Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kuna ajali ilitokea nikiwa kule.. Ilitokea pale Makanya karibu na stand fuso iligongana na gari dogo.. Fuso iliumia sana.. Lakini siku 2 kabla kuna mzee alikuwa keshatoa onyo (alitapeliwa na dereva asiyemfahamu) Akasema huyo dereva hatakatiza hapa makanya na nataka asife bali avunjike mikono na miguu tu.. Na niishuhudie hiyo ajali
Wakati ajali husika inatokea mzee alikuwa pale stand na dereva alivunjika mikono na miguu yote
Mwenyewe sijaona huo uchawi aiseeKwa mazingira hayo, mbona ni tukio la kawaida. Huyo dada shuhuda anasema gari lilitembea bila dereva/ kuendeshwa ni uchawi, kama handbrake/ emergency brake imeachia au haikuwa engaged na kuna mtelemko na nyuma ipo bondeni ajabu ni nini hapo?
Mkuu hii ni Land Cruiser Pick Up hao NEWL ndio wanazotumia kusambaza mafuta kwenye minara, siku hizi wanatumia na Nissan Hardbody pia.Halafu tena gari yenyewe ni Toyota Stout ya mwaka 1986, ambazo zimebaki Kilimanjaro tu. Miaka ya nyuma niliitafuta sana mpaka nikatoa Tangazo hapa bila mafanikio yoyote.
Nikitaka kufika TAE kwa kutokea Arusha napanda gari za kwenda wapi?Haya ndio mazingira ya Tae. Ni milimani kwenye baridi kali lakini kukiwa na greenish nzuri na vijito vinavyotiririsha maji meupe masafi.. Hizi picha niliwahi kutupia hapa JF kule SELFIKA[emoji2]View attachment 1828124View attachment 1828125View attachment 1828126
Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya
Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je dereva wake kakimbilia wapi?
Je wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?
Nilipoona tu reply yako mtafiti nikajua utashusha data za kutosha sana.Nimezaliwa Makanya
Nimekulia na Kusomea Makanya kuanzia chekechea, shule ya msingi mpaka Kidato cha nne,
Niliondoka Makanya nilipofaulu Kidato cha nne.
Makanya ndio kwetu, Makanya ndio watu wangu, nami ni mtoto wao.
Hayo unayosema yapo Kwa kiasi,
Makanya Ushirikina na Uchawi upo na unaathari labda Kwa wageni wasio wazawa.
Makanya inamchanganyiko wa Makabila kutokana na kilimo cha zao la Mkonge.
Wenyeji wengi ni Wapare,
Lakini pia kuna
Wamasai, wasambaa, Wachaga kidogo, Warundi, Wanyambo, Wasukuma, NK.
Pia wapo wanyiramba.
Uchawi Kwa kiasi kikubwa unapatikana Milimani ambapo ipo Mashariki mwa kamji Ka Makanya.
Wasambaa na watu wa Tanga wameongeza nafasi ya UCHAWI katika mji huo wenye ukame.
Makanya ndio Makao makuu ya Biashara ya Mirungi Afrika Mashariki.
Mirungi hiyo itokayo Milimani hasa Tae, Suji, Parane na Chime ina ladha inayopendwa na watumiaji ukilinganisha na Mirungi ya Kenya na Somalia.
Uchawi pia unaisaidia Biashara hiyo ya Mirungi kuendelea kuexist mbali na Rushwa.
Polisi Wanoko wasiotaka Rushwa hukipata cha mtema kuni wakifuatilia Wauza Mirungi huko Milimani.
Hivyo hujikuta wanapata madhara na kuamua kuacha au huamishwa kabisa kituo cha kazi.
Kipindi nakua, baadhi ya ajali za barabarani zilihusishwa na Uchawi na Ushirikina.
Makanya na Hedaru ni moja ya miji Maarufu wilayani Same na pia inaongoza Kwa ujanja ujanja.
Sisi Wana Makanya tunapendana mno,
Nenda Kasulu Nyamnyusi UtajiridhishaKuna vitu napata shida sana kuvielewa au kuviamini.
Na maelezo yake haya hapaHuwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi! Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA
Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani..Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi
Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video.! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika.. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani
Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu.. Nilienda kwenye mishe zangu personal
Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE..Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake
Kule mahakama ya haki ni ushirikina!!! hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana..!!! Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia...Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu
Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae...Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta..Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako
Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha..Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule
Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi...huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima..!
Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba , shughuli za kiserikali na miradi
Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako.. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana
Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa
Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!
Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya
Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je dereva wake kakimbilia wapi?
Je wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?
Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio..Na nikienda huko nitawaletea mrejeshoView attachment 1828122
Mkuu kweli huko ni noma tembea uone mengiHii ndio video husika ya tukio zima.. Dereva kama angepatikana angetupa insights za nini kilitokea dakika zile za mwisho ... Je alienda chobingo? Je ajali ilimtaka yeye? Je dereva naye yuko fit?
View attachment 1828123
Vipi kinga ya mwili na mazindiko mkuu, wako fiti pia?Haya ndio mazingira ya Tae. Ni milimani kwenye baridi kali lakini kukiwa na greenish nzuri na vijito vinavyotiririsha maji meupe masafi.. Hizi picha niliwahi kutupia hapa JF kule SELFIKA[emoji2]View attachment 1828124View attachment 1828125View attachment 1828126
Nenda Kasulu Nyamnyusi Utajiridhisha
Hayo Mambo Ni Magumu Ila Yapo Sana