Uchimbaji Madini katika Mbuga zetu Ufikiriwe mara mbili kabla ya hatua kuchukuliwa

Uchimbaji Madini katika Mbuga zetu Ufikiriwe mara mbili kabla ya hatua kuchukuliwa

Kwako Mhe. Rais,

Mhe. Rais wetu mpendwa, Suluhu Hassan, Nakupongeza kwa jinsi unavyo tujali watanzania, na roho yako ya upendo, kama ulivyosema unatumia maneno ya mama. Siku zote mama uwa na lugha ya upole na sikivu lakini mama ni nguzo kubwa ya Familia.

Katika hotuba yako ulitoa agizo kuwa madini yaliyopo mbugani yachimbwe. Ukadai kuwa wanyama hawali madini kama chakula chao hivyo madini hayo yachimbwe. kivyovyote mnataka kumpa mwekezaji.

Rais wangu kipenzi, naomba tusichimbe madini yetu hasa haya ya mbugani kwa wakati huu. Hatuhitaji kumaliza kila madini yaliyo chini ya ardhi. Nimejiuliza sana, ni kwanini Mungu haya madini aliyaweka mbugani ambako wanyama wanaishi?

Je, huko kwingine kuliko na madini yamekwisha? Hadi tuanze kuchimba haya madini yaliyoko mbugani?


Kipindi cha Nyerere alizuia kuchimbwa madini, akasema, madini hayaozi yakatunzwa kwa kizazi kijacho. Pale watanzania watakapokuwa na utaalamu wa kuchimba. Hivyo migodi mikubwa ilifungwa. Nakumbuka baadhi ya maeneo yaliyokuwa na machimbo aliweka kambi za jeshi. Mfano Kiabakari, na maeneo ya kwenda Mugumu, na kadhalika. Kwanini alifanya hivi? Alitaka yasichimbwe.

Mhe. Rais, kuanza kuchimba madini katika mbuga zetu, moja ni uhatarishi wa asili ya mbuga zetu, na ekolojia. Wanyama hawapendi kubugudhiwa. Uchimbaji, hutumia njia nyingi na hasa milipuko. Hii si nzuri kwa wanyama na italeta sintofahamu kwa wanyama hao.

Kwani wanyama wengi uhitaji utulivu. Tujiulize kwa nini Mungu aliwatenga wanyama akawaweka eneo mbali na shughuli za binadamu? Mungu aliruhusu makabila machache ambayo katika tamaduni zao hawatumii ngoma ktk sherehe na uimbaji wao. Mfano wamasai. Wamasai wanaimba kwa sauti pekee ambazo uleta radha ya mziki hata kumfanya simba asinzie.

Wasukuma na wangoni wangeishi katikati ya Mbuga kama wamasai ingekuwa balaa kila siku ugomvi na wanyama. Make wana midundo mikubwa ya ngoma. Samahani watani zangu wasukuma na wangoni tunapenda ngoma zenu, msikasirike.

Nimewahi kuishi sehemu kuna machimbo, katika huo mji, milipuko ikitokea utadhani kuna bomu kubwa. Mji mzima unafunikwa na wingu kubwa la vumbi. Baadhi ya nyumba nyingi ubomoka na kupata nyufa. lakini pia watu walipata magonjwa ya moyo.

Kulikuwa na kesi za mara kwa mara hasa katika wilaya hiyo ambayo ni yawafugaji. Mifugo ilikufa mara kadhaa kwa kunywa maji katika bwawa ambalo maji yenye kemikali yalihifadhiwa. Unajua watu wa kule wanamifugo mingi hivyo wakati mwingine ni ngumu kuangalia mifugo yote unakuta inatawanyika hivyo na kwenda kunywa maji hayo yenye sumu. Mifugo mingi imepotea.

Si hivyo tu wakati wa mvua kuta au kingo za bwawa lenye maji ya sumu upata nyufa au kubomoka, na sumu utiririka na hivyo kuathiri wanyama na binadamu. Je huko mbugani itakuwaje? Ni kweli tunapenda urithi tulio kabidhiwa na muumba wetu?

Sasa najiuliza hii mifugo ya nyumbani iliathirika je, hao wanyama ambao wanajichunga wenyewe itakuaje? hata uweke nyavu wanyama wa porini watavuka tu. Mfikirie nyati na miguvu yake, mfikirie tembo na minguvu yake na wengineo wengi. Najiuliza tunaharaka ya nini kuchimba hayo madini yaliyoko mbugani.

Nyerere hakuwahi ruhusu yachimbwe, Mwinyi hakuwahi ruhusu yachimbwe, Mkapa hakuwahi ruhusu yachimbwe, Kikwete hakuwai ruhusu yachimbwe, hata magufuli pia. Rais wetu, tunakupenda ila kwa hili fikiria mara mbili. Ukishamruhusu mwekezaji, kila kitu kitaharibiwa hasa uasilia wa huko mbugani. Nimeona katika wilaya niliyoiongelea misitu na uoto mzuri wa asili umeteketezwa. Mhe. nafahamu unalijua hili vyema kabisa.

Kwanini madini yaliyoko mbugani yachimbwe? Sasa! Hatuhitaji jiwekea akiba? Hata mjerumani hakuwahi kuchimba madini yote kwa wakati mmoja. Alichofanya aliweka alama na kuchora ramani za siri niwapi madini yalipo. Hadi leo imebaki siri kwa Taifa hilo. Kuna sehemu kuna majoka makubwa na huko hakuingiriki. Nasi tujali madini yetu. Kwanini tuchimbe kila kitu?

Hivi huko mbugani madini yakiisha tukabaki na mashimo, tutafanya utalii wa haya mashimo? Au tunataka tengeneza Ngorongoro crater nyingine? ili tupate watalii? Itakuwa man made ngorongoro crater!

Ni fedha kiasi gani tutapata yakichimbwa? Nimekusikia unaongea hata ubia wa kampuni ya Twiga tulioingia umetaka kulegezwa kwa misimamo ili tupate hata hicho kidogo. Na Wasiwasi mkubwa Mhe. Rais juu ya kuruhusu uchimbaji huu mbugani kwa wanyama wetu.

Chondechonde! Hatuhitaji kuwekeza kila kitu. Hata baadhi ya nchi Ulaya na Amerika wanamadini lakini hawayachimbi yote. Wanamafuta lakini wameweka akiba kwa vizazi vijavyo.

Kuna nini huko? Wanyama wetu waanze kukimbia ovyo na kuhama mbugani, wapishane na migari mikubwa , wakutane na mashimo makubwa, hata kama ni underground, itakuwa vurugu kubwa. Ni mengi ya kueleza ila leo naomba niishie hapa. Hatuhitaji kuandamana kupinga hili, bali tunajua mama weye ni msikivu. Rais wetu unaetujali watanzania, jali na hawa wanyama.

Hapa nadhani hata mauaji ya wanyama, na usafirishaji wa pembe za ndovu na meno ya tembo utashamiri sana. Hawa hawa watakao chimba, wawekezaji. Mara nyingi machimbo makubwa wanakuwa na viwanja vyao; hivi wakiwa wamebeba hizo pembe au wanyama mtawaona. Nimejifunza wilaya moja ya machimbo. Madini yanaposafirishwa uwa hakuna cha polisi wala nini, wao wanakiwanja chao, na wanajua nini wanabeba.

Tafadhali Mhe. Rais tutunze haya madini kwa kizazi kijacho. tuache kwanza. Kwani hatuna ubunifu wa mambo mengine tukapata fedha mpaka tuanze kuingilia mbuga nzuri za wanyama wetu? Mbona kuna nchi hawana madini lakini ni wabunifu wa mambo mengine ili kuongeza pato la Taifa.

Naomba kuwasilisha, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wako mwananchi.
Mtasema na na kububujikwa na machozi ila MAMA SAMIA TUNAKUOMBEA UWE MALIKIA WA NCHI
 
Utalii sio wa wanyama peke yake. Morocco, Egypt na Dubai wana wanyama? Tatizo ni kama hayo madini yatachimbwa huku mnufaika akiwa mchimbaji na sio nchi. Kama sheria ya madini iko vizuri yachimbwe tu.
 
Moja ya uamuzi wa hovyo kabisa kutoka kwa kiongozi mkuu, sijui washauri wake ni akina nani?!.
Sio kila sehemu unawaza uwekezaji...athari zake ni kubwa tena endelevu kuliko faida utakayoipata.
Migodi inaenda sambamba na hekaheka nyingi ambazo hazifai kabisa katika hifadhi ya wanyama pori.
Hivi Sa100 anadhani marais walimtangulia hawakujua kwamba baadhi ya hifadhi kuna madini lakini hawakuthubutu kufanya anachotaka kukifanya??
Jamani washauri wa huyu mama ni akina nani hao wasio na uchungu na nchi yao???
Blasting za migodi anazijua kweli huyu?!.

Hata hivyo Serengeti iko ktk orodha ya urithi wa Dunia chini ya UNESCO hivyo hawawezi kukubali upuuzi huo wa kuanzisha mgodi wa dhahabu ndani ya Serengeti.
Kauli mbiu ya Serengeti ni Serengeti shall never die!!.
 
Hivi mkianza kulipua Baruti kwenye hìzo Mbuga za Wanyama kuna mnyama atabàkia?!
 
Nje ya mada, ktk nchi nyingi za Kiafrika ikiwamo Tz ni muhimu sana sana nchi ikapata Rais intelligent.
Nasema hivyo kwasabb washauri wa marais huwa wanaangalia boss anataka nn so watashauri kulingana na uelekeo boss anaotaka kuuchukua hata kama uamuzi huo utaigharimu nchi kwa ujumla wenyewe wataitikia tu NDIO boss.
Na hii ni hatari zaidi kwa nchi zenye katiba mbovu kama yetu inayomfanya Rais ni sawa na Mungu kwamba hakosei!!.
 
UCHIMBAJI MADINI KWENYE MAPORI YETU NDIYO ADUI NAMBA MOJA WA MAZINGIRA YETU, TUTAFAKARI KWA KINA!
/Makandarasi wa Tanzania waunga juhudi za rais wetu /

°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°

Umoja wa Wakandarasi na Wahandisi wa Tanzania wamemchangia Rais Samia Suluhu helikopta yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya shughuli za kampeni mwaka 2025.
 
Hata yakichimbwa bado nchi itapata faida kidogo sana. Mara ya mwisho nilisikia serikali inapata 4% ya mrabaha. Kuliko kuziua mbuga kwa madini yanayoisha na yasiyokuwa na faida bora tuendelee kuzilinda mbuga ambazo zina faida za moja kwa moja kwa mwananchi. Ninadhani mama hii 2025 inamletea mapichapicha.. ashauriwe.
 
Back
Top Bottom