A
Anonymous
Guest
Mnamo tarehe 4 Juni 2026, Katibu Mkuu wa TAMISEMI alitoa barua iliyoonesha kiasi cha fedha zilizotolewa kwa ajili ya malipo ya posho za kujikimu na nauli kwa watumishi wapya wa afya walioajiriwa kati ya Januari 2025 na Aprili 2026.
Katika barua hiyo, Wakurugenzi wa Halmashauri walitakiwa kuthibitisha kupokea fedha hizo na kuwasilisha taarifa ya watumishi waliolipwa posho za kujikimu na nauli ifikapo tarehe 15 Juni 2026.
Hata hivyo, hadi leo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale haijatoa taarifa yoyote kuhusu utekelezaji wa maelekezo hayo. Sisi watumishi wapya bado hatujapokea stahiki zetu na tunaelekea kuanza mwaka mpya wa fedha bila kufahamu hatima ya fedha zetu.
Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kutoa ufafanuzi pamoja na kuhakikisha watumishi wote wanaostahili wanalipwa haki zao kwa wakati.