A
Anonymous
Guest
Naomba kuwasilisha kero kuhusu kucheleweshwa kwa mchakato wa usajili wa hati ya nyumba ya marehemu katika Ofisi ya Usajili wa Hati, Wizara ya Ardhi.
Mimi ni msimamizi wa mirathi ya marehemu baba yangu. Nyumba hiyo ipo Kigamboni, Dar es Salaam, ina ukubwa wa SQM 1,122 na hati yake imesajiliwa katika Wizara ya Ardhi. Baada ya baba yangu kufariki, alituachia nyumba hiyo, lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kuipata hati halisi kwa kuwa hatukuwa tukiishi naye. Hata hivyo, tulifanikiwa kupata nakala ya hati hiyo.
Baada ya kufuata taratibu zote na kuandaa nyaraka zilizohitajika, maombi yaliwasilishwa Wizara ya Ardhi tarehe 08/06/2026 na mwanasheria/wakili anayetusimamia. Baadaye, Msajili alirudisha maombi kwa sababu mbili:
Marekebisho hayo yaliwasilishwa tena tarehe 15/07/2026 na mwanasheria/wakili wetu.
Hata hivyo, mpaka sasa hatujapewa majibu ya wazi kuhusu hatua ambayo faili limefikia. Tunapofuatilia, tunaambiwa bado lipo kwa Msajili na halijafanyiwa kazi.
Jambo linalotia wasiwasi ni kwamba tumeelezwa pia kuhusu uwezekano wa kutoa fedha ya hongo ili mchakato uharakishwe na hati ipatikane ndani ya muda mfupi.
Tayari tumelipa TSh 246,000 kwa Wizara ya Ardhi kupitia utaratibu rasmi wa malipo ya Serikali. Hii ni tofauti na TSh 450,000 tulizomlipa mwanasheria kwa ajili ya kuandaa nyaraka zote zilizohitajika.
Kero yangu si kukataa kulipa ada halali. Ninachohitaji ni uwazi na huduma inayotolewa kwa mujibu wa taratibu.
Naomba mamlaka husika:
Mpaka sasa, ni takribani miezi miwili tangu marekebisho ya nyaraka yawasilishwe, lakini bado hatujapata majibu yoyote ya kueleweka.
Naomba msaada na uingiliaji wa mamlaka husika. Asante.
NB: Nyaraka na namba za kumbukumbu za faili zipo, na niko tayari kuziwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya uthibitisho.

- Kulikuwa na tofauti ya jina la marehemu katika nyaraka za mahakama na cheti cha kifo, ikilinganishwa na jina lililo kwenye hati husika.
- Asilimia za hisa za warithi hazikutajwa katika Assent to Bequest.
Marekebisho hayo yaliwasilishwa tena tarehe 15/07/2026 na mwanasheria/wakili wetu.
Hata hivyo, mpaka sasa hatujapewa majibu ya wazi kuhusu hatua ambayo faili limefikia. Tunapofuatilia, tunaambiwa bado lipo kwa Msajili na halijafanyiwa kazi.
Jambo linalotia wasiwasi ni kwamba tumeelezwa pia kuhusu uwezekano wa kutoa fedha ya hongo ili mchakato uharakishwe na hati ipatikane ndani ya muda mfupi.
Tayari tumelipa TSh 246,000 kwa Wizara ya Ardhi kupitia utaratibu rasmi wa malipo ya Serikali. Hii ni tofauti na TSh 450,000 tulizomlipa mwanasheria kwa ajili ya kuandaa nyaraka zote zilizohitajika.
Kero yangu si kukataa kulipa ada halali. Ninachohitaji ni uwazi na huduma inayotolewa kwa mujibu wa taratibu.
Naomba mamlaka husika:
- Ichunguze hatua ambayo faili letu limefikia.
- Itueleze kama kuna nyaraka au malipo yoyote rasmi yaliyobaki.
- Itusaidie kufahamu kwa nini mchakato umechukua muda mrefu bila majibu ya wazi.
- Iweke wazi kama kuna utaratibu rasmi wa kuharakisha huduma na gharama zake.
- Ihakikishe faili linashughulikiwa kwa haki bila mwananchi kulazimika kutoa fedha zisizoeleweka ili kupata huduma.
- Itoe muda maalum ili tujue ni lini mchakato huo utakamilika.