Uchambuzi wa soka TBC World cup 2014 Brazil(by mwl.kashasha)

Danny Massawe

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
1,297
Reaction score
758
TBC huwa siwakubali linapokuja swala la wachambzi wa soka katika mechi mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Lakini huyu mchambuzi wa sasa wanaemuita MWALIMU KASHASHA anajitahidi kuchambua mpira vizuri. Wadau wa kandanda mnamuonaje mwalimu/mchambuzi huyu??
 
Wachambuzi wenyewe ndo uwezo mdogo sasa tbc iwatoe wapi? Watu kweli hamna uzalendo na chombo chako cha umma. Tbc pamoja na bajeti finyu wanafanya vizuri jamani tujivunie, kama ni makosa madogo basi tutoe ushauri mzuri badala ya kuponda.
 
Hatimaye TBC wamepata mchambuzi makini Mwl. Kashasha.
Anawajua wachezaji na mechanism ya soka.
Huyu anafaa sana utapenda kumsikiliza !
... namkubali !
 
Hatimaye tbc wamepata mchambuzi makini wa soka.
Huyu Mwl Kashasha anaujua mpira, wachezaji na mbinu za kisoka.
Namkubali sana !
...ameziba pengo la Dr Liki.
Sasa World Cup ina raha
 
Ni kweli kabisa.
Ila tbc isiwarudishe tena wale watabiri wanaoshabikia badala ya kufanya analysis
 
Nilitaka nikalale lakini kwa anavochambua kitaalamu dah nimejikuta nasubiri mechi ya night kali. I wish angeombwa kuinoa timu yetu ya taifa. Mnamwonaje wakuu?
 
huyu mzee ata mimi nimemkubali sana ni mwalimu hasaa wa mpira.kuhusu kua kocha wa timu ya taifa huko sina la kusema!
 
Nilitaka nikalale lakini kwa anavochambua kitaalamu dah nimejikuta nasubiri mechi ya night kali. I wish angeombwa kuinoa timu yetu ya taifa. Mnamwonaje wakuu?

Mbona nilimsikiliza kabla ya mechi ya Spain na Chile, alikuwa na uhakika kabisa Spain watashinda! kashushuka shuu. Gozi langu limenuna limeenda kulala baada ya mechi maana alikuwa anaishabikia Spain na mimi kwa ushindani tu nikawa naishabikia Chile.

Kwi kwi kwi teh teh teh!

Watanzania porojo tu, huyo mwalimu aangekuwa anajuwa mpira si tungeona mafanikio ya timu zetu? maneno mengi vitendo kidogo, hiyo ndio kawaida ya Watanzania walio wengi.
 
Hahahaaaaaa gozi? mkuu utanyimwa.......

Anaonekana anajua soka ni mwalimu wa mpira
Dr.Riki Abdala aka Google wa Soka ni mzuri kwa uchambuzi wa soka

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
ametulia sana na anaamini katika anachokisema, jana alisema kabisa kwamba tutegemee maadfa mechi ya kameruni na croatia kwani kameruni hamna kitu and it happened exactly
 
Jana nili-tune TBC wanajitahidi kiasi chake ila yule jamaa anayeitwa Mziba ni kanjanja kabisa hana anachokijua
 
huyu mwalimu ni mtaalamu haswa na amesoma kozi mbalimbali za soka, ukimsikiliza anavyoongea huwa anaongea kitaalamu zaidi na si kishabiki kama kiongozi wangu Kimwaga na yule mziba!
pia huwa anachagiza na terminologies fulani za kisoka ili kuonyesha msisitizo
 
Mbona nilimsikiliza kabla ya mechi ya Spain na Chile, alikuwa na uhakika kabisa Spain watashinda! kashushuka shuu. Gozi langu limenuna limeenda kulala baada ya mechi maana alikuwa anaishabikia Spain na mimi kwa ushindani tu nikawa naishabikia Chile.

Kwi kwi kwi teh teh teh!

Watanzania porojo tu, huyo mwalimu aangekuwa anajuwa mpira si tungeona mafanikio ya timu zetu? maneno mengi vitendo kidogo, hiyo ndio kawaida ya Watanzania walio wengi.
kazi ya mkufunzi wa soka sio kutabiri bali ni kuchambua kiufundi na kitaalamu, technically spain walikuwa vizuri sana zaidi ya chile, hivyo kwa mchambuzi yeyote anayejua soka lazima angempa ushindi spain kwa maana ya rank yao, squad depth yao, rekodi zao na kadhalika zilikuwa zinawafanya wawe favorite kushinda, ingawa ktk actual game lolote linaweza kutokea ndio maana Chile wakashinda!
 
DSTV hakuna sauti TBC, kuna mwingine amekutana na hili tatizo?

Linatatuka vipi?
 
kazi ya mkufunzi wa soka sio kutabiri bali ni kuchambua kiufundi na kitaalamu, technically spain walikuwa vizuri sana zaidi ya chile, hivyo kwa mchambuzi yeyote anayejua soka lazima angempa ushindi spain kwa maana ya rank yao, squad depth yao, rekodi zao na kadhalika zilikuwa zinawafanya wawe favorite kushinda, ingawa ktk actual game lolote linaweza kutokea ndio maana Chile wakashinda!

Kama Mwalim wa mpira alitakiwa ajuwe mpira uko duara na unadunda, hakuna team pale ambayo ina uhakika wa 100% kushinda, maneno yake yalikuwa ..."leo Spain itashinda", hiyo ilikuwa katika uchambuzi kabla ya mechi, nakumbuka sana hayo maneno kwani niliuliza na niliokuwa nasikiliza nao, "huyu ni Mwalim au Mtabiri?". hata mimi nisiyejuwa sana mambo ya mpira nilishangaa ikanibidi niishangilie team ambayo alikuwa na uhakika itashindwa, kwa ushabiki tu wa kuwa na "underdogs".

Matokeo? nimenuniwa na Gozi langu, kwani na lenyewe lilikuwa na uhakika wa Spain kushinda.
 
Nahisi umechukizwa zaidi na huko kununiwa kuliko utabiri wake, maana kwa asili yake neno 'kutabiri' ni kukisia na kukadiria. Ndio maana hata Mamlaka ya Hali ya Hewa licha ya vifaa na utaalamu wote walio nao, huishia na kauli 'matazamio ni mabadiliko kidogo'. Kwa hivyo mtu anapotabiri ujue anakusudia 'huenda ikawa ....' na sio 'lazima itakuwa'. Kwa anayefahamu maana ya utabiri, huwa halazimiki kuweka. 'Disclaimer' hiyo. Ndivyo alivyosema mwalimu huyu. Alaumiwe kwa jengine, kama lipo.
 
Neno utabiri nimeuliza mimi, nisome vizuri hakusema yeye. Yeye kasema "leo Spain itashinda" tena expression yake ilikuwa inaonesha ana uhakika kabisa.

Ninune? khaa! Faiza mie kununa huwa nnakusikia kwa wengine tu, AlhamduliLlah si sifa yangu hiyo. Unanchekesha.
 
Wachambuzi wenyewe ndo uwezo mdogo sasa tbc iwatoe wapi? Watu kweli hamna uzalendo na chombo chako cha umma. Tbc pamoja na bajeti finyu wanafanya vizuri jamani tujivunie, kama ni makosa madogo basi tutoe ushauri mzuri badala ya kuponda.

hamna lolote pale,wanachambua mpira kwa kuangalia upepo wa mechi.
Mi nimekomaa na akina Gigs na okocha nawaelewa hivo hivo,japo kizungu hakizoeleki
 
Back
Top Bottom