali nchini wakatae huu ujinga na dharau kubwa iliyofanywa na hawa Maintarahamwe hivyo kupiga kura ya kuikataa katiba hiyo ya MACCM.

https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/729225-askofu-wa-katoliki-aeleza-njia-mpya-kuzuia-katiba.html
 
Rasimu ya Katiba kama hii iliyotolewa na BMK haina maana kabisa kwa kushindwa kujua muundo uliopo sasa hivi, matatizo ya kiutendaji kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar --- haiwezi hata kupendekezwa na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria wa chuo kikuu. Tumeliwa kabisa maana mahakama kuu ya Jamhuri ya Muungano ambayo mipaka yake inaeleweka inakuwa haina mamlaka ndani ya mipaka yake.... mahakama ya nini hiyo?
 
Wapemba wana neno lao wanasema 'FUDU'
 
Kweli kabisa swala la mbunge Kuwait waziri tulikataa,raisi kuwa na madaraka mengi muundo wa muunga serikali 2 hatutaki tunaitaka TANGANYIKA ILI TUJIKWAMUE KWENYE WIMBI LA MATESO YA WATU WACHACHE KAMA HAWA CCM NA WENGINE WATAKAOSHIKA MADARAKA KIFUPI RASIMU YA WARIOBA NDIYO CHAGUO LETU KWA VIZAZI VIJAVYO IWE IWEJE TUTAPIGANIA HAKI HII MPAKA KIELEWEKE EE MWENYEZI MUNGU MUUMBAJI WETU TUSAIDIE KTK HILI HATA KWA KIFO ILI TUPATE MFUMO BORA WA MAISHA AMEN BY MTANGANYIKA KWA ASILI
 
Asante bwana HP tupo pamoja, hii kazi ni ngumu sana lakini vyote vilivyowezekana leo wakatifula vilionekana haviwezekani. Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake. Humphrey Polepole
 
Last edited by a moderator:
Bora wangehacha suala la Muungano pekee; lakini mambo ya msingi ambayo wananchi waliyakataa hawa Washe^#! wameyarudisha, AIBU kubwa:


  • Hakuna suala linaumiza kama kushindwa KUMWAJIBISHA MBUNGE kabla ya muda wa miaka 5! Kulihacha suala hili liendelee pasipo hata kuweka alternative measures ni USALITI mkubwa.
  • Suala la Mbunge kuwa WAZIRI limepigiwa kelele sana, hawa jamaa wameamua kutusaliti na kulihacha hivyo hivyo
  • MADARAKA ya RAIS kila Mwananchi alikuwa anapiga kelele, hawa jamaa wamejaza matumbo yao na kuongeza madaraka zaidi
  • Wakuu wa WILAYA/MIKOA wamepigiwa kelele kila kona... laiti CCM ingejua wakitoka madarakani hawa watu watakuwa mwiba kwao kuliko hata ilivyo kwa upinzani sasa, wangetoa kabisa huu upuuzi

Shime wananchi, jambo la kwanza ikiingia mitaani ni KUICHANA hadharani kuonesha chuki ya wazi. OMBI, tupendekeze njia ya kuwashughulikia wote walioshiriki kurudisha mambo ambayo Wananchi waliyakataa kwa WAZI.
 
Back
Top Bottom