Uchawa utaliangusha taifa

Uchawa utaliangusha taifa

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Hii tabia ya kila kitu mama mama mama inachosha kuchusha kuboa na kutia kinyaa.

Unakuta kijana ana nguvu zake safi tu badala achape kazi atoboe yeye anashabikia mtu ili apate kitu.

Ukiona WALIMU WANAFUNZI WA vyuo nk wanatengeneza makundi ya whasap na kujinasibisha na mama sio kwamba wanampenda hapana wanasaka fursa.

Nyerere aliwahi kuonya juu ya kujipendekeza kunavyoweza kuzaa mauti ya mtu na taifa. Naishauri IDARA iiuwe hii tabia ya unafiki inaliangamiza taifa.
 
upo sahihi kwa sababu target ya uchawa ni kupata teuzi ,au aina fulani ya upendeleo kwenye angle ambayo yawezekana hakustahili .

tunaona sasaivi kila mtu mama ! mama! mama!mama! ili kuongeza uwezekano wa upendeleo kwenye nyazifa teuI n.k

uchawa will destroy our beautiful TANZANIA ever
 
Aahaa, naona kumbe uchawa ni sawa na rushwa, hivyo TAKUKURU ipambane na janga la uchawa.
 
Nchi hii isipopara Katiba inayotoa mamlaka Kwa watu wachache na wengine wakingojea hisani huku wakiwa hawawezi kuwawajibisha hao wayeule, basi ujue hakuna lolote....Tupigane kufa na kupona kupata mwongozo wa kitaifa i.e Katiba ambayo itamfanya Kila mtu awajibike kupitia sheria kanuni na taratibu...Itaounguza sana hizi shida za kutafuta hisani Kwa "wakubwa" na makundi yao
 
Hii tabia ya kila kitu mama mama mama inachosha kuchusha kuboa na kutia kinyaa.

Unakuta kijana ana nguvu zake safi tu badala achape kazi atoboe yeye anashabikia mtu ili apate kitu.

Ukiona WALIMU WANAFUNZI WA vyuo nk wanatengeneza makundi ya whasap na kujinasibisha na mama sio kwamba wanampenda hapana wanasaka fursa.

Nyerere aliwahi kuonya juu ya kujipendekeza kunavyoweza kuzaa mauti ya mtu na taifa. Naishauri IDARA iiuwe hii tabia ya unafiki inaliangamiza taifa.
Vijana wanaoshabikia ccm ni wanashida hasa compos mentis.
 
"Utii ukizidi
unakuwa UOGA. Uoga huzaa
UNAFIKI na KUJIPENDEKEZA
mwisho wake ni MAUTI".
 
Najaribu kuwaza kama Nyerere angekuwepo hii tabia ya uchawa angeisemeaje?
Utawala wa kiimla daima huzaa tabia ya uchawa na chawa. Enzi za Nyerere chawa walishamiri ila walikuwa wastaarabu zaidi ya hawa kizazi hiki. Kuna kijana aliyeitwa Seth Benjamin, alitembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Dar (hakufika) eti kuunga mkono azimio la Arusha. Amesahaulika kama lilivyosahaulika azimio aliliolifia
 
Back
Top Bottom