Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Kama kuna jambo kwa sasa ambalo kama Taifa tunakubaliana, ni kuwa UCHAWA ndilo tatizo linalokua kwa kasi zaidi katika siasa zetu na sekta ya utumishi wa umma.
Athari za uchawa ni bayana; kwakuzitaja chache ni uteuzi wa watu wenye sifa duni, upandishwaji vyeo watu wasio stahili, kushuka kwa uwajibikaji, kushuka kwa uwazi na ukweli, matumizi mabaya ya madaraka n.k
Pamoja na athari hizi nilizozitaja kuwa bayana, sote ni mashahidi wa hali halisi ilivyo sasa. Sio siri uchawa umekuwa ni mkakati rasmi wa baadhi ya wenzetu kutafuta vyeo, kulinda nafasi walizonazo na hata kufanikisha agenda zilizobeba maslahi yao binafsi.
Swali kubwa tunalopaswa kujiuliza tumefikaje hapo? Kwa maoni yangu chimbuko la uchawa ni katiba yetu. Katiba imerundika madaraka karibu yote ya kuteua, kutengua, kupandisha, kushusha cheo n.k mikononi mwa mtu mmoja, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jaribu kutafakari, ni njia gani mtanzania wa kawaida ataitumia ili ateuliwe kuwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa halmashauri, mkurugenzi wa shirika la umma, mwenyekiti wa bodi, n.k. Jibu linabaki kuwa ni kwa KUMPENDEZA RAIS!
Huo ndio mzizi halisi wa UCHAWA. Kila mtu anafatuta kumpendeza Rais, ili aonekane na Rais, maisha yake yasonge mbele. Katika mazingira haya tutawalaumu bure wasomi wetu, watendaji wetu na hata wanasiasa wetu. Kwakuwa mwisho wa siku wanatafuta maisha na fursa ya kuyapata hayo maisha katiba imempa Rais.
Kama kweli tunataka kumaliza tatizo la UCHAWA jibu lake ni kupunguza madaraka ya Rais kuteua kila mtu. Katiba mpya iweke utaratibu wa watu kupanda vyeo kwa weredi, nidhamu na utendaji wao. Vyeo vipatikane kwa mchakato wa wazi wa kushindana, kutolewa kwenye cheo kuwekewe utaratibu wa wazi unaofahamika. Rais ateue tu mawaziri, naibu mawaziri na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Tukifanya hivyo tutapunguza sana tatizo la uchawa.