eddymyinga
Member
- Feb 21, 2011
- 11
- 1
Kuanzi tar 27/11/2020 kumezuka shughuli za uchimbaji mchanga na uchukuaji mchanga wa Mto Msimbazi katika JIMBO LA SEGEREA - KATA YA KIPAWA - MTAA WA MOGO ENEO LA DARAJA LA SEMIMARI, wachimbaji mchanga wamesema wamepewa kibali cha kusafisha mto kitu ambacho raia wanao kaa eneo hilo na wa mitaa ya jilani, MAENEO YA UWANJA WA NDEGE ,KARAKATA MJIMPYA na KATA YOTE YA KIPAWA wamekua wakihofia shughuli hizo .Kuchukua mchanga kutoka kwenye mto kuna hatarisha sana kingo za mto na zinaweza kusababisha kuongezeka ( kupanuka kwa mto )
Mto msimbazi umekua na athari kubwa sana kwa wananchi na miundo mbinu ,hasa zaidi kipindi hiki kilicho kua na mabadiliko ya tabia nchi ,
Mto umekua ukifuata watu/Makazi ya watu kutokana na uchimbaji wa mchanga unaofanywa na watu ,na kwa sasa kampuni iliyo pewa kazi ya kusafisha mto kumbe wanaondoka na mchanga bila ya manufaa kwa waananchi na serikari
Tunaomba mamlaka husika ifuatilie swala hili ( NEMC ,watu wa mali asili na wizara ya madini ) kama ni kusafisha mto ,viongozi watoe elimu kwa wananchi kwa jinsi gani kingo za mto zitalindwa na hapatatokea uharibifu wa kimazingira na athari za kubomoka kwa kingo za mto .
TAHARIFA ZAIDI UTAZIPATA ENEO LA TUKIO NA WANANCHI WAISHIO ENEO HILO .