Uchawa ni mfumo, bila Katiba mpya hauwezi kuisha

Uchawa ni mfumo, bila Katiba mpya hauwezi kuisha

Bila umasikini wa kiuchumi kwa familia na mtu mmojammoja kukuzwa hakuna litakaloiokoa nchi.Elimu ya kujitambua na kujithamini nayo ni muhimu sana.Chawa wote kama si wengi ni masikini wa kiuchumi na hawajitambui.
 
Naungana na wewe hapa. Halafu watu watambue kuwa siyo kila mtu akipinga / kukubali jambo fulani ni kwa mantiki ya kisiasa.

Hii serikali ina mapungufu lukuki lakini kuna maeneo imegusa kuliko serikali zilizopita. Jambo mojawapo ni ajira kwa vijana,

Lakini haiondoi kuwa mabadiliko hayahitajiki. Mabadiliko ya katiba ishakuwa jambo la lazima kwa hali ya sasa.

Sasahivi hata rais kumteua mtu wa form four kuwa naibu waziri ukichunguza zaidi unaweza kuona hakuna utofauti na hata angeteuliwa prof fulani hiyo nafasi[ umuhimu wa katiba mpya].

Naamini hata CCM wale hawapo kwenye mirija ya ulaji wanahitaji katiba mpya.
Naungana na wewe comrade. Kwa hapa tulipofikia katiba imeshakuwa hitaji la lazima.
 
Bila umasikini wa kiuchumi kwa familia na mtu mmojammoja kukuzwa hakuna litakaloiokoa nchi.Elimu ya kujitambua na kujithamini nayo ni muhimu sana.Chawa wote kama si wengi ni masikini wa kiuchumi na hawajitambui.
Comrade, wanaongoza kwa uchawa ni vigogo, tena wasomi wakubwa!
Mtu asiye na elimu au sifa zingine hana sababu ya kujipendekeza, kwasababu hana sifa za kumwezesha kuteuliwa.
Kwa upande mwingine watu wenye elimu na nafasi ndio wapo kwenye hatari kubwa ya kuwa chawa. Kichocheo kikubwa kikiwa ni tamaa ya kupata uteuzi au kupanda cheo au hata kulinda cheo.
 
Daktari!

Hongera kwa andiko.

Binafsi nakubaliana nawe, lakini nina angalizo juu ya hili au mtizamo wa nyongeza.

Katiba peke yake si suluhisho la kutoka hapa tulipo. Hapa tulipo tatizo bado si katiba peke yake bali tumekengeuka tangu kwenye malezi kuanzia ngazi ya jamii/familia.

Naamini katiba mpya haitakuja kutibu matatizo yetu kama hatutarudi kwenye kuangalia mifumo ya malezi yetu tangu ngazi ya familia. Mtoto au mtu aliyelelewa kwa maadili mema na akayaishi, haitaji kuta kuubwa au sheria kumzuia kutenda uharifu. Sheria inabaki kuwa mwongozo wa kufuata, wakati hiari iko ndani yako. Kwa sasa kulingana na kizazi hiki kukosa maadili, tunatafuta jinsi ya kutoroka mkono wa sheria kisomi. Na huyo ndo mjanja na anasifiwa na jamii anapofanikiwa. Ukiishi kwa kadri ha taratibu, wewe ni tatizo kwa jamii inayokuzunguka.

Hii imefanya sehemu kubwa ya jamii yetu kuwa na watu wasioaminika. Kufanyakazi au biashara na Mtanzania ni zoezi gumu kwa ndani ya nchi na nje ya nchi, kifupi hatuaminiki.

Wale wanaoenda kuitengeneza katiba wenyewe wamejaa u-mimi, ndo maana kinachowagusa wao au kitakachowagusa kwa mfumo hasi kwao hawakipendi na hawatakigusa.

Unaweza kuwaza kwa wakati huu kuwa na mtunga sheria anaejua kusoma na kuandika tu!!!?? Ila mfagiaji wa ofisi/support services anatakiwa awe amemaliza kidato cha nne!!??

Jamii iliyokinyume na taratibu imepata nafasi kijamii kuliko inayofuata taratibu.
Wanaotuongoza wanatumia nafasi hiyo kwenda pia kinyume na taratibu.

Tujitafakari sana na kuchukua hatua kwa pande zote mbili.
Ahsante comrade kwa mchango mzuri. Nikiri nimelisoma tena na tena hili andiko lako, ninaamini limeleta mtazamo mpya wa maudhui yangu.
Nakubaliana na wewe kuwa katiba, sheria na miongozo bila kuwepo kwa misingi mizuri ya maadili haviwezi kuleta mabadiliko ya kweli.
Hongera sana kwa mchango mzuri!
 
Kama kuna jambo kwa sasa ambalo kama Taifa tunakubaliana, ni kuwa UCHAWA ndilo tatizo linalokua kwa kasi zaidi katika siasa zetu na sekta ya utumishi wa umma.

Athari za uchawa ni bayana; kwakuzitaja chache ni uteuzi wa watu wenye sifa duni, upandishwaji vyeo watu wasio stahili, kushuka kwa uwajibikaji, kushuka kwa uwazi na ukweli, matumizi mabaya ya madaraka n.k

Pamoja na athari hizi nilizozitaja kuwa bayana, sote ni mashahidi wa hali halisi ilivyo sasa. Sio siri uchawa umekuwa ni mkakati rasmi wa baadhi ya wenzetu kutafuta vyeo, kulinda nafasi walizonazo na hata kufanikisha agenda zilizobeba maslahi yao binafsi.

Swali kubwa tunalopaswa kujiuliza tumefikaje hapo? Kwa maoni yangu chimbuko la uchawa ni katiba yetu. Katiba imerundika madaraka karibu yote ya kuteua, kutengua, kupandisha, kushusha cheo n.k mikononi mwa mtu mmoja, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jaribu kutafakari, ni njia gani mtanzania wa kawaida ataitumia ili ateuliwe kuwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa halmashauri, mkurugenzi wa shirika la umma, mwenyekiti wa bodi, n.k. Jibu linabaki kuwa ni kwa KUMPENDEZA RAIS!

Huo ndio mzizi halisi wa UCHAWA. Kila mtu anafatuta kumpendeza Rais, ili aonekane na Rais, maisha yake yasonge mbele. Katika mazingira haya tutawalaumu bure wasomi wetu, watendaji wetu na hata wanasiasa wetu. Kwakuwa mwisho wa siku wanatafuta maisha na fursa ya kuyapata hayo maisha katiba imempa Rais.

Kama kweli tunataka kumaliza tatizo la UCHAWA jibu lake ni kupunguza madaraka ya Rais kuteua kila mtu. Katiba mpya iweke utaratibu wa watu kupanda vyeo kwa weredi, nidhamu na utendaji wao. Vyeo vipatikane kwa mchakato wa wazi wa kushindana, kutolewa kwenye cheo kuwekewe utaratibu wa wazi unaofahamika. Rais ateue tu mawaziri, naibu mawaziri na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Tukifanya hivyo tutapunguza sana tatizo la uchawa.
Warioba aliandaa rasimu nzuri ila tu machawa hawataki.
 
Point nzuri mkuu ningelikuwa rais ningelivunja bunge nikaanza mchakato wa kuchagua wabunge upya at least wawe na degree au masters
Hapa hili ni taifa la watu wote
Wasomi na wasio wasomi.
Hatuwezi kuwa na bunge linalobagua watu kwa misingi ya kielimu. La sivyo yawekwe mazingira ya kuhakikisha kila mtoto aliyepo shule kwa sasa anafika ngazi hata ya diploma au degree kabla ya kuja na kigezo cha kutaka mbunge awe na degree.
 
Back
Top Bottom