Uchawi upo duniani na una nguvu kubwa,lakini aliyeumba vyote chini ya jua ndiye mwenye nguvu zaidi

Uchawi upo duniani na una nguvu kubwa,lakini aliyeumba vyote chini ya jua ndiye mwenye nguvu zaidi

Baba Ndubwi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
1,223
Reaction score
1,992
Wakuu naimani kwa pamoja tunaendelea kujikinga sisi na familia zetu dhidi ya COVID-19.Ni jukumu letu sote kujikinga,kuwakinga na kuwaelimisha wengine jinsi ya kujikinga.

Moja kati ya visa vingi ambavyo nimewahi kukumbana navyo katika maisha ya kuteswa na kutaabishwa na wachawi kwa miaka zaidi ya 20 ktk tasnia hii ya wazee wa nguvu za giza/wachawi/wanga au wazee wa kuloga/kuruka usiku ni hili;

Yakupasa kufahamu ya kwamba;Mchawi akitaka kukuua/kukuharibia maisha muda mwingine hutengeneza mbinu za kupoteza ushahidi(haswa wachawi ndugu,kama wanatoka kwenye ukoo au familia) kiasi kwamba hata watu au wanandugu hawawezi kuhisi kama umethulumiwa haki yako ya kuishi au mafanikio.

Yatatengenezwa mazingira na mwisho wa siku itaonekana ulikuwa ni uzembe wako ama bahati mbaya wewe kuharibikiwa maisha ama kupoteza maisha.

Mwaka 2018 nilikwenda Morogoro kijiji kinaitwa kisama,kama unakwenda magogoni yaani njia ya kwenda ngerengere.

Ni pale ukifika ubena kama unatokea dar basi unakula kona kushoto.

Huko nilikwenda kwa ajili ya biashara ya mbao baada ya kualikwa na jamaa yangu tena kiroho safi kabisaa.

Usafiri wa kwenda huko kijiji cha Chanyumbu kata ya Kisama ni wa shida balaa,gari ni coaster au daladala za dar zinazozamiaga ruti na ni moja tuu kwa siku, na kipindi cha masika hakuna usafiri tena wa gari zaidi ya pikipiki na sio nyingi maana wengi hufungia ndani toyo zao.

Nilifika kijijini Kisama;Kazi ilianza,ni mwendo wa masaa 3 kwa mguu kwenda chaka,msituni yaani huko ni mwendo wa kupiga kambi chaka,full mijoka na mifisi kufukuzia ng'ombe za wamang'ati,mjengo ni kusimamisha miti kisha kuweka turubai tuu juu basi pembeni no ukuta na mvua ikianza hapo ni mtafutanoo,ni mwendo wa kulala wima kama mchongoma,mkeshaa(nadhani wavunaji wa mbao,wazee wa chain saw watakuwa wananielewa hapo).

Kiukweli walipanga kunimaliza kabisa hawa wachawi;Porini mimi nilikuwa msimamizi wa ile chain sawa jamaangu yeye akaondoka akaniachia kwa makubaliano fulani.

Kila mara watu niliokuwa nao porini walikuwa wakinieleza vile nimekuwa nikiota usiku,napiga makelele na kutamka maneno yanayooashiria niko kwenye mapigano.."Niachenii,msinifungee". Moja kati ya maneno niliyowahi kuyatamka.(nilielezwa asubuhi baada ya kuamka) na ilikuwa kawaida mimi kuota ndoto hatari,za hovyo,chafu za kishetani.

Mwezi mmoja baadae sijui hata ilikuwaje tuu,siku hiyo tumetoka chaka jioni nikakuta ujumbe pale kijijini kwa mwenyeji wetu eti jamaangu anadai mashine nikabidhi,nisisimamie tena.

Nikasema sawa ila lipa kwanza madai yangu ya usimamizi duuh hapo ndipo balaa lilipoanzia,jamaa bila aibu akagoma kulipa,akadai nilizoiba zinanitosha.

Aise sijui tuu ilikuwaje mtu aloambiwa aichukue chain saw kaanza kuniropokea,ghaflaa nikabeba panga lah ni Mungu tuu lakini dhumuni ilikuwa nimkate halafu afe/adhurike me nipotezwe jela.Hata mwenyeji wetu alishangaa sanaa kuniona nimepagawa na kuleta balaa kubwa,watu kibaoo.

Mgogoro ule uliisha baada ya kulipwa nusu ya pesa tu na iliyobakia mpaka leo sijalipwa.

Baada ya wiki nikaamua siondoki, naendelea kupambana chaka.Nikazungumza na jamaa mwengine alikuwa na chain saw,nikanunua mafuta na chakula tukazama chaka(nikawa boss na mimi)akanichania mbao,zikasombwa kuletwa kijijini ili wanunuzi toka Chalinze/Magindu waje kuzinunua.Sasa hapo ndipo nilipoiona dunia chungu.

Kila aliyekuaja alikuwa akiangalia anasema mbao super kweli nitakuja,lakini cha kushangaza kwesho yake haji mtu utasikia tuu alishapita na mzigo kachukulia kwingine.

Nilikaa wiki 3 mzigo hauuziki,Tumboni kuna dude lilikuwaga linafanya kama linafinya,maumivu makalii na hali hii ilikuwa inajitokeza haswa nikiwa nafanya inshu za kusaka pesa.

Na lilikuwa likishika hili dude hapo hakuna kitu kitafanikiwa,yaani yatatokea mazingira flani tuu inshu itavurugika tena kwa ugomvi au mimi kuondoka tuu.

Wiki ya tatu baadae nilikata tamaa,sijauza mbao hata moja.Jamaangu kutoka jiji fulani akanambia niende tuu kwanza nikapumzike ili nijipange upya(namshukuru sanaa sana huyu jamaa).

Alinitumia nauli,saa moja usiku niliondoka kwa mguu kuelekea chalinze.Usiku kucha nilichanja mbuga umbali wa zaidi ya kilometa 75, nikipitia njia ya seregeti A na B.Nilifika chalinze mishale ya saa tano asubuhi.

Nikadaka ndinga mpaka jijini.

Cha ajabu nlivyofika jijini kesho yake mtu niliyemuachia mzigo wa mbao kule kijijini akawa hapatikani kwenye simu,kaja kupatikana siku 3 baadae.Ananambia siku nimeondoka tuu kesho yake mzigo ukaunuliwa woote ila simu ndo ilimuharibikia.

Pia akadai mtoto wake usiku huo alishikwa na homa kali hivyo akalazimika kumega pesa ya mauzo ya mbao ili kumnusuru mtoto so atanirejeshea,nikamwambia shaka hakuna.

Daah,kumwambia anitume kilichobakia sikuamini, ni robo ya pesa nlokuwa nimewekeza kwenye ile biashara. Na hapo ndio ukawa mwisho wangu wa biashara ya mbao.

Visa vingine nitaandika kadiri nitakavyokuwa ninapata muda.
 
katika vitu cjawahi kuamini kama vipo ni USHIRIKINA au UCHAWI never...
enewei,AISIFIAYE MVUA UJUE IMEMNYEA...🚶🚶🚶
Umemalizia vyema mkuu,hakika wewe great thinker.
Ni sawa na ''kitanda usichokilalia,huwezi jua kunguni wake''
 
Sijsoma ngonjera yako ila hakuna uchawi/ushirikina/wanga zote ni story za kusadikika na zinaaminiwa sana wa wajinga.

NB: Ujinga sio tusi.
 
Aah hii nini sasa umeandika mzee?

Swala la kuota ndoto za kutisha hizo nightmare ni jambo ambalo linaelezeka bila kuweka dhana potofu (uchawi)

Kuna sababu nyingi ambazo unaweza ukakosa wateja kulingana na wewe unavyojiweka na sio kwamba uchawi

We kama umetishia kutoa uhai wa mwenzako kwa panga na watu wameona, hivi unafikiri ni mjinga gani anayeweza kuthubutu kuja kununua bidhaa kutoka kwako?

Anauhakika gani na usalama wa maisha yake endapo mtashindana bei?

Anauhakika gani na uaminifu wako kua hautamfata na panga kwenda kumteka uchukue mzigo alioununua kwako ili upate faida mara mbili?

Ni mjinga gani asiyeweza kutafsiri mambo yaani mtoni mamba kibao halafu we unamsubiri ng'ambo ukitarajia atakuja halafu akajitosa mtoni kweli?

Halafu unajichanganya sana, umesema wachawi wakifanya uchawi wao hua hawaachi ushahidi ila hapo hapo umeweka ushahidi kuonesha kua ulilogwa. Tukueleweje?
 
katika vitu cjawahi kuamini kama vipo ni USHIRIKINA au UCHAWI never...
enewei,AISIFIAYE MVUA UJUE IMEMNYEA...🚶🚶🚶
Wanaofanya uchawi wanakuchek wanakushangaa.
Wachawi hawaonekani lakini kuna WAGANGA tunaishi nao mitaani tunawaona kila siku. Wachawi na WAGANGA baba yao ni mmoja
 
Uchawi upo ika sio kwa ajili ya kila mtu. Wapo watakaozaliwa na kufa hawajasikia wala kuona uchawi.
Cc. Kiranga
 
Daa hayavmambo sijui nini yani
Kuna baadhi ya mambo yanatokea unatafuta conection na sababu za kisayansi/kimazingira hupati jibu.kama jibu halipatikani huko basi yabidi tuseme ni uchawi!!

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Aah hii nini sasa umeandika mzee?

Swala la kuota ndoto za kutisha hizo nightmare ni jambo ambalo linaelezeka bila kuweka dhana potofu (uchawi)

Kuna sababu nyingi ambazo unaweza ukakosa wateja kulingana na wewe unavyojiweka na sio kwamba uchawi

We kama umetishia kutoa uhai wa mwenzako kwa panga na watu wameona, hivi unafikiri ni mjinga gani anayeweza kuthubutu kuja kununua bidhaa kutoka kwako?

Anauhakika gani na usalama wa maisha yake endapo mtashindana bei?

Anauhakika gani na uaminifu wako kua hautamfata na panga kwenda kumteka uchukue mzigo alioununua kwako ili upate faida mara mbili?

Ni mjinga gani asiyeweza kutafsiri mambo yaani mtoni mamba kibao halafu we unamsubiri ng'ambo ukitarajia atakuja halafu akajitosa mtoni kweli?

Halafu unajichanganya sana, umesema wachawi wakifanya uchawi wao hua hawaachi ushahidi ila hapo hapo umeweka ushahidi kuonesha kua ulilogwa. Tukueleweje?
''Aah hii nini sasa umeandika mzee?''
1.Hii ni imani kama zilivyo imani nakatika masuala ya imani M/Mungu hakuweka ulazima ama sheria kali ya kiumbe alichokiumba kifuate ama kiamini kila kilichopo.
2.Katika ulimwengu wa ndoto kuna ndoto zitokazo kwa malaika na ndoto za kishetani/kichawi.
3.Huo mzigo mpaka unafika kijijini aliyekuwa anajua ni wangu ni fundi na mwenyeji wetu tuu,hivyo me kwa kuwa nilikuwa sina uzoefu bado nilimkabidhi yeye kusimamia kila kitu.
4.Watu waliona mtu akitishiwa panga katika ugomvi wa kukabidhi chain sawa,na baada ya hapo hakuna aliyejua kama bado ninachanisha mbao.(niliamua kufanya kwa siri)
5.Sikusimamia mimi mchakato wa uuzaji,nilijiweka pembeni ili kupata uzoefu kwa kuwa iikuwa ni mara ya kwanza.
6.Hofu ya kutekwa ni kweli haswa mtu akijua anafanya biashara na wewe lakini kwa bahati wateja walikuwa wakijua mimi siku zoote ni muajiriwa tuu.
7.Kiukweli kwa kipindi hicho nisingeweza kujua ni mjinga gani asiyeweza kutafsiri mambo.
8.Halafu sijajichanganya saana kwa sababu neno langu sio sheria na sio mwisho. Wewe umeelewaje mkuu??!!
 
Back
Top Bottom