Huwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi! Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA
Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani..Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi
Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video.! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika.. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani
Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu.. Nilienda kwenye mishe zangu personal
Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE..Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake
Kule mahakama ya haki ni ushirikina!!! hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana..!!! Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia...Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu
Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae...Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta..Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako
Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha..Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule
Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi...huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima..!
Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba , shughuli za kiserikali na miradi
Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako.. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana
Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa
Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!
Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya
Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je dereva wake kakimbilia wapi?
Je wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?
Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio..Na nikienda huko nitawaletea mrejesho
View attachment 1828122