Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Ila mshana umeongeza chumvi kuhusu huko ulipopasema. Japo kweli ushirikina upo
Kumbe Mrs Bishanga umeolewa na wahaya ila ni mpare[emoji23][emoji23][emoji23], huyu ndugu yetu kaongeza chumvi...hivi Mshana Jr we sí mpare wa lushoto kweli[emoji39][emoji39]
 
Kumbe Mrs Bishanga umeolewa na wahaya ila ni mpare[emoji23][emoji23][emoji23], huyu ndugu yetu kaongeza chumvi...hivi Mshana Jr we sí mpare wa lushoto kweli[emoji39][emoji39]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Lushoto kuna Wasambaa hakuna wapare wa Lushoto... Ningesimulia kila kitu kwa siku 3 nilizokaa kijijini Tae si mngesema nimeweka vinegar kabisa....!!?[emoji23]
Kuna watu tayari leo wanaenda huko ikiwapendeza nao wataleta mrejesho wao...
 
Kwa jinsi supervisor wa shemeji anavyoiburuza kampuni nzima mpaka bosi wa kampuni mimi nakuambia ulozi upo. Yaani HR akiambiwa anakuambia huyo Supervisor ndiyo alivyo hivyo hivyo na bosi hua hana cha kumfanya.

Sasa nikamshauri shemeji, ajiendeleze kielimu kidogo kisha afanye namna apate nafasi ya juu ofisini ambayo haitamtaka asimamiwe na supervisor.

Akanijibu "Kua bosi bongo miyeyusho, kwani na mi si nitakua nasimamia watu nitakua bosi wao? Sasa ninaowasimamia waniloge ili niwapende, nyumbani dada yako aniloge nimpende, mchepuko uniloge ili nizidi kutoa hela, bosi aniloge nisifikirie kuacha kazi, hapo mgahawani nilogwe nisihame mgahawa mwisho niwe zombi kwa mchanganyiko wa madawa. Nitakomaa na huyu mwana hadi kieleweke"
Kuna bosi wangu wa zamani pia mpare wa uko uko aisee hatari yaani halipi mishahara kwa wakati anaweza akasafiri miezi 3 watu wanapewa posho akija anaitisha kikao anaanza polojo watu wanatulia wanamsikiliza na hawasemi chochote.

Huyu jamaa Mke wake ndiye mhasibu wa kampuni na pesa zote na signatory ni yeye.

Yaani niliondoka na kukimbia nikiwa nadai laki 9 yaani alitaka kuwa niwe msukule wa taasisi ambayo yeye ni CEO

Staff inafanya kazi kweli cha ajabu halipi mishahara yaani akija ni story na watu wote wamefanywe mazombi wanamsikiliza tu.

Hawa watu nimewaogopa kufanya nao kazi aisee imagine kampun inayoingiza netprofit milion 200+ per year inashindwa kulipa mishahara.

Kuna wafanyakazi pale wana miaka 10 ila wanalia njaa ya pesa.

Kuna jamaa alimfokea ili amlipe alivyokuwa anaondoka baada ya kulipwa alipata ajali na kufa kabla ajafika kwao

Hii ndio ilinifanya Mimi nikimbie mpaka niache laki 9 hizi kazi hizi.


Nasikia alikuwa akifanya matambiko ya chakula kila akirudi kutoka safari maana alipenda kila akirudi anachinja mbuzi kwa ajiri ya staff yake.. Ukila tu tayari unakuwa mzee wa ndio
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Lushoto kuna Wasambaa hakuna wapare wa Lushoto... Ningesimulia kila kitu kwa siku 3 nilizokaa kijijini Tae si mngesema nimeweka vinegar kabisa....!!?[emoji23]
Kuna watu tayari leo wanaenda huko ikiwapendeza nao wataleta mrejesho wao...
Lushoto kuna wapare kibao, yaani wapare wa kutosha... kuanzia hapa mombo kupandisha huko juu ni wamejaa wa kutosha.
 
Lushoto kuna wapare kibao, yaani wapare wa kutosha... kuanzia hapa mombo kupandisha huko juu ni wamejaa wa kutosha.
Nimekulia Lushoto ... Hao wote ni wahamiaji ...kuna wambugu lakini hawa si wapare kamili wana usomali 50%
 
Huwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA.

Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani. Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi.

Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani.

Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu. Nilienda kwenye mishe zangu personal. Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE. Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake.

Kule mahakama ya haki ni ushirikina hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana. Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia. Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu.

Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae. Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta. Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako.

Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha. Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule. Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima.

Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba, shughuli za kiserikali na miradi.

Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana. Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa.

Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!

Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya. Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je, dereva wake kakimbilia wapi?
Je, wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?

Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio. Na nikienda huko nitawaletea mrejesho.

View attachment 1828122
Yaani sisi wazee wa Swax (Sumbawanga) huwa tunavishwa hili joho la kupiga ndele na chekeche as if mahala pengine hakuna kbsa mambo ya kupiga gia hewani ,kumbe hata kaskazini kuna mambo ya kutisha namna hii?
Tunaonewa Sana asee
 
Yaani sisi wazee wa Swax (Sumbawanga) huwa tunavishwa hili joho la kupiga ndele na chekeche as if mahala pengine hakuna kbsa mambo ya kupiga gia hewani ,kumbe hata kaskazini kuna mambo ya kutisha namna hii?
Tunaonewa Sana asee
[emoji3][emoji3][emoji3]Kilinge changu kimechukuliwa na mtu wa huko kwenyu Sumbawanga
 
[emoji2][emoji2][emoji2]muache babu yangu...
Ni rafiki yangu sana ujue.. Kule shamba kwakwe vijana hata wakute mua umeng'oka wenyewe hawagusi[emoji3][emoji3][emoji3] wala ndizi zake hata kima hasogei[emoji23][emoji848][emoji2815][emoji2827]
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Lushoto kuna Wasambaa hakuna wapare wa Lushoto... Ningesimulia kila kitu kwa siku 3 nilizokaa kijijini Tae si mngesema nimeweka vinegar kabisa....!!?[emoji23]
Kuna watu tayari leo wanaenda huko ikiwapendeza nao wataleta mrejesho wao...
Unataka kusema wale wanaoongea kipare kuanzia Mtae, Mnadani, Sigi na kuteremka mpaka Mlalo Ni wambugu?
 
Kwanin Wanawake wakishana Wanawaka moto usiku
Neno kushana maana yake Ni ku unda au ku mould au kutengeneza. Ukoo wa washana ndio walikua wanatengeneza au kufua vyuma na kutengeneza zana Kama panga, jembe n.k.
Utaalamu huu ulihusishwa na uchawi na ilikua Siri yao tu, yaani hawakuruhusu ukoo mwingine ujue kuunda zana ili ku protect hiyo trade yao.
Ndio maana ukoo unaoogopwa kwa uchawi upareni Ni washana. Zamani watu wa Koo nyingine waliepuka kuoa washana kwa sababu za kishirikina. Hata Sasa wanaojielewa hawaoi washana.
Mshana Jr correct me kabla sijaanza kutaja Mambo ya milango
 
Back
Top Bottom