Uchebe afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumshambulia Shilole

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Dar es Salaam.

Ashiraf Geuza maarufu' Uchebe' amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na kosa la kumjeruhi Zuwena Mohamed maarufu 'Shilole' na kumsababishia maumivu makali.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali, Chesensi Gavyole mbele Hakimu Mkazi Hudi Hudi, alidai kuwa Julai 6, 2020 maeneo ya Dar Estate Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa huyo alimpiga Zuwena Mohamed sehemu ya kichwa na shingoni na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana shtaka linalomkabili. Gavyole alidai kuwa upelelezi umekamika na aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Hakimu Hudi alisema dhamana ipo wazi mshtakiwa anatakiwa awe na wadhamini wawili ambao wanatakiwa kuwa na barua inayotambulika na watasaini bondi ya Sh2 milioni pamoja na mshtakiwa.

Mshtakiwa huyo alikidhi masharti ya dhamana shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 23, 2020 itakapokuja kwa ajili ya usikilizwaji wa hoja za awali.
 
Binafsi nilitarajia hili.

Nchi inayohubiri 50/ 50. Usawa kwa jinsi zote na mkutano wa Beijing ikahudhuria, dawati la jinsia vituo vya polisi hii ishu ilitakiwa ifike mahakamani.

Isipokua imechelewa kufika huko.

On another note. Abusive relationship ni two way traffic Nuh Mziwanda kwa Shilole was going through it but nobody intervened as wanaume tunagewa treatment ya tofauti even before legal institutions.

Wengi hatusapoti mtu anayepiga wanawake. Regardless if that lady is a dumbfvck, whore and whichever name you can come up with the same attitude should be shown when a man is swimming in the same water.
 
Sasa kama 50/50 kesi ipowapi maana sawasawa wote wananguvu wote hakuna dhaifu walanini wamepigana mmoja kampiga mwenzie.
 
Mbona Shilole alikuwa anampiga sana Nuhu Mziwanda? Hizi Sheria za kukandamiza wanaume zitaleta chuki na mpasuko kwenye jamii
Ni ujinga wa NUHU kutopaza sauti asaidiwe
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…