KERO Ucheleweshaji wa mikopo ya pesa za kujikimu (boom) awamu ya nne kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

KERO Ucheleweshaji wa mikopo ya pesa za kujikimu (boom) awamu ya nne kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha kikuu cha Dar es Salaam UDSM kampasi kuu ya mwalimu Nyerere Dsm.

Kwasasa kuna changamoto ambayo wanafunzi wengi tunaipotia ni ucheleweshwaji wa pesa za kujikimu (meals and accomodations) maarufu kama BOOM.

Kwa kawaida pesa hii huingia baada ya wiki nne za masomo au siku 60 ambapo ni sawa na miezi 2 kwa semester na kwa mara ya mwisho pesa hii iliingia tarehe 22/03/2025 lakini cha kushangaza mpaka wakati huu naandika haya pesa hii haijaingia ikiwa ni tarehe 26/05/2025. Na waliongiziwa ni wanafunzi wachache sana hapa chuoni.

Kitu kinachotushangaza na kutusikitisha ni kwamba hakuna taarifa yeyeote kutoka bodi ya mikopo (HESLB) kuhusiana na ucheleweshwaji huu wa pesa ya kujikimu.

Kimsingi hali za wanafunzi ni mbaya sana, uendeshaji wa maisha umekuwa mgumu, tunaziomba mamlaka husika yaani wizara ya Elimu na Bodi ya mikopo kutoa ufafanuzi na kuingilia kati suala hili kwani wanafunzi wengi wanateseka na ugumu wa maisha kwa kukosa stahiki zao kwa wakati kwani Boom ndilo linawezesha wanafunzi kujikimu wanapokuwa chuoni.

c61e55959ad24cbcaf6a4c4caed9862b.jpg

Naomba kuwasilisha, Asante.
 
Fanyeni mgomo, maandamano. tatizo lenu nyinyi wanafunzi mmejiingiza kwenye siasa si ajabu ukamkuta mwanafumzi wa chuo akimsifia mama eti mitano tena, wakati wetu hawakuthubutu kuchelewesha boom maana walijua kitakacho tokea ni moto lazima uwake, waulize wakina Ali Hapi na David Silinde hao walikuwa viongozi wa migomo na wanaharajati hapo UDSM. Boom ni haki yenu sio jambo la kuombaomba.
 
Wanawatunzia final year wapate chakuanzia maisha mtaani
 
Back
Top Bottom