Janja weed
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 3,000
- 5,606
Mkuu Mshana yani hata wewe unaamini hii kitu , mbona ni scenario ya kawaida tuu, mosi barabara ikiwa inapita juu na nyumba ziko chini possibility ya kuanguka ni kubwa sana huko upareni ni milimani tena barabara zake ni za ajabu sana , kuna baadhi ya maeneo ya marangu huko moshi na yenyewe yako hivyo barabara zimechongwa milimani kona nyiiingi ili kuwezesha magari kupita , sasa ikitokea bahatimbaya gari ikafeli na barabara zenyewe za vumbi lazima ikite kwenye mapaa tu. Hakuna ushirikina wowote hapo ni wewe tu mkuu mshana , kwakua na wewe ulienda kwa masuala hayo kwa siku tatu zote lazima tu ungeamini hivyo.