Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Huwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA.

Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani. Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi.

Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani.

Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu. Nilienda kwenye mishe zangu personal. Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE. Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake.

Kule mahakama ya haki ni ushirikina hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana. Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia. Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu.

Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae. Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta. Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako.

Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha. Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule. Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima.

Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba, shughuli za kiserikali na miradi.

Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana. Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa.

Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!

Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya. Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je, dereva wake kakimbilia wapi?
Je, wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?

Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio. Na nikienda huko nitawaletea mrejesho.

IMG-20210623-WA0029.jpg
 
Kwa mazingira hayo, mbona ni tukio la kawaida. Huyo dada shuhuda anasema gari lilitembea bila dereva/ kuendeshwa ni uchawi, kama handbrake/ emergency brake imeachia au haikuwa engaged na kuna mtelemko na nyumba ipo bondeni ajabu ni nini hapo?
 
Nawaambiaha watu huko upareni ndio kuna magwiji wa kila sekta ya ulozi...tena kubwa ulilosema ni ushirikiano wa waganga...yani kama mganga Ilo tatizo yeye sio master,,basi anampigia mkali wa hio sector na unasolviwa tatizo faster
 
Kwa jinsi supervisor wa shemeji anavyoiburuza kampuni nzima mpaka bosi wa kampuni mimi nakuambia ulozi upo. Yaani HR akiambiwa anakuambia huyo Supervisor ndiyo alivyo hivyo hivyo na bosi hua hana cha kumfanya.

Sasa nikamshauri shemeji, ajiendeleze kielimu kidogo kisha afanye namna apate nafasi ya juu ofisini ambayo haitamtaka asimamiwe na supervisor.

Akanijibu "Kua bosi bongo miyeyusho, kwani na mi si nitakua nasimamia watu nitakua bosi wao? Sasa ninaowasimamia waniloge ili niwapende, nyumbani dada yako aniloge nimpende, mchepuko uniloge ili nizidi kutoa hela, bosi aniloge nisifikirie kuacha kazi, hapo mgahawani nilogwe nisihame mgahawa mwisho niwe zombi kwa mchanganyiko wa madawa. Nitakomaa na huyu mwana hadi kieleweke"
 
Sasa ninaowasimamia waniloge ili niwapende, nyumbani dada yako aniloge nimpende, mchepuko uniloge ili nizidi kutoa hela, bosi aniloge nisifikirie kuacha kazi, hapo mgahawani nilogwe nisihame mgahawa mwisho niwe zombi kwa mchanganyiko wa madawa. Nitakomaa na huyu mwana hadi kieleweke"[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimezaliwa Makanya
Nimekulia na Kusomea Makanya kuanzia chekechea, shule ya msingi mpaka Kidato cha nne,
Niliondoka Makanya nilipofaulu Kidato cha nne.

Makanya ndio kwetu, Makanya ndio watu wangu, nami ni mtoto wao.

Hayo unayosema yapo Kwa kiasi,

Makanya Ushirikina na Uchawi upo na unaathari labda Kwa wageni wasio wazawa.

Makanya inamchanganyiko wa Makabila kutokana na kilimo cha zao la Mkonge.

Wenyeji wengi ni Wapare,
Lakini pia kuna
Wamasai, wasambaa, Wachaga kidogo, Warundi, Wanyambo, Wasukuma, NK.

Pia wapo wanyiramba.

Uchawi Kwa kiasi kikubwa unapatikana Milimani ambapo ipo Mashariki mwa kamji Ka Makanya.

Wasambaa na watu wa Tanga wameongeza nafasi ya UCHAWI katika mji huo wenye ukame.

Makanya ndio Makao makuu ya Biashara ya Mirungi Afrika Mashariki.

Mirungi hiyo itokayo Milimani hasa Tae, Suji, Parane na Chime ina ladha inayopendwa na watumiaji ukilinganisha na Mirungi ya Kenya na Somalia.

Uchawi pia unaisaidia Biashara hiyo ya Mirungi kuendelea kuexist mbali na Rushwa.

Polisi Wanoko wasiotaka Rushwa hukipata cha mtema kuni wakifuatilia Wauza Mirungi huko Milimani.
Hivyo hujikuta wanapata madhara na kuamua kuacha au huamishwa kabisa kituo cha kazi.

Kipindi nakua, baadhi ya ajali za barabarani zilihusishwa na Uchawi na Ushirikina.

Makanya pia ni moja ya miji iliyojaliwa Madini ya Mawe ya Nasi(Gypsum stone) ambapo hutumika kutengeneza Saruji(Cement).
Ipo dhana katika mji huo kuwa Migodi ya Jasi inaathiri unyeshaji wa Mvua.
Watu wa Makanya kipindi nakua waliamini kuwa Mvua inahamishwa na wenye Migodi ya Mawe Jasi.

Ni kawaida Makanya Wingu Jeusi kutanda lakini upepo ukatokea na kupeperusha mawingu hayo na mvua kugoma kunyesha.

Hata hivyo, kitaaluma Tabia nchi ya Makanya na tambarare ya magharibi ya wilaya ya SAME ni SEMI-ARID DESERT.
Hivyo sifikiri uhaba wa Mvua Makanya unaotokana na uchawi na Ushirikina Bali ni tabia ya nchi ya eneo hilo

AINA ZA UCHAWI ULIOPO MAKANYA KULINGANA NA ASILI;

1. Uchawi wa Wapare wenye asili ya Milimani sio Tambarare
2. Uchawi wa kisambaa
3. Uchawi wa kizigua na Kibondei
4. uchawi wa Kimasai unaotokea magharibi ya Mji wa Makanya ambapo kuna Mji wa Ruvu.
5. Uchawi wa Kirundi kutokana na Wakazi wa Makanya wenye Asili ya Burundi ambao wengi walikuja kufanya vibarua kwenye mashanba ya Mkonge

6. Uchawi wa Wanyambo na Wasukuma. Hawa pia walikuja Kama vibarua vya Mkonge.

7. Uchawi chotara
Ambao kutokana na mchanganyiko wa Makabila Makanya kuna uchawi chotara.
Wachimba Jasi wanaotaka Maeneo mengine ya Tanzania wamechangia kiasi katika uchawi huu.

Msamiati Kama Zongo ni moja ya maneno ya kawaida Makanya.

Kuvunja Jungu, n.k
Makanya na Hedaru ni moja ya miji Maarufu wilayani Same na pia inaongoza Kwa ujanja ujanja.

Sisi Wana Makanya tunapendana mno,
 
Hakuna uchawi hapo, huko same, ugweno ni sehemu ya milima sana, hii gari ilipaki kwenye mnara wa simu, minara ya simu kwa meneo haya, ipo kwenye milima, nyumba unaziona kwa chini, gari iliserereka tu, kwa Mujibu wa polisi, dereva yupo ndani.

Kwa wale ambao wmeishapita njia ya kwenda Tunduma, ukitoka Songwe/vwawa,Kuna sehemu inaitwa Anseketwa,mkono wa kushoto juu, kuna mlima, na juu Kuna mnara wa simu,nyumba za watu zipo chini.

Au kama umewahi Kufika Chenene Dodoma, njia ya kwenda Kondoa, au Kibaya Hill Kiteto, ni mazingira kama hayo.
 
Nimezaliwa Makanya
Nimekulia na Kusomea Makanya kuanzia chekechea, shule ya msingi mpaka Kidato cha nne,
Niliondoka Makanya nilipofaulu Kidato cha nne.

Makanya ndio kwetu, Makanya ndio watu wangu, nami ni mtoto wao.

Hayo unayosema yapo Kwa kiasi,

Makanya Ushirikina na Uchawi upo na unaathari labda Kwa wageni wasio wazawa.

Makanya inamchanganyiko wa Makabila kutokana na kilimo cha zao la Mkonge.

Wenyeji wengi ni Wapare,
Lakini pia kuna
Wamasai, wasambaa, Wachaga kidogo, Warundi, Wanyambo, Wasukuma, NK.

Pia wapo wanyiramba.

Uchawi Kwa kiasi kikubwa unapatikana Milimani ambapo ipo Mashariki mwa kamji Ka Makanya.

Wasambaa na watu wa Tanga wameongeza nafasi ya UCHAWI katika mji huo wenye ukame.

Makanya ndio Makao makuu ya Biashara ya Mirungi Afrika Mashariki.

Mirungi hiyo itokayo Milimani hasa Tae, Suji, Parane na Chime ina ladha inayopendwa na watumiaji ukilinganisha na Mirungi ya Kenya na Somalia.

Uchawi pia unaisaidia Biashara hiyo ya Mirungi kuendelea kuexist mbali na Rushwa.

Polisi Wanoko wasiotaka Rushwa hukipata cha mtema kuni wakifuatilia Wauza Mirungi huko Milimani.
Hivyo hujikuta wanapata madhara na kuamua kuacha au huamishwa kabisa kituo cha kazi.

Kipindi nakua, baadhi ya ajali za barabarani zilihusishwa na Uchawi na Ushirikina.

Makanya na Hedaru ni moja ya miji Maarufu wilayani Same na pia inaongoza Kwa ujanja ujanja.

Sisi Wana Makanya tunapendana mno,
Kuna ajali ilitokea nikiwa kule. Ilitokea pale Makanya karibu na stand fuso iligongana na gari dogo. Fuso iliumia sana. Lakini siku 2 kabla kuna mzee alikuwa keshatoa onyo (alitapeliwa na dereva asiyemfahamu) Akasema huyo dereva hatakatiza hapa makanya na nataka asife bali avunjike mikono na miguu tu. Na niishuhudie hiyo ajali.

Wakati ajali husika inatokea mzee alikuwa pale stand na dereva alivunjika mikono na miguu yote.
 
Hakuna uchawi hapo, huko same, ugweno ni sehemu ya milima sana, hii gari ilipaki kwenye mnara wa simu, minara ya simu kwa meneo haya, ipo kwenye milima, nyumba unaziona kwa chini, gari iliserereka tu, kwa Mujibu wa polisi, dereva yupo ndani.

Kwa wale ambao wmeishapita njia ya kwenda Tunduma, ukitoka Songwe/vwawa,Kuna sehemu inaitwa Anseketwa,mkono wa kushoto juu, kuna mlima, na juu Kuna mnara wa simu,nyumba za watu zipo chini.

Au kama umewahi Kufika Chenene Dodoma, njia ya kwenda Kondoa, au Kibaya Hill Kiteto, ni mazingira kama hayo.
Nimejaribu kuwapa picha ya huko lakini naona sijaeleweka na wengi. Binafsi sijaihusisha moja kwa moja na ushirikina, nilichofanya ni kutoa picha pana ya kinachoendelea kwenye hiyo milima.
 
Nawaambiaha watu huko upareni ndio kuna magwiji wa kila sekta ya ulozi tena kubwa ulilosema ni ushirikiano wa waganga...yani kama mganga Ilo tatizo yeye sio master, basi anampigia mkali wa hio sector na unasolviwa tatizo faster
Wana vi note wanaandikiana vina code na saini zao. Wana ushirikiano wa ajabu sijapata kuona
 
Kwa mazingira hayo, mbona ni tukio la kawaida. Huyo dada shuhuda anasema gari lilitembea bila dereva/ kuendeshwa ni uchawi, kama handbrake/ emergency brake imeachia au haikuwa engaged na kuna mtelemko na nyuma ipo bondeni ajabu ni nini hapo?
Jaribu kuiele we a hiyo picha vyema, jaribu kumuelewa na mtaalamuna wa vilinge afrika mashariki na kati hahahahaha
1. Gari kuachwa na mmiliki?
2. Uimara gani wa nyumba ukilinganisha na uzito wa gari
3. Inawezekana kuna mtu anapewa onyo alizungua
 
Back
Top Bottom