Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Neno kushana maana yake Ni ku unda au ku mould au kutengeneza. Ukoo wa washana ndio walikua wanatengeneza au kufua vyuma na kutengeneza zana Kama panga, jembe n.k.
Utaalamu huu ulihusishwa na uchawi na ilikua Siri yao tu, yaani hawakuruhusu ukoo mwingine ujue kuunda zana ili ku protect hiyo trade yao.
Ndio maana ukoo unaoogopwa kwa uchawi upareni Ni washana. Zamani watu wa Koo nyingine waliepuka kuoa washana kwa sababu za kishirikina. Hata Sasa wanaojielewa hawaoi washana.
Mshana Jr correct me kabla sijaanza kutaja Mambo ya milango
Kuna jamii ya washana ndo walikua wnafua chuma, sababu Kuna Koo nyingi za kishana majina yanafanana lakin sio ndugu kabisa
 
Kule ni full package
Mkuu hivi ni kweli uchawi o.g wa Tanganyika ya enzi za kichifu na makabila yetu umehifadhiwa Ujerumani?!Maana nilisikia mtu fulani mkuu alipigwa dude la kimwera kule Lindi,wakaitwa kila aina ya waganga hapa bongo wakashindwa lakini jamaa akaenda kuponea ujerumani kwa kutumia uchawi wa zamani wa kimwera uliohifadhiwa huko ndio ukaweza kutengua ile teknolojia ya sasa hivi haikufua dafu ikakausha😁😆
 
Umenikumbusha wambugu, Ila wambugu ni wapare wa asili kabisa, ni kama washana, wachome, wabwambo etc. Nadhani hata kipare hujui wewe...oshie iwe mshambaa[emoji23][emoji23][emoji23]
Hao wambugu wanapatikana maeneo gani ya huko?Suji,Kihurio,au?
 
Neno kushana maana yake Ni ku unda au ku mould au kutengeneza. Ukoo wa washana ndio walikua wanatengeneza au kufua vyuma na kutengeneza zana Kama panga, jembe n.k.
Utaalamu huu ulihusishwa na uchawi na ilikua Siri yao tu, yaani hawakuruhusu ukoo mwingine ujue kuunda zana ili ku protect hiyo trade yao.
Ndio maana ukoo unaoogopwa kwa uchawi upareni Ni washana. Zamani watu wa Koo nyingine waliepuka kuoa washana kwa sababu za kishirikina. Hata Sasa wanaojielewa hawaoi washana.
Mshana Jr correct me kabla sijaanza kutaja Mambo ya milango
Ndio maana ukoo unaoogopwa kwa uchawi upareni Ni washana. Zamani watu wa Koo nyingine waliepuka kuoa washana kwa sababu za kishirikina. Hata Sasa wanaojielewa hawaoi washana.[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Umenikumbusha wambugu, Ila wambugu ni wapare wa asili kabisa, ni kama washana, wachome, wabwambo etc. Nadhani hata kipare hujui wewe...oshie iwe mshambaa[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]oshie iwe mshambaa!!! Umechapia hapa.. Ulipaswa kusema Osie iwe u mshambaa?
 
Mkuu hivi ni kweli uchawi o.g wa Tanganyika ya enzi za kichifu na makabila yetu umehifadhiwa Ujerumani?!Maana nilisikia mtu fulani mkuu alipigwa dude la kimwera kule Lindi,wakaitwa kila aina ya waganga hapa bongo wakashindwa lakini jamaa akaenda kuponea ujerumani kwa kutumia uchawi wa zamani wa kimwera uliohifadhiwa huko ndio ukaweza kutengua ile teknolojia ya sasa hivi haikufua dafu ikakausha[emoji16][emoji38]
Wajerumani waluondoka na hazina kubwa sana ... Yaani hata haya mambo ya kishirikina walibeba yote
 
🤣🤣🤣🤣
Hao Wapare hawajafikia "Mabeberu"......wacha tu watutawale...


1624747774293.png

1624747814537.png

1624747844886.png

1624747882426.png

1624747941314.png
 
Me nimezaliwa same. .thou me ni mchaga ...Ila kwa uchawi tuu hawa jamaa wako vizuri mnoo adse ...nlikulia kijiji kimoja kinaitwa "Mahuu" huko ni balaa
 
Nipo huku muda huu mkuu yaani full uchawi mpaka naogopa kulala leo,nimeingia Jana Liwale baada ya kutembea zaidi ya saa 10 kutoka Nangulukuru hadi Liwale,huwezi amini kiongozi Jana nilipanda gari pale Nangulukuru saa 8 mchana lkn ajabu tukaingia Liwale mjini saa 7 usiku[emoji15][emoji15] asubuhi nikajihimu kwenda Ngende gharama ya pikipiki go and return ni zaidi ya sh 35000[emoji15]nipo huku muda huu wakuu wangu niombeeni nirudi salama
Nipe namba ya huyo fundi pm, uchaguzi ukifika nimchape mtu
 
Kwa jinsi supervisor wa shemeji anavyoiburuza kampuni nzima mpaka bosi wa kampuni mimi nakuambia ulozi upo. Yaani HR akiambiwa anakuambia huyo Supervisor ndiyo alivyo hivyo hivyo na bosi hua hana cha kumfanya.

Sasa nikamshauri shemeji, ajiendeleze kielimu kidogo kisha afanye namna apate nafasi ya juu ofisini ambayo haitamtaka asimamiwe na supervisor.

Akanijibu "Kua bosi bongo miyeyusho, kwani na mi si nitakua nasimamia watu nitakua bosi wao? Sasa ninaowasimamia waniloge ili niwapende, nyumbani dada yako aniloge nimpende, mchepuko uniloge ili nizidi kutoa hela, bosi aniloge nisifikirie kuacha kazi, hapo mgahawani nilogwe nisihame mgahawa mwisho niwe zombi kwa mchanganyiko wa madawa. Nitakomaa na huyu mwana hadi kieleweke"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kimeumanaaah.
 
Halafu tena gari yenyewe ni Toyota Stout ya mwaka 1986, ambazo zimebaki Kilimanjaro tu. Miaka ya nyuma niliitafuta sana mpaka nikatoa Tangazo hapa bila mafanikio yoyote.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lol
 
Huwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA.

Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani. Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi.

Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani.

Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu. Nilienda kwenye mishe zangu personal. Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE. Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake.

Kule mahakama ya haki ni ushirikina hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana. Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia. Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu.

Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae. Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta. Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako.

Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha. Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule. Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima.

Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba, shughuli za kiserikali na miradi.

Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana. Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa.

Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!

Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya. Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je, dereva wake kakimbilia wapi?
Je, wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?

Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio. Na nikienda huko nitawaletea mrejesho.

View attachment 1828122
Aiseee....
 
Back
Top Bottom