Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Jaribu kuiele we a hiyo picha vyema, jaribu kumuelewa na mtaalamuna wa vilinge afrika mashariki na kati hahahahaha
1. Gari kuachwa na mmiliki?
2. Uimara gani wa nyumba ukilinganisha na uzito wa gari
3. Inawezekana kuna mtu anapewa onyo alizungua
Sasa Bakari Msangi ameishaenda kumalizana na Sabaya huko milimani.. tusubiri matokeo tu. Hata Sabaya akiachiwa na mahakama adhabu yake iko palepale kutoka kwa wazee wa kipare
 
Kwahiyo Mimi ni dada wa mama yako leo?? Mm sio dada tuheshimiane naweza kuoa ukoo wenu wote Kwa mahali ndogo sana

Sema unaweza olewa na ukoo wetu wote kwa kutolewa mahari siyo MAHALI kilaza wewe. Huko ulikoolewa sasa umelipiwa sh. Ngapi mpaka unatetea hivyo? Unaumia sana au ni ID nyingine? 😁😁😁😁😁
 
uchawi upo zaidi ugweno,usangi na lomwe..
muulize rais wa awamu ya 2.

nadhani hata kwenye kitabu chake hakusalimia na hataki kukumbuka!

aliporudi pwani akatafuta wataalam waliobobea akawatuma kule wakasafishe vijiji vya kishirikina!

ilitokea kasheshe kubwa sana wakati huo ikawa ndio habari ya mjini kipindi hicho!

kuna mzee ana mabasi yatokayo moshi-usangi (sitamtaja)huyo mzee ni fire.
ametesa sana matrafiki waliokuwa wanasumbua basi zake.

kuna trafik alizoea kupiga mkono basi zake hadi leo mkono umebakia kauunyosha juu.hapana chezea huyo mzee!

hiyo ni ruti yake na kila ijumaa usafiri ni bure ole wako konda uchkue nauli unajikuta secret parts hazipo...!
Kilenga hayupo usangi, yupo juu ya vijiji vya mwembe huko juu. Kama unaenda msitu wa shengena
 
Mimi naishi upareni huku hakuna kudhulimiana wala wizi wa kijinga wana uchawi unaitwa " MMA" ni hatari aisee unasafisa ukoo mzima alafu aliyefanya tukio anakua wa mwisho kufa !!!
Hawa jamaa ni shida!!! Nawaogopa sana sana hata mademu akikuendea kwa babu utasahau familia yako!!!
Huku upareni kwa wafugaji hata ngombe wakiibiwa kinachofanyika ni kwamba aliyeibiwa ngombe wakati wanawafatilia ngombe wanachokifanya ni kuokota nyayo za hao ng'ombe (udongo) kisha wanafunga hapo Ngombe walioibiwa wanagoma kwenda wanakoelekezwa na wezi hapo wakati huo wafalikia nyayo wanasogelea
 
Wengi wao Ila sio wote.

Chunguza watu wote wanaotuhumiwa Uchawi Wana sifa zifuatazo;

1. Waadilifu
2. Sio walevi
3. Sio watu wa kutia aibu
4. Wanakijistiri yaani wanavaa nguo za adabu.
5. Wana lugha nzuri.

Kwa ujumla Wenye tuhuma za uchawi sifa zao kitabia ni zile zile zinazofanana na Wacha Mungu.

Sema Washirikina wao ndio Wanazingua maana ndio wahuni
Duh!
 
Tae Kuna kipindi mkuu wa wilaya ya Same wa zamani anaitwa Kapufi kama sikosei,alijifanya mjuaji anataka kupambana na mirungi. Alichukua askari akaongozana nao kwenda kukata miti ya mirungi yote. Kufika hapo kijijini mara hawaoni nyumba wala mashamba... wakati wa kurudi sasa wakapotea. Waliteseka hao mpaka wakakoma..Hawakuthubutu kurudi tena
Kuna mdau kasema nimetia chumvi sana ushirikina wa Tae, wakati nilichosimulia ni tone tuu
 
uchawi upo zaidi ugweno,usangi na lomwe..
muulize rais wa awamu ya 2.

nadhani hata kwenye kitabu chake hakusalimia na hataki kukumbuka!

aliporudi pwani akatafuta wataalam waliobobea akawatuma kule wakasafishe vijiji vya kishirikina!

ilitokea kasheshe kubwa sana wakati huo ikawa ndio habari ya mjini kipindi hicho!

kuna mzee ana mabasi yatokayo moshi-usangi (sitamtaja)huyo mzee ni fire.
ametesa sana matrafiki waliokuwa wanasumbua basi zake.

kuna trafik alizoea kupiga mkono basi zake hadi leo mkono umebakia kauunyosha juu.hapana chezea huyo mzee!

hiyo ni ruti yake na kila ijumaa usafiri ni bure ole wako konda uchkue nauli unajikuta secret parts hazipo...!
Mwinyi kilimkuta nini huko upareni? Nadhani hao wazee wa pwani hawakuamini walichokutana nacho huko. Wapare ni kiboko hawapishani sana na waha wa kigoma
 
Hahahaa wazee wa cbumaulete na kuagiza kuku nakaniki
Jamaa wanapata vitambi kwa kuku wa kuagiza, wanaongezea tu lete mweupe, au mweusi ili usimshtukie, ila kuku wako palepale.
 
Huwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA.

Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani. Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi.

Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani.

Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu. Nilienda kwenye mishe zangu personal. Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE. Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake.

Kule mahakama ya haki ni ushirikina hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana. Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia. Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu.

Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae. Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta. Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako.

Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha. Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule. Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima.

Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba, shughuli za kiserikali na miradi.

Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana. Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa.

Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!

Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya. Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je, dereva wake kakimbilia wapi?
Je, wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?

Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio. Na nikienda huko nitawaletea mrejesho.

View attachment 1828122
Duh
 
Hao waganga wa huko Upareni ndio nawataka wanitengeneze, maana naona kuna mtu keshanizowea sana, Mshana Jr mtani wangu hebu nipe connection niende niko serious kabisa
 
Back
Top Bottom